Dunia sio duara, wala haina obiti ya kuzungukia

Dunia sio duara, wala haina obiti ya kuzungukia

Mkuu tuseme geograpy, physics vyote hivi hukusoma kabisa wewe...umesema ni elimu imeletwa...hvi hujui saiv kwenye ISS watu wanaiona dunia ilivo bila kutumia camera....?sidhan ata kama unajua ISS ni nini
 
wala husiangaike mkuu hebu tupe picha mbili tutakuelewa bila mzozo.
1. picha ya mbele ya dunia.
2. picha ya nyuma ya dunia.

Hahahahaaaa., Picha ya mbele ipo hapo juu, picha ya nyuma, mwambie mwenye hiyo ramani aiinue.
 
Unapinga wanasayansi huku ukitumia hizo picha zao, una uhakika gani kama hiyo picha ya uthibitisho wa unachokiamini kwamba ndivyo ilivyo? Au umetumia picha zao hizohizo kuthibitisha?
 
Katika jambo nilio shangaa tokea mwaka uanze hili ni la pili... La kwanza leicester kua bingwa la pili la huyu jamaa... Kwaiyo jua ndio linazama ndo kuna kua giza???
 
Binafsi sijawahi ona lenzi ya pembe 3,4,5,6,2 n.k
lenzi ambazo nimekuwa nikizishuhudia ni lenzi Mviringo. (Duara)

Hata krunzi(toch) nayenyewe ina frash ya duara.

Sasa ukichukua tochi ukamurika chini, mwanga wa tochi utakuwa na umbo ya Duara.
Hii sio sahihi kuwa unapo pamurika kuwa ni Duara la hasha, Uduara ule umeasababishwa na Tochi yenyewe kuwa na Frashi ya Duara, Kuwa na Kamera ya Duara(lenzi)
Sasa hata kamera zilizopo kwenye seteilite zinatoa majibu kutokana na zenyewe zilivyo.
Basi ngoja nitumie fikria zako...lenzi ina umbo la duara sawa...wewe ukipiga picha ua unatoka umbo la duara au unatoka jins ww ulivyo ..?

Pili sio lenzi zote zina umbo la duara weka kichwan hii kitu...kuna lenz pembe nne....inategemea tu wewe unataka umbo gani na umbo lipi unaona rahisi kwako

Fanya ivi chukua hio hio tochi unasema ina flash ya duara...chukua box la pembe nne afu limulike usiku ilo box, kimvuli chake kikitokea kwa umbo la duara njoo Hapa utupe taarifa...na ujue kiama kitakua kimefika aisee
 
Tobaa!!!

Yaani huu uzi mbali na kunichekesha umenikumbusha maneno ya Albert Einstein

Einstein aliwahi kusema,
If theory does not fit the fact,change the fact

Kama nadharia yako haiendani na ukweli,badilisha ukweli tu.Ndio mleta mada anachokifanya

Basically,the wholly biblical cosmogony perpetuates a fallacious ptolemaic cosmology which puts the flat and unmovable Earth at the middle of the universe

Biblia imepitwa na wakati,na kama Mungu ndio mwaandishi wa biblia,

Basi kuna mawili,hayupo au hana akili

Mkuu neno la Mungu halipitwi na wakati kamwe. Kila kitu kitapita lakini si neno la Mungu.
Jambo moja unalopaswa kujua ni kuwa unahitaji ufunuo (revelation) kuelewa kwa sehemu yale yaliyoandikwa kwenye Biblia!
 
Hiyo ramani ya dunia imechorwa kwa pembe nne ili kila nchi iweze kuonekana. Kwa hali ya kawaida unaweza kuona nchi unazoziona mwanzoni upande wa kushoto na zile za mwishoni kulia Kama zipo mbali mbali Sana ila zimepakana. Na masaa yao pia yanafanana ila siku ndo tofauti.
 
