Shapeshifters: Watawala wa Kweli wa Dunia?

Shapeshifters: Watawala wa Kweli wa Dunia?

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
733
Reaction score
1,714
SHAPESHIFTER

Hawa ni watu wenye nguvu kubwa za kichawi. Inaelezwa kuwa hawa ndio watu wenye kuongoza dunia hii. Mataifa makubwa yote yanamilikiwa na binadamu wa aina hii binadamu ambao kidunia wanatajwa kama wafu lakini uhalisia wapo hai.

Mfano ziliwahi kuvuja taarifa za ndani kuhusu maraisi kadhaa wa marekani wanatambulika kuwa wafu lakini wanaonekana kwenye ikulu ya White house.

Dunia ina mfumo huu wa waaminishe kisichokuwa na uhalisia alafu ukweli huwa wanabaki nao wenyewe kulingana na dhamira yao. Inaelezwa pia wapo watu wengi leo maarufu duniani sio watu kweli bali ni viini macho.

Mfano wa watu hao ni kama Oprah Winfrey. Habari za ndani zinasema huyu sio Oprah mwenyewe bali mwenyewe alishakufa huyu ni kiini macho. Huyu tunaemuona ni pandikizi la kizimwi ambalo yupo kwa maslahi ya hao shapeshifter.

Hawa ni watu wenye nguvu kubwa duniani na wanaweza kufanya chochote kwenye dunia hii. Baadhi ya watafiti wa mambo wanasema hili ni kundi linalotoka kwenye Illuminati.

Mark Coney anasema jamii hii ya siri ndio inayosimamia mashirika yote makubwa ya kitaifa. Lengo la jamii hii huko mbeleni ni kuja kuanzisha serikali moja yenye nguvu duniani kote.

Dunia ina vitu vingi vya siri vinaendelea lakini hufichwa kwa nadharia nyengine ili dhamira yao ibaki kuwa siri. Wewe utaambiwa ni mambo ya kisayansi kumbe tawala za kishetani ndizo zinazohusika kwenye teknolojia.
 
Back
Top Bottom