Dubai tumesaini nao mikataba ya maendeleo zaidi ya 30. Watanzania wanaopenda Maendeleo tumieni fursa alizotuletea Rais Samia

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,890
109,226
Nawashangaa sana Tanzania chamber of Commerce na BET ambao ndiyo wanashughulikia mambo ya biashara baina ya Tanzania na nchi za nje.

Nawashangaa zaidi waandishi wa habari wa Tanzania, hususan hawa free lancers waliojazana sasa hivi kwenye mtandao. Alziandika Mwandishi. Mmoja tu, msome chini hapa.

Walitakiwa wazitangaze sana fursa hizi. Hii siyo mikataba ya siri wala kuficha ni mikataba iliyosainiwa kihalali na vyonbo vya habari vya nje viliiandika.

Nadiriki kusema Mkataba wa bandari unaoshangiliwa na kukoromewa na kila mtu sasa hivi ni mkataba mdogo sana ukilinganisha na mikataba iliyisainiwa na fursa zilizopo. Jisomee 👇🏾

Tanzania-UAE Relations: President Samia Suluhu’s milestones

Tanzania-UAE Relations:​

By Giza MdoeMarch 4, 2022.

  • Tanzania has signed a US$7.49 billion business partnership deal with the United Arab Emirates (UAE)
  • Samia Suluhu spearheaded the signing of some 36 MoUs of which 12 were signed by government public institutions
  • Working with Tanzania, she said, the UAE will enjoy a market of 177 million people of the East African Community (EAC)
Tanzania’s President Samia Suluhu Hassan is making headlines, the latest of which is an impressive US$7.49 billion business partnership deal with the United Arab Emirates (UAE).

President Samia, the first woman president of the country, attended Dubai Expo 2020 at the turn of the week. She was received by Vice President and Ruler of Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid, at the start of this month.
Among other things, Sheikh Mohammed and President Samia discussed ways to extend cooperation between their countries. The meeting was strategically held during Tanzania’s national day at the fair.

Themed, Connecting Minds, Creating The Future chimed well with her country’s own theme, Ready To Take Off, the Expo gave the two leaders the opportunity to discuss bilateral relations and open up business opportunities for both countries.

“These two themes embrace the new age of investment and trade with strategic partners like the UAE, in particular, and the Gulf in general,” President Samia commented about the Expo theme.

President Samia took the opportunity to invite UAE investors to Tanzania saying in line with the Expo theme, Tanzania is ‘Ready to take off.’

“I would like to take this opportunity to welcome you all to Tanzania, where the business and investment environment are more than conducive. Come one, come all to Tanzania,” she said.

Soma zaidi: Tanzania-UAE Relations: President Samia Suluhu's milestones

Tafsiri kwa Kiswahili itafatia chini huko.
 
  • Tanzania imesaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara wa dola za Marekani bilioni 7.49 na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)
  • Samia Suluhu aliongoza utiaji saini wa mikataba 36 ambapo 12 ilitiwa saini na taasisi za serikali.
  • Kwa kufanya kazi na Tanzania, alisema, UAE itafurahia soko la watu milioni 177 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anaingia kwenye vichwa vya habari, cha hivi punde zaidi ni mkataba wa kuvutia wa kibiashara wa dola za Marekani bilioni 7.49 na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
 
Nawashangaa sana Tanzania chamber of Commerce na BET ambao ndiyo wanashughulikia mambo ya biashara baina ya Tanzania na nchi za nje...
Na amejtahidi kuuweka uwazi lakini hofu tu ya baadhi ya watu muhimu kuboresha vipengele vyenye utata.
Kuna watu walikuwa na hofu kama hii wakati hayati Mkapa alivyoleta FDI za SA lakini nyingi zinafanya vizuri mpaka leo
 
Endeleeni kuuza Raslimali zaTanganyika kwa raha zenu.
Sawa tumekusikia. Wale wa zamani wenzangu watakumbuka tulisikia hayo ya mapoyoyo wakisema "nchi wanauziwa makaburu". Akiambiwa Mkapa anauza nchi. Mbona benki bado ipo mpaka leo?

Wajanja wachache wenye exposure wakaiona fursa, wakaikumbatia, keo mabilionea Tanzania hii.

Wewe ningekuona una akili ungeuliza, hizo fursa tunazipata vipi , siyo kubwabwaja bila mpango. Kauze vyako kama rahisi.

. Kalaga baho.
 
Na amejtahidi kuuweka uwazi lakini hofu tu ya baadhi ya watu muhimu kuboresha vipengele vyenye utata.
Kuna watu walikuwa na hofu kama hii wakati hayati Mkapa alivyoleta FDI za SA lakini nyingi zinafanya vizuri mpaka leo
Hakuna kipengele chenye utata, mkataba nimeusoma wenyewe unajibu kila hoja.

Kwanza. Hamuwaamini wanasheria wetu?

Pili, Waarabu wa Dubai hawana zaidi ya kufanya biashara, hawawezi kuharibu reputation yao kwa kuilalia nchi yoyote ile kibiashara.

