Duniani kote hakunaga maandamano ya hivyo

Duniani kote hakunaga maandamano ya hivyo

Hapa CCM ilipofikia hata wenyewe wanajua kuwa nikwaneema tu .
Kwa takribani miaka 30 sasa CCM imekuwa inashindana na nyakati. Mpaka sasa wapo madarakani kwa sababu ya hadaa, janja janja na uhuni wa kila aina.
 
Sa
Matukio mengi yametokea ambayo yangeweza kuwafanya watanzania waonyeshe wazi hisia zao ila kimya.
sa kwa nini wewe inakufanya uhangaike kuwahimiza waendelee kuwa kama unavyotaka wewe.
Hawa waTanzania umewashikia akili zao wote kwamba kila mara utajuwa ni kipi watakifanya?

Kwa nini unataka wafanye unavyotaka wewe?
 
Hayo maandamano yasingekuwa na tija au kuwasumbua akili tusingeona maafisa wa ubalozi pale wakilipa magenge ya wamexico kuja kufanya maandamano.

Picha & video zipo walipoongeleshwa hata salamu tu ya kiswahili hawakuweka kujibu.

Basi msingetumia kodi za watanganyika muache maandamano yaliyofeli na yasiyowasumbua ili tujionee sote.
 
Kabla haujasoma ninachotaka kusema, embu tuelewane kidogo. Sijawahi kuisifia wala kuitetea CCM na serikali zake. Siungi mkono vitendo vyovyote vya unyanyasaji, utekaji, mauaji na uminywaji wa haki na uhuru wa raia wa Tanzania. Baada ya kusema hayo, naomba niendelee na mada yangu ya leo.

Hauwezi kutangaza takribani miezi miwili kabla kuwa unaenda kufanya maandamano ambayo nia yake ni kuiondoa serikali halafu uende kufanikiwa. Hivi mnadhani miezi hii yote hao CCM na serikali yake wamekaa tu wanawasubiri nyie hiyo October 29 muende kuwaondoa?

Maandamano ya kweli, yenye nguvu na yanayofanikiwa huwa yanaibuka tu "organically" na yanachochewa na hasira na hisia kali kutokana na matendo maovu ya wakati husika siyo haya ya kutangaza miezi miwili kabla.

Kwa Tanzania yametokea matendo mangapi ambayo yangeweza kuibua maandamano lakini kimya kikatanda mitaani hadi watu wakapoa? Watu wamebaki kugugumia na kunong'onezana tu ila hakuna action. Nguvu hiyo ya kuwavuta hao watu waingie road itatoka wapi wakati mmewapa watesi wenu muda wa kujiandaa na kujizatiti na wakati huo huo hisia za watu kupungua?

Kuna jambo nililisema kuhusu Polepole, Mpina na Mange wiki kadhaa nyuma katika post yangu ya mwisho na nasimama na maneno yangu maana baada ya nilichoandika ndiyo siku kadhaa nikasikia "ametekwa". Nasimama na kauli yangu ya awali.

Narudia jambo ambalo nimelisema mara kwa mara. Watanzania bila kuamua kusimama wenyewe bila kutegeana au kutegemea viongozi au watu fulani wawaongoze (au sasa hivi mmeingizwa chaka la eti jeshi lipo tayari kuwasaidia), hamtaiondoa CCM kamwe.
Maandamano ya kutangaza ni yale ya amani kama enzi za kuunga mkono azimio la arusha.
Labda haya maandamano kama ya oktoba 29 ni jitihada za kuwapa uelewa kidogokidogo wabongo kwamba ndo silaha inayoogopwa sana na watawala kote duniani. Wakishaanza kuelewa hivyo watajua huko baadaye jinsi ya kuitumia. Nakingine nadhani bongo hatujaweza kupata bahati ya watu wenye vipaji vya kuambikiza hasira zao watu wengine.
 
