Ushauri: Ianzishwe kodi ya Matumizi ya Mitandao ya Kijamii na Matumizi ya Mfuko wa Jimbo yatazamwe upya!

ELIZAYO LAMU

Member
May 5, 2020
11
24
Barua yangu kwa mh Rais John Pombe Magufuli

ELIZAYO PASCAL LAMU
S. L. P 100,
KASULU - KIGOMA
Mobile : +2555766033331
E-mail : lamuelizayo@gmail.com


Kwa

Mh Rais wa Tanzania,
S.L.P 11400,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA.

YAH: MAPENDEKEZO NA USHAURI WANGU KWA SERIKALI TUKUFU YA AWAMU YA TANO

Mh Rais mpendwa wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk JOHN POMBE MAGUFULI kwa unyenyekevu mkubwa nakusalim shikamoo, kidumu Chama cha Mapinduzi (CCM). Pole na hongera kwa mapambano dhidi ya adui anayetunyima amani Tanzania, Africa na dunia nzima CORONA hakika kwa kumtumainia Mungu tutashinda.

Mh Rais kipenzi cha Watanzania naandika barua hii kwa unyenyekevu mkubwa kufikisha kwako maoni yangu binafsi yenye dhamira njema ya kulijenga taifa na kuunga mkono mapambano yako ya kuimarisha uchumi wetu na kuboresha maisha ya Watanzania.

Naomba kufikisha kwako mapendekezo haya kwako ambayo naamini ni yenye tija kwa taifa langu.

1. NAPENDEKEZA KUANZISHWA KODI YA MITANDAO YA KIJAMII (WhatsApp, Facebook, Instagram na Tweeter)

Mh Rais pamoja na kuwepo kwa gharama ya kununua vifurushi katika mitandao ya simu kwa ajili ya mitandao ya kijamii nashauri serikali yako tukufu ianzishe kodi ya moja kwa moja na ninapendekeza kwa siku iwe Tsh 100 na ilipwe moja kwa moja TRA kwa mfumo rasmi utakaoratibiwa na mitandao ya simu pamoja na serikali.

Kwanini napendekeza kodi hii:

a. Ni chanzo cha uhakika cha mapato ukizingatia watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaongezeka siku hadi siku na kwa kuwa Tanzania inapaswa kujengwa na Watanzania, siyo dhambi kutumia fursa inayojitokeza kutokana na Watanzania.

b. Itapunguza matumizi yasiyo na tija na kuleta nidhamu ya matumizi ya mitandao ya kijamii.

c. Kwa asilimia kubwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wanatumia kwa starehe kama ilivyo unywaji wa pombe, hivyo hakuna dhambi kuchukua kodi hii muhimu ukizingatia kodi hii haitawagusa wanyonge.

Mh Rais nakusihi utoe agizo mamlaka husika zitazame namna ya kunufaika na kodi hii muhimu katika kuimarisha mapato yetu.

2. NAPENDEKEZA MATUMIZI YA FEDHA YA MFUKO WA JIMBO YATAZAMWE UPYA

Mh mpendwa Rais nimefanya tafakari ya kina juu ya matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo nimegundua mambo haya:

a. Hakuna matokeo ya moja kwa moja kwa wananch katika majimbo mengi fedha za mfuko wa jimbo zinatumika bila kuzingatia mahitaji ya jamii badala yake ni mapenzi binafsi ya mbunge na kamati yake.

b. Mfuko wa jimbo imegeuka rushwa ya kutafutia kura kwa baadhi ya wabunge wamekuwa wanaunda vikundi vya ubabaishaji na kuwapa fedha za mfuko wa jimbo kwa mwamvuli wa vikundi vya ujasiriamali wakati kihalisia hakuna ukweli wowote na hakuna matokeo chanya ya migao hii.

d. Matumizi ya mfuko wa jimbo katika majimbo mengi hayazingatii katika kuboresha miundombinu na maisha ya watanzania badala yake imekuwa pesa za kugawana kiholela nathubutu kusema imekuwa zaidi ya utakasishaji fedha katika majimbo kadhaa.

