Duniani kuna mengi sikutegemea hili kunipata

Duniani kuna mengi sikutegemea hili kunipata

Nimeishia Kuhuzunika tu........ nisijue cha kufanya Ufukara Mbaya sanaa.........................!!!!!!
Ni kweli inahuzunisha lakini tusiishie hapo, hebu tuone nini twaweza fanya kumsaidia huyu member mwenzetu.
 
Ocean road kwa matangazo ni bure ila pata mgonywa au umwa uende hapo utajuta kuzaliwa hakuna cha bure pale ndugu zangu watanzani vitu vya bure pale ni vidogo vidogo sana hakuna dawa za kumpa mtu bure pale za bei kubwa utapewa panado hata dawa ya kikohozi benline hawana utaambiwa ukanunue hapo nje duka la dawa na nje inauzwa 14500 ni hatari sana
Ni kweli usemayo mkuu, mimi nilikuwa na mgonjwa pale akaandikiwa dawa ambapo ilitakiwa awe anapatiwa dozi kila baada ya muda fulani, kila dozi ilikuwa 420,000/= ilikuwa kazi kweli kweli, maana dozi zilitakiwa ziwe nne, sasa jumlisha mwenyewe hicho kiasi mara nne
 
H
Ndugu wana JF habari zenu ,poleni kwa kazi na majukumu mbalimbali ya ujenzi wa taifa.Nimeamua kuchukua uamuzi huu mgumu wa kuwashirikisha maisha yangu pengine naweza kupata faraja maana ni mzigo ambao unazidi kunielemea kadri siku zinavyozidi kwenda. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28 nina mke na mtoto mmoja na naishi maeneo ya mbagala Dar es laam nikijishughulisha na kazi za ujenzi wa nyumba ,kama msaidizi wa mafundi ujenzi.

Stori yenyewe ni hii, toka mwaka 2014 nimekuwa najisikia maumivu makali sana tumboni ambayo huwa yananipata kwa muda na kupotea, hivyo sikufuatilia sana nikijua labda ni tatizo la kawaida tu maana maumivu yenyewe hunipata na kupotea hata kwa miezi kadhaa, lakini kadri ya siku zilivyozidi kwenda ndipo maumivu haya yaliendelea kunisumbua mara kwa mara na pia ikajitokeza tatizo la tumbo kujaa gesi ,baadhi ya watu wakaniambia labda nitakuwa na vidonda vya tumbo na kunishauri kuepuka vyakula aina fulani na kula aina flan flan pia kuzingatia mda wa kula kuepuka kushinda njaa nilifanya hivyo bila mafanikio yeyote baadae nikaenda kituo cha afya cha jiran nilivyowaeleza pia wakaniambia kuwa ni dalili ya vidonda vya tumbo wakanipatia utaratibu ambao niliufuata lakini sikupata nafuu maumivu yaliendelea japo yalikuwa yakipotea na kuyasahau lakini baadae yananirudia na kuathiri shughuli zangu za kujitafutia mahitaji.

Kufika mwezi wa nane 2017 ,nikaamua kwenda kupata vipimo zaidi maana tatizo lilizidi nikawa napungua uzito pamoja na kuanza kuona damu kidogo nyeusi kwenye haja kubwa, ilinishtua sana hali hii nikaamua niende hospitali ya Temeke kupata vipimo zaidi.

Baada ya vipimo Temeke wakanipa rufaa ya muhimbili, nikaenda muhimbili wakanifanyia vipimo , majibu yake ndio yaliyonifanya niandike hapa ,nilipata mshituko mkubwa sana nilivyoambiwa kuwa nina kansa ya utumbo mpana (colon cancer ) na iko stage IIA. wakaniambia watanitransfer ocean road nianze matibabu mara moja ambapo yatahusisha operation.

Kwakweli toka siku hiyo nimekuwa ni mtu wa kuchanganyikiwa nisijue la kufanya nikiangalia maisha yangu mimi ndio tegemeo la mama yangu huko kijijini pamoja na familia yangu hapa mjini na maisha yangu yanategemea kazi zangu hizi za kutumia nguvu nitawezaje kupata matibabu na hata baada ya matibabu nitaendeshaje maisha yangu, kwanini mungu ameamua kunipatia haya majanga katika umri wangu huu mdogo nikiwa mwenye majukumu mengi na kutegemewa sana na familia yangu ,hata hivyo sina uwezo wa kulaumu wala kujua mpango wa Mungu katika maisha yangu.

Nimeshindwa hata kumjulisha mama yangu kijijini maana najua nitamwongezea msongo wa mawazo tu. Nimejaribu kuwaomba ndugu marafiki msaada ambapo napata ahadi tu bila msaada na siwezi kuwalaumu maana natambua hali zao pia.

Nimekuwa nikitumia dawa ambazo ni za maumivu tu, nikiendelea kutafuta hela za matibabu japo hii hali imeathiri sana sana kazi zangu na kipato changu pia ila sina namna nyingine siwezi kufa nimekaa bora nifie kazini .Hela niliyoambiwa inahitajika kwa matibabu ya awali na operation ni sh.593,000/=ndio ambayo bado nahangaika kuitafuta japo nianze matibabu japo sijui nikiwa kwenye matibabu familia yangu itaishi vipi maana bila kutoka kutafuta chochote hata chakula itakuwa ngumu kupatikana na kazi zangu ni za kutumia nguvu .

