Hivi halali dume zima kufanya birthday.
Binafsi sioni tatizo.
Tunatakiwa kujua malengo ya Birthday ni yepi.
1. Lengo kuu ni kufurahia siku yako ya kuzaliwa kwa kumshukuru Muumba wako kwa kukupa neema ya uhai na mpaka siku hiyo bado kuweza kupumua maana wengi walitaka hiyo neema lakini hawapo nasi tena. Mwingine ata sali, mwingine atafunga, mwingine atatoa sadaka na kadhalika.
2. Lengo lingine ni kuonesha upendo wako wa dhati kwa watu wako wa karibu wenye kukupenda na unaowapenda. kusherehekea kwa keki, chakula na vinywaji.
3. Kuimarisha undugu, urafiki na kujuana na watu zaidi. Kwenye sherehe unapata kufahamiana na watu tofauti. Watu wanafahamiana kwenye misiba na sherehe pia na sehem tofauti tofauti zinginezo.
4. Kuna kamsemo kanasem, No Concentration without Relaxation. Kama binadamu tuna stress nyingi sana akilini mwetu, kazini umegombana na mtu, umerudi nyumbani dada kachelewa kupika na una njaa, mara umeenda kwenye ATM kutoa pesa umekutana na foleni kama wale wanaoenda kuchota maji kisimani, halafu kipindi inafika zamu yako baada ya kusubiri masaa mawili unakuta mashine inasema Temporarily out of service, hapo umechukua boda boda mfukoni huna hela zipo bank, ndo unaenda kwa mangi dukani kukopa umtoe mwenye boda boda, mara mkeo/demu wako kakujibu ovyo, mara mtu kakuudhi mtaani, tunakutana na stress nyingi sana, unavumilia mwaka mzima, sasa unapopata siku kama hii unajaribu kujipooza japo kwa siku moja.
5. Kiafya ina shauriwa pia hasa kimawazo, kua na mimi napendwa na marafiki zangu na ndugu, hata yule mwanaume ambae ana roho ngumu isio na hurumu kuliko jambazi, lakini akifanyiwa mstukizo na keki na mtu ampendae awe ni mamaake mzazi au yeyote yule lazima atahisi faraja ya moyoni, maana ana moyo sio jiwe.
Faida zipo nyingi sana, kama tunajipa muda wa mapumziko kama za serekali, uhuru day, karume day, sijui nyerere day, kwanini usiwe na birthday?
Mawazo yangu, nimewakilisha.