sweetlady
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 16,947
- 8,409
Mbona sijaona kama ni ya cnn? Au zipo mbili?
Umeona ni ya nini?
Inaonekana vizuri tu mbona!
Mbona sijaona kama ni ya cnn? Au zipo mbili?
Mwangwi wa mauaji ya kinyama na kikatili yaliyofanywa na jeshi la polisi mkoani Iringa sasa umeenea dunia nzima.
Shirika la habari la Marekani CNN limeripoti tukio hilo kwa kina na uhalisia wa pekee.Shirika hilo pia limeelezea matukio yote ya mauji ya kinyama yaliyowahi kufanywa huko nyuma ambayo yote yalikuwa ni kuidhibiti demokrasia na kutaka kukifunga mdomo chama kikuu cha upinzani CDM.
Shirika hilo pia limeeleza kushangazwa na ukimya wa tume ya haki za binadamu nchini Tanzania kufumbia unyama huu.
Habari kamili soma link ifuatayo:
Tanzanian journalist killed; Police under fire! - CNN iReport
sijui kwa kweli nieleweshe... kuna news na report?Hiyo linki uliyowekewa ni page ya wapi dada?unaweza kuisoma hiyo web address?unajuwa kuhusu ccnireport?
hujambo wewe ? miss u dearlyUmeona ni ya nini?
Inaonekana vizuri tu mbona!
Kuna taarifa kuwa Al Jazeera nao wameahidi kutoa ripoti maalum juu ya mauaji ya Raia nchini Tanzania.
Molemo tanx brother,nimesoma hiyo report ya cnn mara tatu na nimegundua hao waandishi habari ya nje ndio wazalendo kuliko wa kwetu,na nimegundua pia mwanahalisi ilikuwa inatupa ukweli 100 %,habari iko open and clear sasa soma hivi vigazeti uchwara vya bongo...
poa tutaonana mtaani kwetu kuna kitu namalizia hapa nakujaMiss u more dearest
Am good sijui wewe!
hapo kwenye red/underline ni lazima siku ipo na endapo wahusika watakuwa hai basi lolote linawezekana. raisi wa zamani wa Kenya (Moi) ana pesa za kutosha lakini kwa sasa hana raha kutokana na makosa aliyoyafanya akiwa ofisiniImekaa hivi
In the past year or so there have been almost seven incidents where the police have used excessive force against unarmed men. All this has happened whenever CHADEMA has tried to conduct a peaceful march or a political rally. No police officer has been held accountable in any way. Tanzania's Attorney General Office has been silent and the national Human Rights Commission has not issued any statement of concern with the growing use of force by the police against unarmed individuals. Efforts to reach Iringa regional Police Commander Mr. Michael Kamuhanda proved to be futile. It was Mr. Kamuhanda who was Ruvuma Regional Police Commander when in February this year four people were killed by police.
CHADEMA's leadership was not available immediately for their reaction of today's incident.
soma heading we kijakazi usiyetumia akili!tangu lini "dunia" ndo wazungu?cnn inatizamwa dunia nzima wakiwemo hao dhaifu anaowapeleka bakuli la kimatonya every now and then.Mbona husemi kitu akiwa anapiga kiguu na njia kwa hao wazungu kuomba pamoja na vitu vingine hizo silaha zinazotumika kuuwa raia wasio na hatia?tumia akili na fikiri kabla ya kubandika ***** humu.Mwafrika habadiliki na wala hajifunzi kitu na siku zote tutabaki kuwa watumwa na kutawaliwa hata tufanye nini kwa maana tumeshindwa kutambua mawe yaliyowekwa mbele ya njia tunayopita na hao hao ambao tunawalilia waje watusaidie!
Watu wanalilia wazungu waseme chochote kuhusu mauaji ya Serikali dhidi ya raia, sasa sijui wakishasema ndio iwe nini? tangu lini hii Dunia ikawa fair?
Hivi mnafikiri hao wazungu mnaowaomba waseme kitu hawajui nini kinaendelea Tanzania? Kama wanaweza kujua kifo cha Raisi wa nchi nyingine kabla nchi hiyo haijatangaza watashindwa kujua kupigwa risasi kwa raia wasio na hatia?
Kwa nini siku zote tunategemea mtu mwingine ndio aje atusaidie? Kama kuna binadamu mwenye experience mbaya na wageni ktk histora ya Dunia hii ni sisi Waafrika hakuna watu waliodanganywa na kutumiwa vibaya na wageni kama sisi Waafrika kutoka Utumwa, Ukoloni mpaka Dini lakini bado tu tunafikiri nakuamini kwamba wazungu wanatupenda sana na watakuja kutetea!
Hivi ni nini kifanyike ili tuelewe Dunia hii its all about interest? Unafikiri Wazungu au sijui Wachina au Wajapani wanaweza kuja kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu kama maslahi yao hayaguswi?
Tubadilke tutafute suluhisho ndani ya mipaka yetu, Wazungu HAWAJAHI KUTUPENDA HAWATUPENDI NA HAWATAKUJA KUTUPENDA na mtaandika Barua sijui CNN sijui BBC sijui Radio China lakni kama maslahi yao yako intact hakuna lolote litakalofanyika!