Dunia ingekuwaje bila wazungu?

Dunia ingekuwaje bila wazungu?

Wakuu hili swali huwa najiuliza sana, kwamba hii dunia ingekuwaje bila hawa watu. Mambo mengi katika hii dunia wao ndo wagunduzi kuanzia mambo ya teknolojia, kieletroniki, sayansi na mengine mengi wakati Africa hakuna kitu cha maana chochote tulichofanya wakati white people ndo walioifikisha dunia hapa ilipo.

Hivi bila hawa jamaa ingekuwaje?
Dunia ingekuwa kama wahazabe, amazonian, mursi t
Wakuu hili swali huwa najiuliza sana, kwamba hii dunia ingekuwaje bila hawa watu. Mambo mengi katika hii dunia wao ndo wagunduzi kuanzia mambo ya teknolojia, kieletroniki, sayansi na mengine mengi wakati Africa hakuna kitu cha maana chochote tulichofanya wakati white people ndo walioifikisha dunia hapa ilipo.

Hivi bila hawa jamaa ingekuwaje?
Tungekuwa kama Wamasai, wahazabe, Amazonian s,mursi, hotentals na wale Kule mvumi Dodoma
 
Wakuu hili swali huwa najiuliza sana, kwamba hii dunia ingekuwaje bila hawa watu. Mambo mengi katika hii dunia wao ndo wagunduzi kuanzia mambo ya teknolojia, kieletroniki, sayansi na mengine mengi wakati Africa hakuna kitu cha maana chochote tulichofanya wakati white people ndo walioifikisha dunia hapa ilipo.

Hivi bila hawa jamaa ingekuwaje?
Soma vizuri historia yako kuhusu Africa kabla before Christ
 
Siku wakisema kila nchi itumie vitu ilivyotengeneza yenyewe hata sipati picha! msafara wa rais utakuwa na lundo la mikokoteni,kuhamia Dodoma ndo itakuwa basi tena,wali tutalia vidole,kuangalia Tv na kusikiliza redio ndo kwaheri,show za fiesta hazitakuwa na maiki wala spika,fikiria nguo za mitumba zote,majinsi makali,makadeti,viatu vyote vya wazungu vikachukuliwa...ndio utajuwa waafrika tuko nyuma kiasi gani,Tujenge viwanda tuache utani.
 
Sijui waafrika wangelikuwaje! Kosa alilolifanya Mungu ni kuwaumba waafrika
 
Mushi siyo kwamba sisi hatuwezi tatizo Africa ni viongozi wamewekeza kwenye siasa badala ya utaalamu, kila MTU anafikiria kuwa. mwanasiasa iliaishi vizuri, hats Leo Afrika kipaumbele ikiwa elimu baada ya miaka 20 Africa itakuwa mbali sn.
 
wangekuwepo wengine kama vile wachina na wajapani
 
Siyo kweli ni bora ungerekebisha swali lako na kuuliza Dunia ningekuwaje bila ya Binadamu? Kumbuka kwamba kila ukionacho leo hii kilikuwepo tangu kale na sasa hivi kinachofanyika ni kuboresha tu, hivyo ingawaje Wazungu au watu wa Magharibi leo hii ndiyo wenye uchumi mkubwa Duniani na kuongoza kwenye mambo ya Sayansi na Teknolojia lkn pia wamejifunza/kuchukua au niseme kuendeleza mambo mengi sana ktk jamii nyingine!

We are not talking of ccm, we are talking science and development.
 
Hawa jamaa wanatuona sisi mbwiga sana. Ninakumbuka wakati nilisikia kesi ya kaka wa kichaga, alikwenda kufanya PhD Uingereza, walimpa thesis ngumu sana ambayo wanafunzi wengi waliishindwa, mchaga aliipasua, hawakuamini, walimwita na kumpa kazi, lakini hawakumpa mshahara wa PhD holder, kaka wa watu aliifikiria ile package, na visa, alikubali. Mke wake alipelekewa barua kutoka mgombani anafika Dar anaambiwa lete passport yako na za watoto mchukue visa zenu.