..mapokezi ya Lissu, na maandamano ya Ngorongoro, ndio maandamano makubwa yaliyofanyika katika awamu ya 5, na awamu ya 6. Hoja yangu ni kwamba maandamano Tanzania yanawezekana.
Yalifanyika kwa sababu waliruhusu yafanyike aseeee
 
Kabla haujasoma ninachotaka kusema, embu tuelewane kidogo. Sijawahi kuisifia wala kuitetea CCM na serikali zake. Siungi mkono vitendo vyovyote vya unyanyasaji, utekaji, mauaji na uminywaji wa haki na uhuru wa raia wa Tanzania. Baada ya kusema hayo, naomba niendelee na mada yangu ya leo.

Hauwezi kutangaza takribani miezi miwili kabla kuwa unaenda kufanya maandamano ambayo nia yake ni kuiondoa serikali halafu uende kufanikiwa. Hivi mnadhani miezi hii yote hao CCM na serikali yake wamekaa tu wanawasubiri nyie hiyo October 29 muende kuwaondoa?

Maandamano ya kweli, yenye nguvu na yanayofanikiwa huwa yanaibuka tu "organically" na yanachochewa na hasira na hisia kali kutokana na matendo maovu ya wakati husika siyo haya ya kutangaza miezi miwili kabla.

Kwa Tanzania yametokea matendo mangapi ambayo yangeweza kuibua maandamano lakini kimya kikatanda mitaani hadi watu wakapoa? Watu wamebaki kugugumia na kunong'onezana tu ila hakuna action. Nguvu hiyo ya kuwavuta hao watu waingie road itatoka wapi wakati mmewapa watesi wenu muda wa kujiandaa na kujizatiti na wakati huo huo hisia za watu kupungua?

Kuna jambo nililisema kuhusu Polepole, Mpina na Mange wiki kadhaa nyuma katika post yangu ya mwisho na nasimama na maneno yangu maana baada ya nilichoandika ndiyo siku kadhaa nikasikia "ametekwa". Nasimama na kauli yangu ya awali.

Narudia jambo ambalo nimelisema mara kwa mara. Watanzania bila kuamua kusimama wenyewe bila kutegeana au kutegemea viongozi au watu fulani wawaongoze (au sasa hivi mmeingizwa chaka la eti jeshi lipo tayari kuwasaidia), hamtaiondoa CCM kamwe.
THE REVOLUTION WILL NOT BE TELEVISED 😂😂😂😂
 
Yalifanyika kwa sababu waliruhusu yafanyike aseeee

..Waliruhusu vipi wakati Wamaasai hawakuomba kibali kuandamana ktk geti la hifadhi ya Ngorongoro?

..Polisi wakizidiwa huwa hawana jinsi zaidi ya kusalimu amri.

..kule Ngorongoro Polisi walizidiwa na Wamaasai ikabidi wawe wapole.

..Ndio maana wakatumwa Wazee Kabudi na Lukuvi kwenda kuwabembeleza Wamaasai.
 
Maandamano yaliyopangwa ni ya kipuuzi. Sababu za maandamano ni nyingi zisizoeleweka kiasi kwamba ukizisoma hadi uzimalize tayari umesahau sababu ya kwanza. Wapinzani angalau wangekuwa na akili wangesimama na sababu moja nzito inayoeleweka. Haiwezekani mtu unasema sababu ni kupinga utekaji mara hapohapo sababu nyingine ni kuitoa CCM madarakani na ghafla sababu inaibuka kutaka reforms za uchaguzi. Yaani ujinga mtupu. Hawajui wanataka kuandamana kwa sababu gani.
Una uwezo mdogo wa kufikiria, ila jua wanao Andamana sio wapinzani ila ni Wananchi wenye Takwa lao
 
mkuu Bongo hakuna maandamano, wewe umeskia wapi maandamano ya kuiondoa serikali yakawa hivyo?
 
Punguza ushauri kwenye mambo ya Gen Z , sisi wazee tumeshindwa tuwaache vijana nao wajaribu
 
Back
Top Bottom