Napendekeza haya yafanyike

a. Ifanyike ukaguzi na uchunguzi wa kina katika majimbo yote nchini na wabunge wakabithi documents za matumizi ya miaka mitano .

b. Kuwepo kamati ya matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo ambayo inampunguzia nguvu mbunge mamlaka ya kuamua matumizi ya fedha kwa matakwa binafsi maana kamati zilizopo zipo mikononi mwa mbunge.

c. Kuwekwe mkakati wa kulazimisha fedha za mfuko wa jimbo kujenga angalau miradi miwili au mmoja mkubwa katika jimbo kuliko kuzitawanya katika miradi mingi isiyokamilika.

Mh mpendwa Rais fedha za mfuko wa jimbo zikisimamiwa vizuri zitaleta tija katika kujenga maisha bora ya watanzania lakini zikiendelea kutumika ilivyo ni hasara kwa serikali .

3. MAPENDEKEZO KUHUSU UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA HALMASHAURI .

Mh mtufuku Rais kumekuwepo na changamoto sugu katika utaratibu wa ujenzi wa barabara na miundombinu ya barabara kwa ujumla katika halmashauri nyingi nchini .

a. Kumekuwepo tabia ya kila diwani kudai apatiwe miradi kwa kila fedha bila kujali uwezo wa budget kitu hiki kinapelekea fedha kidogo kugawanywa katika kata zote kujenga barabara zenye kiwango cha chini zisizodumu

b. Halmashauri nyingi zimekuwa na tabia ya kujenga barabara kwa gharama kubwa na baadae kubomoa ndani ya muda mfupi . Mfano inajengwa barabara ya kawaidana mifereji ya kisasa au barabara ya lami kiwango cha chini baada ya muda inaborewa na kujengwa barabara ya lami nyingine.

Mapendekezo yangu

a. Napendekeza kila budget zijenjwa KM kadhaa za lami standard katika halmashauri nchini kuliko kulazimisha kugawa fedha kata zote kitu kinachopelekea kurudia ujenzi kila mwaka badala ya kujenga barabara za kudumu . Utaratibu wa kujenga barabara lami KM chache kila budget itazifanya halmashauri zetu ziwe na KM nyingi za lami baada ya miaka michache.

b. Kabla ya kujenzi wa barabara watalaam wazingatia mipango ya serikali ni aibu kujenga barabara na miundombinu kwa gharama kubwa sehemu ambayo inafahamika utapita mradi mkubwa wa TANROAD au mradi mwingine huu ni mgawanyo mbaya wa fedha za umma.

Mh Rais fedha za ndani halmashauri pamoja na ruzuku kutoka serikali kuu zikitumika vizuri ndani ya miaka mitano nchi yetu itakuwa na barabara nyingi za lami mtaani.

4. KUHUSU MAFUNZO YA LAZIMA YA JESHI LA KUJENGA TAIFA ( JKT)

Mh Rais kwa nia njema kabisa serikali ilianzisha mafunzo ya lazima ya JKT kwa wahitimu wa kidato cha sita kabla ya kujiunga vyuo vikuu. Nimefanya tathmini ya kina kwa kutazama vijana waliohitimu mafunzo hayo karibuni kwa kulinganisha na vizazi vilivyopita JKT miaka hiyo nimetambua yafuatayo:

a. Vijana wengi waliopita huko hawana ujuzi wa kujitegemea kama ilivyotegemewa. Vizazi ilivyopita JKT zamani wanao ujuzi wa kilimo, ufundi stadi katika fani mbali mbalimbali tofauti na kizazi cha sasa.

b. Kwa kuzingatia maelezo ya (a) serikali inatumia gharama kubwa kuendesha mafunzo ya JKT kwa wahitimu wa kidato cha sita lakini matokeo ni kinyume hakuna faida kubwa kama matarajio na nia ya kuanzia program.

Napendekeza haya kwako:

a. Fedha ambazo zinaelekezwa kwenye mafunzo ya lazima JKT zielekezwe kwenye kujenga vyuo vya ufundi stadi katika wilaya vijana wafundishwe ujuzi kama ufundi washi, uselemala, umeme, computer, nk hii itasaidia kuondoa tatizo la ajira na kujenga kizazi cha Tanzania ya kujitegemea.

b. Mafunzo ya JKT kwa wahitimu wa kidato cha sita yajikite zaidi katika kufundisha ujuzi wa kupambana na maisha kwa wasomi wetu pasipo kutegemea ajira yaani makambi ya JKT yapewe budget ya kuandaa wabobezi wa ufundi katika fani mbalimbali ili vijana wajiunge vyuo vikuu wakiwa na ujuzi wa kutengeneza ajira wenyewe pia itakuwa nguvu kazi ya kutimiza azima ya Tanzania ya viwanda.

Mh Rais kwa unyenyekevu mkubwa naomba kuwasilisha maoni haya manne pamoja kuwa yapo mengi lakini naomba kufikisha haya . Mh Rais natumia barua kwasababu sina namna ya kufika kwako na kuzungumza lakini ninayo mengi mno ya kukufikishia .

Natambua juhudi zako na uthubutu wako mkubwa wa kuijenga Tanzania iliyo tumaini la watanzania wengi. Usikatishwe tamaa na genge la Watanzania wachache waliochagua upande wa kubeza na kupinga kila jambo maana Watanzania wengi tupo pamoja nawe.

NDANI YAKO YAPO MATUMAINI MAKUBWA YA WATANZANIA.

Kidumu chama cha mapinduzi.

Elizayo Pascal Lamu,
Mtanzania
 
Serikali tukufu italifanyia kazi wazo lako


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huyo Rais huwa yuko busy sana na Hana tabia ya kusoma barua anazotumiwa na Wananchi wake moja kwa moja sembuse za mitandaoni; labda kwa kuwa umependekeza kukomoa watumiaji wa mitandao kwa Kodi atakusikiliza!!!!
 
Mkuu hongera sana kwa manono mazuri hasa hapo kwenye mfuko wa jimbo, nipo katika halmashauri moja hivi watumishi wa ofisi ya mbunge (katibu wa mbunge) na idara ya mipango wanacheza sana rafu, Wanawaingizia kijiji mfano milioni 3.5 alafu wanawambia wakatoe then wawape milioni 1.5, kijiji kibaki na milioni 2. Kama wakigoma wanazihamisha na kuzipeleka kijiji kingine. Yaani huu mfuko una upigaji sana, jamaa hawana huruma na hizi pesa.
 
Huyo Rais huwa yuko busy sana na Hana tabia ya kusoma barua anazotumiwa na Wananchi wake moja kwa moja sembuse za mitandaoni; labda kwa kuwa umependekeza kukomoa watumiaji wa mitandao kwa Kodi atakusikiliza!!!!
True angekuwa na tabia ya kuyachukua ya positive toka kwa wananchi wake tungekuwa mbali Sana Kama wafanyavyo nchi zilizoendelea,shida ya mifumo mibovu ya kiuongozi Africa ukiwa mtawala means una akili na unajua kila kitu kuliko unaowatawala.By reaserch thus watawala wa kiafrica huwa na akili wakishatoka madarakani check hata speech zao baada ya kustaafu zinakuwa Kama zinaponda waliyoyafanya
 
True angekuwa na tabia ya kuyachukua ya positive toka kwa wananchi wake tungekuwa mbali Sana Kama wafanyavyo nchi zilizoendelea,shida ya mifumo mibovu ya kiuongozi Africa ukiwa mtawala means una akili na unajua kila kitu kuliko unaowatawala.By reaserch thus watawala wa kiafrica huwa na akili wakishatoka madarakani check hata speech zao baada ya kustaafu zinakuwa Kama zinaponda waliyoyafanya
Sawa. Ila huyu wa hapa ana zaidi ya ulichosema. Ana roho mbaya, dharau na "much know." Ukichanganya vyote hivyo ni disaster!!!
 
Wazo zuri sana

Nchi za Mabeberu ukiwa na wafuasi kuanzia alfu moja kwenye mtandao unalipa kodi
1588663404836.png


Mabeberu eeeh! Aisifiaye mvua imenyea. Kazi ya beberu twaijua.

Pichani, Beberu akinywa Bia yetu
 
Back
Top Bottom