Tuwe na mawazo chanya. Tuzitumie fursa.
 
Kwa hakika Rais wetu shupavu ,imara,mzalendo, madhubuti na mchapa kazi mama Samia suluhu Hassani amedhamiria kuhakikisha kuwa Tanzania na watanzania tunanufaika na fursa za kiuchumi kutoka kila pembe ya Dunia.

Rais Samia ni Neema kwa maisha ya watanzania kwa kuwa tunakwenda kushuhudia mtirirko wa fursa za kiuchumi kwa nchi yetu, tunakwenda kupata fursa nyingi Sana za ajira hasa kwetu vijana,tunakwenda kuona mapato yetu yakipaa zaidi,tunakwenda kuona kipato na uchumi wa mtu mmoja mmoja ukikua na kuongezeka ,tunakwenda kuona Hali ya maisha ya watanzania ikiboreka na kuwa yenye kutia matumaini.

Tunakwenda kushuhudia na kuona uchumi wetu ukigusa maisha ya watanzania,tunakwenda kuona mzunguko wa fedha mitaani ukiwa wenye Afya ,tunakwenda kuona biashara zikishamiri hapa nchini ,tunakwenda kuona Tanzania ikizipita kiuchumi nchi za jumuiya ya Afrika mashariki na Kati,tunakwenda kuona Tanzania ikiwa chaguo namba moja kwa watalii na wawekezaji.

Hii Ni kutokana na uwezo mkubwa alio nao Rais wetu mpendwa mama Samia kiushawishi na katika kuwashawishi wawekezaji, pia kutokana na mazingira Bora na rafiki katika kuwekeza lakini yanayozingatia maslahi mapana ya Taifa letu.

Najuwa na Nafahamu kuwa wapo wengine kwa Sasa hawawezi kuona fursa ambazo nchi yetu inakwenda kuzipata na kunufaika nazo. Mbele ya safari Hawa wachache wanaompinga Rais watapiga magoti mahala walipo kumuomba msamaha Rais kama kiongozi na katika uongozi najuwa ni kawaida kushambuliwa ba kiongozi mwenye maono hubaki katika msimamo anao amini utalipeleka mbele Taifa kiuchumi,Ndio maana Rais wetu kwa ushupavu na umadhubuti wake ameendelea kuwa mtulivu na na Kuendelea kuchapa kazi kwa ajili ya kuleta Tabasamu na matumaini katika mioyo ya watanzania.
 
Ni jambo jema

Jussa: Ya Bandari Hayatuhusu Pambaneni na hali zenu

Kanisa Moja Takatifu la Mitume
Ana akili sana Jussa kujibu hivyo, anawaambia ujinga wenu wa kuyakataa maendeleo mwisho chumbe. Soma hiyo habari juu huko, Zanzibar walisaini mikataba yao, kibindoni, ona wanafanya nini👇🏾

1687372170692.png

zanzibar domino commercial tower’, a spiraling skyscraper on a manmade island off the west coast of tanzania‘s zanzibar.

Tena natamani mama awaambie DP World wakafanye biashara ya bandari Zanzibar, halafu mizigo yao ya Tanzania bara yote tuifate Zanzibar, ndiyo tutajuwa kuwa hatujuwi.
 
Nawashangaa sana Tanzania chamber of Commerce na BET ambao ndiyo wanashughulikia mambo ya biashara baina ya Tanzania na nchi za nje...
Mbona hujafafanua ni mikataba kwenye maeneo gani, japo angalao michache.

Najua watanzania tunafanya biashara na Dubai kwa kiasi kikubwa sana, hasa sisi kununua bidhaa toka kwao kuliko sisi tunavyouza kwao. Kampuni yetu karibia kila mwezi tu-import, hasa parts toka Dubai, maana hapa kwetu zimejaa parts takataka toka China. Dubai hawatengenezi machines wala parts lakini parts nyingi kwenye machinery zinazotengenezwa na mataifa mbalimbali Duniani, utazipata Dubai, tena kwa bei nafuu kuliko ungeagiza toka kwa original manufacturing country.

Weka hiyo mikataba ili tuijue labda tutaziba pengo kati ya tunachonunua sisi toka kwao na wao watakachonunua toka kwetu.

Dubai ni kati ya maeneo yaliyofanikiwa sana kupata maendeleo kwa muda mfupi sana kuliko nchi yoyote. Maendeleo ya Dubai, kimsingi yalipatikana ndani ya miaka 15 tu.

Tungenufaika sana na Dubai kama tungejifunza toka kwao, wenzetu walifanya nini kwa muda mfupi kiasi kile cha kuigeuza nchi yao kutoka kwenye umaskini mpaka kwenye ustawi mkubwa. Nchi nyingine tulistahili kujifunza toka kwao ni Singapore, Mauritius na Botswana.

Tatizo, kwa kiasi kikubwa viongozi wetu wanaoenda nje huwa wanaenda kushangaa maendeleo ya wenzetu, na siyo kujifunza.
 
Back
Top Bottom