Kuna tofauti Kati ya neno “faith” na “beliefs”. Pamoja na uelewa wangu mdogo wa mambo ya kidini na elimu dunia. Binafsi fikra zangu huteseka sana kuhusiana na mapokeo ya kiimani. Imani ya kuamini kuwa ipo nguvu inayotuweka duniani naamini 100%. Neno linalofuata kwangu. Je! Ni lazima kuwa na imani ya kidini.? Halo nakosa jibu kwa mitazamo ya kielimu, ni kuwa dini hizi tulizo nazo tulizipokea toka kwa wakoloni walioitwa missionaries. Tukaacha ya kwetu hatimae tukashika ya wakoloni. Ninapochanganyikiwa kabisa dini hizi tumezishika kuliko wenye dini. Imani hizi kwetu ndio uponyaji, nguvu za kiuchumi na maisha ya baadae baada ya kuacha ulimwengu huu . Najiuliza tungebaki na zile imani za zamani tungekuwaje hizi sasa. Je nisipofuata imani hizo itakuwaje! Imani kwangu ni jambo zito naombeni uelewa zaidi.
Andiko lako ni zuri.
Kwa kweli huwa siwaelewi watu wanaodai kuwa tulikuwa na dini yetu (zetu) Afrika. Naweza kusema ni suala la uelewa.
Dini ni utaratibu wa kutekeleza mambo au vitu vitakatifu.
Tunaposema dini tofauti na imani tunazungumzia watu "waliotengwa" na "kuingizwa" kwa kufanyiwa tendo la kidini na kiliturujia la sakramenti, baraka na wakfu linalompatia mtu uwezo wa kutekeleza uweza mtakatifu, ambao hauwezi kutoka mahali pengine popote isipokuwa kwa Mungu.
Yako mambo au vitu ulimwenguni haviwezi kufanywa na kila mtu isipokuwa na watu tu waliopewa mamlaka hayo. Ziko kazi ili kuweza kuzitekeleza lazima kuacha mambo mengine yote ya maisha kwa ajili ya kazi hiyo.
Utaratibu huu sio wa nyakati zetu. Haukuanza wakati wa sheria ya Kristo au wakati wa Musa -sheria ya Musa. Ni utaratibu wa wakati wote. Hivi ndivyo maisha ya mtu (binadamu) yalivyo tangu kuwepo kwake na ni wa mahali pote duniani.
Wafrika wanadai waalikuwa na dini zao kabla ya kuja wamisionari (Ukristo) Afrika. Hii ni kweli.
Lakini kitu Wafrika wanafanya makosa ni kushindwa kuelewa kuwa hata wamisionari (wazungu) nao walikuwa na dini zao.
Hapo hapo, makosa mengine wanayofanya Wafrika wanaodai walikuwa na dini zao ni juu ya namna walivyokuwa wanafanya au wanatekeleza matambiko (kutolea sadaka) ya dini yao na namna dini ya kikristo inavyofanya au kutekeleza tambiko-kutolea sadaka.
Ukichunguza madai hayo ya hao wanaojiita wafrika unagundua ni upotoshaji wenye malengo na tamaa ya uchumi na utawala.
Hakuna ukweli wowote kwamba Wafrika walikuwa na dini zao ambazo jamii za maeneo mengine hawakuwa nazo, hakuna!
Utaratibu wa dini hata kama ni ya uongo ni mmoja, unafanana pote duniani.
Dini ni watu waliopewa na Mungu mwenyewe mamlaka ya kutekeleza uweza mtakatifu; uwezo wa kufanya mambo matakatifu.
Mtu anaweza kuwa na imani lakini sio kila mtu anaweza kutekeleza uweza mtakatifu. Kwa mfano kutolea sadaka au tambiko anatakiwa mtu aliyetengwa na kuingizwa kwa kuwekewa mikono mitakatifu kwa ajili ya dini.
Tufahamu kwamba kutolea sadaka au matambiko ni mambo au vitu vitakatifu. Haya ni mambo ya akili, matakatifu.
Aidha mafundisho ya imani na maadili ni mambo ya akili matakatifu. Hapa moja kwa moja tunaona Kanisa ambalo ni mamlaka ya dini.
Yesu angeweza kusistiza au kusema tu juu ya imani kama kitu pekee anachotakiwa mtu kuwanacho.
Lakini pamoja na kufanya hivyo kusema juu ya imani, Yesu aliweka Kanisa -mamlaka ya dini. Kwa nini? Kwa sababu imani ni pia pamoja na watu waliotengwa na kuingizwa kwa kuwekewa mikono mitakatifu tendo la kidini na kilitirujia la sakramenti, baraka na wakfu linalompatia mtu uwezo wa kutekeleza uweza mtakatifu.
Kama hatujifunzi maana yake hatuwezi kuwa na imani pia hatuwezi kuijua dini.
Wafrika hatufahamu dini tunayosema "Dini Yetu" ndio sababu tunasema dini ya wazungu. Kama tungeifahamu vizuri dini tusingesema hii ni dini yetu na hii ni dini yao.