Dunia itoze rushwa kodi

Dunia itoze rushwa kodi

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,614
Kwakuwa imethibitika kwamba rushwa haiwezikwisha asilani duniani, nadhani tuanze kutoza kodi rushwa kubwa kubwa ambazo zihalalishwe na kupangiwa utaratibu wa kupokelewa/kutolewa kupitia akaunti za benki ili serikali zichukuwe kodi zao huko huko.

Huenda serikali zikajikuta zinaingiza mapato makubwa kuliko inavyodhani. Kama hili haliwezekani basi ni bora tukaondoa Itifaki ya Haki za Binadamu wakati wa kushughulikia makosa ya rushwa ili watoaji na wapokeaji wastahili death penalty baada ya kuthibitika kisheria kufanya kosa hilo na utekelezaji wa death penalty ufanyike hima.

Hivi sasa mla rushwa anakamatika na kushitakiwa lakini huko huko kwa Pilato nako anaenda kuhonga na kuachiwa huru kwamba hana hatia na anarudi kuwashughulikia washitaki wake, ZITAISHAJE RUSHWA KUBWA KUBWA AMBAZO NDIZO ZIMEELEMEA DUNIA?

1642591818915.png
1642592013485.png
1642592145443.png
1642592324362.png


Taswira zote kwa hisani ya google.
 
Mkuu naunga mkono hoja yako maana hata sasa rushwa imeshamili pamoja na mabango na matangazo mengi ktk tv na maredio ila ndo kwanza watoaji na wapokeaji wanazidi kuongezeka kwa iyo kutoza kodi ni sahihi kabisaa ili serkal ipate mapato kuliko ilivo sasa watu hawalipi kodi.
 
Kumbe tayari Imerasimishwa! Hakika tunapoteza mapato huko
Mkuu,

Haijarasimishwa, ila imethibitika kwamba haiwezikwisha duniani maana hata Misahafu inathibitisha juu ya uwepo wake.

Sasa ya nini kufa na tai shingoni, si bora tuchukuwemo kodi ziende hazina ya nchi ili kufadhili bajeti za serikali.

Tutoze kodi wote wanaotoa na wanaopokea, hata kama ikiwa ni rushwa ya ngono basi kikokotoo chake cha asilimia ya kutoza itengenezwe.

Kwahiyo ile kauli ya mama kwamba viongozi (Mawaziri) wale lkn wasivimbiwe haitakuwa Kleptocratic wala nchi haitabezwa kwamba ni narco-state, kwasababu rushwa itakuwa ni halali kisheria.
 
Huo utakuwa mwisho wa dunia mnamtamani shetani namna hio
 
Mkuu,

Haijarasimishwa, ila imethibitika kwamba haiwezikwisha duniani maana hata Misahafu inathibitisha juu ya uwepo wake.

Sasa ya nini kufa na tai shingoni, si bora tuchukuwemo kodi ziende hazina ya nchi ili kufadhili bajeti za serikali.

Tutoze kodi wote wanaotoa na wanaopokea, hata kama ikiwa ni rushwa ya ngono basi kikokotoo chake cha asilimia ya kutoza itengenezwe.

Kwahiyo ile kauli ya mama kwamba viongozi (Mawaziri) wale lkn kwa kiasi haitakuwa Kleptocratic wala nchi haitabezwa kwamba ni narco-state, kwasababu rushwa itakuwa ni halali kisheria.
Hakika mkuu
 
Huo utakuwa mwisho wa dunia mnamtamani shetani namna hio
Rushwa ilikuwepo hata tangu BC tena Biblia imerejelea rushwa lakini hadi leo bado ingalipo, ndiyo maana watafiti wamehitimisha kwamba haiwezikwisha. SASA MBONA DUNIA HAIJAFIKA MWISHO? Kumbe bora tuibadili rushwa iwe na tija kwa umma (kodi).

Kutoka.23:8 And you shall take no bribe, for a bribe blinds the clear-sighted and subverts the cause of those who are in the right.

Mithali.17:23 The wicked accepts a bribe in secret to pervert the ways of justice.

Mithali.15:27 Whoever is greedy for unjust gain troubles his own household, but he who hates bribes will live.

Mithali.17.8 A bribe is like a magic stone in the eyes of the one who gives it, wherever he turns he prospers.
 
Back
Top Bottom