What was that thesis about? Einstein alimaliza kila kitu hicho kigumu kilikuwa kipi
 
MUNGU HANA UPENDELEO HATA CHEMBE, SIKU NCHI ZETU ZIKIWA NA MFUMO BORA WA KUENDELEZA VIPAJI, NA KUTOA ELIMU BORA BASI AFRICA TUTAKUWA ZAIDI YA ULAYA. TUMEZIDI KUWA WABINAFSI SANA, KUANZIA KWENYE NGAZI ZA FAMILIA HADI UONGOZI WA NCHI.

Umesoma nguin with that argument
 
fuatilieni historia ya mafarao wa egypt kabla ya kuja hao wazungu timbuktu,kushi na vi states vyote
 
YANGETOKEA YAFUATAYO
1.Jamiiforums isingekuwepo

2.Tusingekuwa na Bombardier

3.Laptop na Smartphone, visingekuwepo

4.Biashara ya kubeti isingekuwepo

5.Tungekuwa na dini pamoja na tamaduni zetu wenyewe.

6.Pale posta pangekuwepo na vichaka vya kuogofya na tusingekuwa na barabara za lami.

7.Tusingekuwa na TANESCO, TCRA, NEC, TBC, n.k

8.Pasingekuwepo na UKIMWI wala CONDOM.

9.Mapenzi yangetegemea hisia za dhati na sii pesa.

10.Nisingekuwa naisubiri game ya Liverpool na Manchester United 17 ya October.
Hahahahah umetisha sana mkuu
 
Maisha magumu ndio yanayozalisha watu wabunifuni na wanafalisafa. Maisha legelege na rahisi yanazaa watu legelege pia. maisha ya wazungu na Waasia yalikuwa magumu sana yaliyotawaliwa na baridi kali, utawala wa kibabe, dhuluma, njaa kali, masaa mengi ya kufanya kazi, ujira kidogo, n.k. Maisha ya aina hii yalisababisha wazungu, wachina, wakoroea, nk wawe na ujasiri wa kupambana na maisha yao ili waweze kusurvive. Hata hapa Tanzania ile mikoa yenye maisha magumu ya baridi, milima, ardhi kidogo, kama vile Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Makambako, nk maendeleo yao yana ahueni kulinganisha na maeneo yenye joto, ardhi kibao yenye mbolea, nk kama vile pwani, Dodoma, singida, nk

Tanzania mna maisha magumu, mmebuni nini
 
Tungekuwa mbali sana...kwa sabab kabla ya ujio wao tulikuwa tuko sawa kimaendeleo
 
Elimu tumeifanya kama dini ambayo makao yake makuu ni huko kwa wazungu,na ndiyo maana tunawasikiliza wao kwa kila jambo(ya uongo na kweli) na ndiyo maana tuna amini hatuwezi kufanya kama wao.

Leo hata kitu kikitengenezwa Japan au china ila utasikia tukisifia wazungu balaa.
 
Siyo kweli ni bora ungerekebisha swali lako na kuuliza Dunia ningekuwaje bila ya Binadamu? Kumbuka kwamba kila ukionacho leo hii kilikuwepo tangu kale na sasa hivi kinachofanyika ni kuboresha tu, hivyo ingawaje Wazungu au watu wa Magharibi leo hii ndiyo wenye uchumi mkubwa Duniani na kuongoza kwenye mambo ya Sayansi na Teknolojia lkn pia wamejifunza/kuchukua au niseme kuendeleza mambo mengi sana ktk jamii nyingine!
Utakuwa umesoma history na hivi ndivyo mlivyokuwa mnadanganywa na Pan Africanists!! Nijibu swali moja: Industrial revolution iliyotokea Europe zaidi ya miaka 500 iliyopita, hadi hivi sasa Afrika hatujaifikia pamoja na kwamba tuna kwa kujifunza... NDIYO AU HAPANA? Kama HAPANA, fafanua!
 
Wakuu hili swali huwa najiuliza sana, kwamba hii dunia ingekuwaje bila hawa watu. Mambo mengi katika hii dunia wao ndo wagunduzi kuanzia mambo ya teknolojia, kieletroniki, sayansi na mengine mengi wakati Africa hakuna kitu cha maana chochote tulichofanya wakati white people ndo walioifikisha dunia hapa ilipo.

Hivi bila hawa jamaa ingekuwaje?
Kusingekuwa na silaha za maangamizi kama ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom