Duniani kuna mengi sikutegemea hili kunipata

Toa vielelezo kamamoja alivyosema.Itasaidia sana.Kama hujui.namna ya kutumia.Mtafute MTU yeyote Pm Mwombe no.Ya Whatsaap.Mtumie vielelezo.kwa.njia ya Whatsaap ambayo ni rahisi.Then yy ataweka hapa.Mana kuweka hapa ni ujuzi mwingine.Wengi hawajui.
 
Utapata matibabu vizuri kabisa kwa kutumia bima ya afya kwa hiyo 76,500 kwa mwaka
Hebu nieleweshe hii njia inavofanya kazi naweza nikamlipia hio nina ya afya!! Please reply
 
Duuu pole sana mkuu nimehuzunika sana usijali MUNGU mkubwa atakufanyia wepesi
 
Matibabu pale ocean road naambiwa ni kama bure vile!
Sina uhakika.
Pole kwa mtihani unaokukabili.
Bure za kwenye makaratasi tu ndugu mwimbili kwenyew wanasema almost free ukiulizia unaambiwa 8m
Mungu amjaalie ndugu yetu uyo apate matibabu
 
Nimependa ulivyo waza
 
Inawezekana wala hawezi kufanya hizo mambo mkuu,km kweli Mungu kakuelekeza kwake nakushauri umpigie umuelekeze pa kukukuta na umweleze aje na viambatanisho vyote vya Hospital, ikibidi kuanzia vile vya Temeke,Muhimbili hadi Ocean road,....naimani utapata malipo makubwa mbele za Mungu.
 
Mkuu sis ni vijana wenzako na wengine ni wazaz wako tunapenda sana kukupa msaada kaka yetu mpendwa kwa sababu tumeguswa na tatizo lako kama member mwenzetu..tunaomba tu uweke document za matibabu hapa ili tuthibitishe na tuweze kukusaidia kwa tulichojaliwa.kukwambia uweke document haina maana ya kukudhalilisha bali ni sisi kua na aman na jinsi ya kukusaidia ndugu yetu..tunakuomba tafadhali weka documents tuthibitishe huwezi jua mwenyezi mungu akawa amepanga tukusaidie hapa jamii forums
 
Naomba ujibu maswali haya..
Maumivu yako yakikushika je hua unatapika?
Ukitapika tumbo linatulia?
Wakati wa maumivu unasikia kizunguzungu?
 
Pole kwa shida unayopitia, lakini nina mashaka makubwa kama Kweli wamegundua una kansa ya utumbo mpana(ca colon) Kwa sababu ya umri wako. Aina ya kansa iyo uwapata wazee ambao umri umekwenda Ie above 60.Yawezekana ukawa na vivimbe tu kwenye utumbo mpana ambavyo havijabadilika kuwa kansa.
Kama ni Kweli umekutwa na iyo kansa yawezekana ukawa wa kwanza kwa umri huo kukutwa na ca Colon.
Ata hivyo uwezekano upo wa kupata kansa ya colon kwa umri mdogo, hivyo basi weka documents mbambali kuthibitisha hilo ili tuwe na imani ya kuchangia.
Cha muhimu weka vielelezo ili tuwe na imani zaidi
 
Pole rafiki.. Ukifuata ushauri naamini utapona,tuko pamoja.
 
Mimi pia nitamchangia nikiona vithibitisho,mjini sasa kumeharibika.
 
kwa kuwa upo dar nakushauri pambana nenda kwa rc makonda,nakuhakkishia ukikutana nae tuu jua, umesaidiwa, pia afya ndo kila kitu ndugu, kama we ni muislamu au mkiristo shiriki kwenye nyumva za ibada omba nafasi kwa waumini, jieleze hela unayoihitaj n ndogo tu watakuchangia;! NB; fanyia kaz
 
 
Pole sana huwa kuna usemi wa kizungu unasema Nothing just happen. Mungu ataonesha njia Hakika.
Pole sana .
 
Huyu mgonjwa hajarudi tena? Amekwamia wapi?
 
Pia amtafute humu kuna member mwenzetu anaitwa FADILI PAUL, huyu ana utaalamu wa tiba hizi za kawaida za kutumia vyakula na majani.
Kuna dawa aliwahi kuizungumzia ni very simple,ni majani ya mstafeli, alisema ni tiba nzuri ya aina nyingi za kansa.
Kwa hiyo namshauri awasiliane nae anaweza kumpa ushauri utakao leta faraja kwake.
Pia aingie youtube aandike SOUR SOUP ataona hayo majani nisemayo,lakini ni bora sana awasiliane ma huyu member mwenzetu kwa kuwa anweza mwelekeza namna ya kufanya.
Huo ndio mchango wangu kwa member mwenzetu huku nikimtakia afya njema ma matumaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…