Hivyo ndugu zangu NIMEAMUA NIWASHIRIKISHE WATU WENGI ZAIDI KUHUSU TATIZO LANGU MAANA SIWEZI KUJUA NI WAPI NAWEZA KUPATA MSAADA AMA FARAJA.Nimekaa nalo naona msongo wa mawazo unanizidia nimeamua kushirikisha watu naweza pata ushauri, faraja ,matumaini ,kukutana na walio wahi kupata tatizo kama langu na kufarijiana na hata msaada pia kwa atakayeguswa na shida yangu akanichangia atakachojaliwa kikanisaidia pia katika hali yangu ngumu.

Kwa atakaye guswa na hali yangu anaweza kunisaidi atakachojaaliwa chochote namba yangu ni [HASHTAG]#0678856312[/HASHTAG] jina Fidelis peter.nitashukuru sana.

Samahanini sitaweza kuwa online mara nyingi maana naingia kwa kutumia computer ya rafiki yangu sio mara zote naweza kuwa naye karibu nilikuwa na smartphone nikaiuza kutokana na tatizo hilhili ili kusaidia familia maana kazi zangu zimeathirika sana.


Asanteni ,
Pole sana ikiwa ni kweli unachosema. Umeandika kwa usitadi wa hali ya juu. Lakini huenda utahitaji namna bora zaidi kuthibitisha madai haya.
 
Pole sana Kaka. Nakushauri Umtafute FLORA LAUWO Wa kipindi cha "NITETEE SAUTI YA WANYONGE". Nauhakika kupitia yeye/kipindi chake utapata msaada Wa HARAKA SANA. POLE SANA, MUNGU AKAENDELEE KUWA UPANDE WAKO DAIMA
 
Matibabu pale ocean road naambiwa ni kama bure vile!
Sina uhakika.
Pole kwa mtihani unaokukabili.
Sio kweli mkuu, pale ocean road kama pesa huna utafia sakafuni. Fanya utafiti!!
 
Ni kweli inahuzunisha lakini tusiishie hapo, hebu tuone nini twaweza fanya kumsaidia huyu member mwenzetu.
kusaidia hapo panahitaji CHAI na siyo Pole tu..........Ni yale yale ya Ufakiri................!!!!
 
Mkuu pole sana na kuumwa nasi pengine tunaumwa lakini hatujajua Tu. Cha msingi weka uthibitisho wa vielelezo vya ugonjwa Kama barua za rufaa na majibu ya vipimo pamoja na kitambulisho chako Ili tuamini maana matapeli wengi nowdays. Binafsi ntakuchangia elfu 10 endapo ntapata uthibitisho wako
 
Kwanini haweki vielelezo na amepotea mazima? No offense, ila nadhani jibu linaweza kuwa computed hapo chini

-New member
-28 yr old
-married with one kid
-anakaa mbagala
-msaidizi wa Fundi ujenzi
(natamani kuelewa zaidi hapa)
-amegundulika na kansa
-aina ya uandishi (hii ni give-away kwa scenario hii, ya "kibarua wa Fundi")

-angalizo maana anatumia pc ya rafiki yake atakuwa hapatikani.



Pole sana
 
Si kasema hana smartphone,hivyo anaingia Jf kwa kuomba laptop ya jamaa, so subirini atawajibu,au bora mumpigie
 
Pole sana...matatizo tumeumbiwa wanadamu binafsi nitakusaidia nilichoojaliwa
 
Pole sana, mungu akusaidie na kukuponya. Mimi nipo tayari kukuchangia hela ya matibabu na pia kukuombea mchango from my coworkers, kama hutojali kuweka wazi vielelezo vitavyosaidia kuthibitisha ukweli wa hii habari. eg. makaratasi ya huko hospitali ocean road re: the diagnosis and required treatment
Hapo umeongea vyema sana aisee,me pia am in
 
Pole sana, mungu akusaidie na kukuponya. Mimi nipo tayari kukuchangia hela ya matibabu na pia kukuombea mchango from my coworkers, kama hutojali kuweka wazi vielelezo vitavyosaidia kuthibitisha ukweli wa hii habari. eg. makaratasi ya huko hospitali ocean road re: the diagnosis and required treatment
Ukipata uthibitisho wa hii issue nijulishe pia nione tutamsaidiaje.
 
Kwanini haweki vielelezo na amepotea mazima? No offense, ila nadhani jibu linaweza kuwa computed hapo chini

-New member
-28 yr old
-married with one kid
-anakaa mbagala
-msaidizi wa Fundi ujenzi
(natamani kuelewa zaidi hapa)
-amegundulika na kansa
-aina ya uandishi (hii ni give-away kwa scenario hii, ya "kibarua wa Fundi")

-angalizo maana anatumia pc ya rafiki yake atakuwa hapatikani.



Pole sana

Kwa mwandiko huu, inawezekana alifaulu vizuri sana kidato cha nne akakosa ada ya kwenda shule.
 
Pole ndugu, zaidi MUNGU ndo kimbilio lako na ndo faraja ya kweli kwako tafuta faraja iliyo ya kweli kutoka kwake yeye ndo kimbilio kwa ote na usihofu atakuponya.
 
Back
Top Bottom