Duru : Utangamano, Amani na Ustawi. Taifa linaelekea wapi?

Duru : Utangamano, Amani na Ustawi. Taifa linaelekea wapi?

MAHAKAMA IJITENGE NA MITEGO YA SIASA
Wananchi wakipoteza Imani na Mahakama, wakimbilie wapi?


Kwanza, tunapo ongelea kesi ya Mh Tundu Lissu hatuongelei kosa analotuhumiwa nalo, tunaongelea mwenendo wa taratibu zinazotumika. Kwa namna yoyote hatutaongelea suala linalohusu kesi yenyewe.

Hatua za awali (committal) zimekamilika, kesi imepeleka Mahakama kuu. Hadi sasa haijapangiwa tarehe

Malalamiko ya Wananchi ni kuhusu cheleweshajwi wa kesi uliochukua zaidi ya siku 100.Lissu alipokamatwa ni dhahiri kulikuwa na ushahidi wa kutosha, lakini kwa namna ya ajabu sababu za kuahirisha kesi zikatolewa kila siku na kupata baraka za Mahakama. Sura inayojitokeza ni Mahakama ''kusaidia'' ucheleweshaji kwa hisia za ''kutumika''

Kuna kesi mbili Mahakamani zikihusu CHADEMA. Kwanza hii inayomhusu Lissu kwasababu ni mwenyekiti wa Chama.
Pili, inayohusu mgawanyo wa rasilimali za CHADEMA. Kesi zote mbili zina chembe za siasa ndani yake.

Nchi inaelekea uchaguzi mkuu October. Endapo kuna ushiriki au kutoshiri uchaguzi hayo yanahusu Vyama na Taasisi zinazosimamia chaguzi.

Kilicho wazi, ni msimu wa siasa za uchaguzi , Wananchi kupitia taasisi zao wana haki ya kushiriki siasa bila vikwazo.

Ucheleweshaji wa kesi kwa visingizio au kutozingatia hali ya Nchi kunapelekea hisia mbaya dhidi ya mifumo ya haki.
Kwamba kuna mbinu zinatumiwa ''kuzuia'' baadhi ya Taasisi kushiriki katika siasa kuelekea uchaguzi

Mahakama isiingie katika mtego huo, kuna uwezekano wa kumaliza mashauri kwa njia za dharura kwa kuzingatia hali ya nchi. Hii ina maana maamuzi yatoke kwa kuzingatia sheria bila kuathiriwa na udharura au hali ya siasa.

Hilo linawezekana! hoja kubwa ni kupatikana kwa haki ikimaanisha hatma ya kesi bila kujali matokeo
Hukumu zikitoka Mahakama itajivua lawama za 'siasa' zinazoelekezwa kwake na Umma.

Si kazi ya Mahakama kujua endapo CHADEMA watashiriki uchaguzi au la, ni wajibu wa Mahakama kufanya '' informed decision'' ili kulinda integrity ya Tribunal.

In public perception, the integrity and sanctity of judicial system is at an all time low!

Kama Taifa tunazuiaje uharibu zaidi?
 
MAHAKAMA NA KESI ZA KISIASA
Dhana zinaharibu taswira ya Mahakama
Kesi za CCM na CHADEMA !


Kuna dhana mbili kuhusu yanayoendelea Mahakamani na taswira iliyopo mbele ya jamii.

1. '' Preconceived notion'' kwa kiswahili ni kama 'ubashiri' wa jambo kutokea bila kuwa na ithbati au ushahidi wa kwanini itakuwa inavyodhaniwa. Ni mawazo tu kwamba jambo fulani litakuwa hivi au vile hata kabla ya kutokea

Mfano, mazungumzo ndani ya jamii ni Mahakama kutotenda haki kesi za kisiasa ikionekana 'dhidi' ya Wapinzani.

Uchaguzi wa 2020 uliokuwa mbaya na mbovu katika historia ya nchi yetu , hakuna kesi hata moja ya kupinga matokeo iliyopelekwa Mahakamani. Wapinzani walikuwa na 'preconceived noton' kwamba hakuna haki

Preconceived notion haitokei kwa bahati mbaya, inatokea pale dhana fulani inapopata ushahidi hivyo ushahidi huo hutumiwa kwa dhana ya matukio mengine ambayo hayajatokea wala hayana ushahidi.

2. Conspiracy theory (CT), dhana- kwamba kuna jambo la siri linafanywa na taasisi fulani kwa lengo fulani.
CT haitokei hewani, ina ukweli unaotangulia na ukweli huo ima hufanyiwa hila ''distortion' au unajengewa nadharia kutokana na mazingira fulani.

Mfano, kuna CT kwamba Mahakama zetu kwavile mfumo wake mzima ni 'tegemezi'' kuanzia rasilimali fedha na Watu, ,Mahakama hazitendi haki hasa kesi za kisiasa zinazohusu Wapinzani.

Preconceived notion na conspiracy theory zinapotawala maongezi, hata pale Mahakama zinaposimamia utoaji wa haki kikamilifu ''to the letter'' dhana hizo mbili haziipi Mahakama taswira nzuri mbele ya jamii

Chanzo cha dhana hizo mbili ni kipi?
Mahakama kwa nyakati fulani imepoteza Uaminifu '' credibility and integrity'' kwa maamuzi yanyotolewa.

Mfano, Mahakama iliposema '' Wakurugenzi wasimamie uchaguzi kwasababu wanakula kiapo'' ni hukumu ya hovyo!
Ni hukumu iliyolenga kuisaidia serikali na CCM kwa ujumla hata kwa mtu asiye na elimu kabisa, achilia ya sheria

Viongozi wa dini wanakula viapo mbele ya Mungum bado wanafanya uhalifu.
Viongozi wa siasa wanakula viapo kila uchao lakini bado wanafanya uhalifu.
Maamuzi ya eti watatenda haki kwa kula kiapo yameipotezea Mahakama ''integrity and credibility''

Tuangalie kesi zilizopo Mahakamani. Kesi inayohusu CCM kutofanya uchaguzi kwa njia halali, imepangiwa Jaji na tayari hukumu imetoka. Kesi zinazohusu CHADEMA zinapigwa kalenda na ubabaishaji tunaouona bila elimu ya sheria

Kuna uwezekano kesi za CCM zina mtazamo unaoruhusu kufanyiwa maamuzi haraka tofauti na za CHADEMA, hata hivyo kwa uchechefu unao onekana Mahakamani, ni haki kwa wenye ''preconceived notion and Conspiracy theory'' kunyooshea vidole Mahakama kwamba haitendi haki kwa makundi fulani ya jamii

Ni kwa msingi huo, tunaiasa Mahakama kwamba kile kidogo kilichobaki katika ''credibility and integrity'' kisibomolewe zaidi kwa kesi za kisiasa. Katika msimu huu wa siasa za uchaguzi, maamuzi yatolewe bila kujali ni ya aina gani

Kuahirisha kesi na kupoteza muda kunajenga conspiracy theory kwamba Mahakama ni sehemu ya kile kinachodaiwa uwepo wa '' cable'' kusaidia uchaguzi kwa baadhi ya vyama. Hata kama si kweli, madhara ya conspiracy theory husambaa kama moto wa nyika.

Mahakama isifike huko, kwani ni kimbilio la mwisho. Wananchi wakichoka na kukata tamaa na Mahakama, matokeo yake si mazuri! yana madhara

Kama Taifa tunaelekea wapi?
 
Back
Top Bottom