Dunia ni kama sinia la pilau..sio duara[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nadhani hili swala la dunia kuwa na umbo la tufe( sio duara) liko dhahili. maana hata picha zinazopigwa kutoka kwenye international space station zinaonyesha hivyo.
 
Kwa namna nilivyomuelewa mleta mada ni kuwa, hapo mwanzo dunia ilikuwa imejawa maji ndipo Mungu Muumbaji akumba ardhi juu ya hayo maji.. ni sawa na kutengeneza maboya juu ya maji.
Ahsanteni!!
 
Nimejaribu kuyafafanua maelezo yake but si kwamba naungana nae mawazo
 
Mleta uzi nimekuwa kuelewa kama wengine walivyokuelewa ndio maana kuna wanaokupinga, ila hii ni hoja na imekaa poa tu sema watu wanataka ushahidi wa hyo hoja yako, but kiukweli tukikaa na kutafakari kama watu ambao hatujaijua sayansi tutamuelewa mtoa hoja maana hata katika wanaothibitisha theory ya dunia duara ni wachache sana humu duniani kuliko wasioweza kuthibitisha hilo, na ndio hapo ninapokuelewa mtoa uzi. Je wanaokupinga wao kama wao wanathibitisha vp kama sikuamini yale ya waliothibitisha kwa theory zao mapo no kutokana na maendeleo yao ya kitechnology.
Mimi mwenyewe bado hiko kitu kinaniumiza kichwa lakini siwezi pata hou ushahidi wangu kuupinga ushahidi wao maana itanibidi nami nipae anga za mbali na uwezo huo sina.
Wanasayansi wote wa mambo ya anga na uchunguzi wa dunia kuwa duara ukiwajumlisha hawafiki idadi hata ya raia wa nchi moja yoyote duniani, ina maana dunia inawaamini wachache katika wengi,
Kwa hyo kwa hoja kama hizi tukichangia kwa uwezo mkubwa wakufikiri kama lengo la jf lilivyo tunaweza kutoka na theory yakuthibitisha kuwa si duara au comment kwa waliothibitisha.
Na hili suala sio la mleta uzi tuu, kuna wanasayansi walishatoa theory ya dunia sio duara na bado wanaendelea na tafiti juu ya hilo, ukija ktk dini kuna mambo yanaoingana na hoja ya dunia ni duaea as if dunia ya kwny bible sio hii.
Naomba kuuliza kidogo,
Nikielekea ktk mwelekeo mnyoofu na ndege let say magharibi kuzunguka dunia nitatokea mashariki?
Kama dunia inajizungusha, ni kwa spewd ngapi na je hakuna chombo kinachoizidi speed?
Nitakuja na eefference toka youtube za wanasayansi wanaopinga hoja hyo kama nitachelewa kushusha link hyo just tafuta youtube maana clip zipo.
Hii ni hoja japo haina uthibitisho sasa tujaribu kuichambua maana hata hao waliotuambia sisi bado hatujaweza kuthibitisha theory zao, naunga mkono uzi huu.


mhhh, elimu yetu imepatwa na balaa gani?
 
Mimi bwana wamenifutia uzi wangu nilikua nawaelekeza vizr kuhusu hili.
 
Mkuu sijaona sababu za msingi za hoja yako naona umeleta maandiko tu apa ambayo awali nimeona unaponda mambo tulioletewa kama bible au Quruan sasa naona una ya quote hayo kuelezea ukweli unakosea. Science sio static ndio mana kuna Geocentric theory na Heliocentric Watu wamekaa na kuandika mtu mwenye hoja na maana lake linapitishwa sasa ww lete mtazamo wako kisayansi juu ya dunia haipo ktk orbit na haizunguki..Swali kwanini tuna usiku na mchana?
Jua sio tufe nalo,linapo angaza mbele nyuma huacha kivuli ndicho husababisha kiiza na kuwa usiku.....
 
5122acd841acf0a54baed6a4be315a31.jpg

7c280ae908a97a4f018ea8035932c1c4.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom