Dunia ingekuwaje bila wazungu?

Yaani umekaaa na kupoteza muda wako kufikiria bila hata kupata jibu kaswali haka kadogo tu....duh ama kweli sisi wavivu
 
Ukitaka kupata jibu ni rahisi saaana soma maendeleo ya afrika kabla ya ukoloni alafu Vuta picha stage tulipoishia mpka sasa HV tungekuwa wapi...
 
Mimi si mwana historia na historia yenyewe niliachana nayo tangia nikiwa kidato cha pili!! Hata hivyo, sidhani kama nahitaji kuwa mwanahistoria niliyefuzu kubashiri tungekuwa wapi!

Inakera, inachukiza na kuchefua manake kwa haraka haraka ni kama tunahusudu uzungu... lakini ukiweka pembeni African Pride bado ukweli mchungu wa swali unabaki pale pale... tungekuwa wapi! Wapo wanaodai kama si Wazungu kuja ingekuwa tumeshapiga hatua lakini kuja kwao kukatudumaza na hatukuwa tena na sababu za kutumia vichwavitu kukabiliana na changamoto tulizonazo kwavile kila kitu kingefanywa na mzungu! Inawezekana lakini hata hivyo labda hivi sasa huenda tungekuwa kama Wazungu walivyokuwa zaidi ya miaka 1000 iliyopita manake inaonekana kasi ya akili zetu katika kukabiliana na changamoto zilizotuzunguka ilikuwa ndogo kupita maelezo!

Haijalishi ikiwa Mzungu ujanja aliiba wapi na wapi; au nani alikuwa na ujanja huo kabla yake lakini lililo wazi ni kwamba, jamii zote zilishapoteza mwelekeo hata kama katika kipindi fulani walikuwa super power! Lililo wazi ni kwamba, wakati Mzungu ameshafikia industrial revolution takribani miaka 500 iiyopita bado jamii za kiafrika zilikuwa zinaishi primitive life ambazo hazikuwa na dira yoyote ya maana!
 
Mungu ndio kila kitu,wao ni sababu tu.
Kwani Bila wanawake watu wasingezaa?au Bila wanaume wanawake wasingezaa?Mungu angefanya iwe tu kama angeamua

Na kila kitu ambacho Mungu amekileta basi ni Mawaidha tosha kwa binaadam.Na vingine ni kujaribu kama Binaadam anaweza kutambua kwamba Mungu anauwezo mkubwa kiasi gani.Either utakufuru kama mleta Post au utashukuru na kumkubali Mungu uwezo wake.

Mungu anahekma zake anapoleta kitu
 
Mkuu Retired, hesabu walianzisha Waarabu, Wagiriki walileta demokrasia, Roman empire ndiyo iliwafundisha wazungu ustaarabu, tuliwafundisha wazungu kufua chuma.

Mhhh, binti mwema Sky, hizi historia siziamini. I HAVE NEVER HEARD OF ANY GREAT EGYPTIAN MATHEMATICIAN. After all what did they mean by ustaarabu. Last week niliweka a list of great scientist who have shaped this world, hakuna wa Egypt wala Greece etc anyway
 


Unasahau kitu kimoja muhimu sana, hapa Daniani civilization huja na civilization hupotea, kuna wakati Farao misri ndiyo waliokuwa Dunia wakapotea, wakaja Wachina, wakaja Waarabu sasakuna Wazungu, hata Wazungu pia wamefikia ukingoni na sasa wanaanza kuanguka, ukiangalia leo hii Capitalism inafail kila mahali, Wazungu unemployment inaongezeka wanashindwa kuzalisha ajira kuna ushindani mkubwa ambao haukuwepo miaka 50 iliyopita hasa kutoka Asia hivyo miaka 50-100 ijayo Dunia haitakuwa hii ya leo ...
 
Leo ninashughuli I can't go in deep, weekend nitakujibu.
 
Come on, tunasema science, hiyo simu usingelikuwa nayo.



sio kweli kila kitu kingekuwepo mana waliwakuta mababu wameendelea kwenye nyanja za sayansi ndio mana walikuwa wanawakata mikono
 
Tanzania mna maisha magumu, mmebuni nini
Tanzania tulikuwa na maisha rahisi sana ya ujamaa, amani, utulivu, ardhi nyingi unaweza kulima, kujenga, kuchungia popote, joto, mifugo mingi inayojiendea popote, elimu na matibabu bure. MAISHA HAya 'rahisi' yalitufanya tushindwe kupambana kifikra ukilinganisha na watu kama Wakenya, Rwanda, Burundi, UGANDA, Ethiopia, Ulaya, Uchina, Marekani, Cuba, n.k. Inatulazimu kutafuta hata wachezaji kutoka Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda, Zimbabwe, nk kuja kucheza mpira Simba na Yanga. Marekakani kwa taarifa yako wako kama hivyo walivyo kwasababu ya maisha magumu na mifumo migumu sana, kule kama hutafanyakazi hutakula, hutatibiwa, hutalala, hutaolewa, hutasafiri, hutasikiliza redio wala kuangalia tv, wala hutamiliki simu. kule ni 'all or none' hakuna half way. Magufuli anachokifanya ndicho walichofanya na wanachoendelea kukifanya wazungu hata kufikia hapo unapowaona leo. Shida yetu ni kuwa na hata maprofessor wapenda kuajiriwa na kutumwa na wengine badala ya wao ku create ajira kwa watu wengine.
 
Kumbuka vyuo vikuu vya kwanza ni Afrika,chuo chwa kwanza kikuu kilianzishwa na mwanamke huko Tunisia na kuguatia cha Misri,zote ni nchi za kiafrika.Na hata elimu nyingi zilianza Afrika za kugundua majanga mbali mbali kwa kutumia njia za asili,kabla majanga hayajatkea.
Kwenye elimu ya tiba,upasuaji ulianza Misri,nchi iliyopo bara la Afrika.Mababu zetu wa kiafrika waligundua tiba za miti na matunda,na tiba hizo hazikuwa na madhara yoyote.Mpaka leo tiba hizo zinatumika,na kuhimizwa ulimwenguni kote.
Kumbuka vyuo vikuu vya kwanza ni Afrika,chuo chwa kwanza kikuu kilianzishwa na mwanamke huko Tunisia na kuguatia cha Misri,zote ni nchi za kiafrika.Na hata elimu nyingi zilianza Afrika za kugundua majanga mbali mbali kwa kutumia njia za asili,kabla majanga hayajatkea.
Kwenye elimu ya tiba,upasuaji ulianza Misri,nchi iliyopo bara la Afrika.Mababu zetu wa kiafrika waligundua tiba za miti na matunda,na tiba hizo hazikuwa na madhara yoyote.Mpaka leo tiba
 
Sasa wewe unalazimisha mambo. Jibu kwanza ndio utoe mapendekezo yako.
 
Sio kweli,hivyo vyote tungekuwa navyo,kilichotokea ni kuwa walituzidi kete wakatupanda vichwa hatimaye wakafanikiwa kwenye uchumi kwa kupitia migongo yetu,otherwise tusingekuwepo sisi na wao wasingefika hapo walipo.
 
Sio kweli,hivyo vyote tungekuwa navyo,kilichotokea ni kuwa walituzidi kete wakatupanda vichwa hatimaye wakafanikiwa kwenye uchumi kwa kupitia migongo yetu,otherwise tusingekuwepo sisi na wao wasingefika hapo walipo.
Endelea kujipa moyo, ipo siku utayashinda.
 
Hahahaaa labda hapo kwa wake zaidi ya kumi wanawake wangekuja weka pingamizi
Tungekuwaje na michepuko ili hali kila mmoja angekuwa na wake kumi kidogo?

Chips zisingekuwepo na wa Dar wangekuwa strong.
 
Walipogundua Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kama vile babu zetu hawakuyaona.
Eeh sasa watu kama walikuwa hawana majina?Mpaka majina yetu yote si mengi ya kizungu au?Ila tulikuwa na technlojia ya kufua vyuma mjue sema basi tu mzungu katuwahi na akatia sumu kali saana mpaka leo bado ipo.Hatujikubali na kama tunajikubali basi 40%
 
Tungetembea bila hata nguo,yaani full kiyoyozi,hawa jamaa wameharibu kweli!
 
Hahahaaa labda hapo kwa wake zaidi ya kumi wanawake wangekuja weka pingamizi
Wasingethubutu kukenua pua mbele ya mfumo dume kudai 50*50 sababu tusingekuwa na Mashirika ya kichochezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…