Habari ya Mungu isingekosa muongozo kwa watu watakaokuja kuishi South Pole ambako kuna siku zina jua kuwaka masaa 24 na usiku wa masaa 24.
Nakuuliza swali,je watu wa huko hawafungi ? Hawali Idd ? Umejibiwa swali kielimu lakini unauliza maswali ya kitoto. Nakupa faida uone kwamba jambo hili ishara linayo,ukisoma ishara za kiyama,hasa masiku atakayo ishi Masih Dajjaal,yatakuwa yanabadilika urefu na hii ni kwa hekima za Mola wetu mlezi,kwamba kuna siku itakuwa ina urefu wa mwezi,na siku moja itakuwa na urefu sawa na juma,wakauliza itakuwaje kuhusu muda wa sala,wakaambiwa watakadiria kutokana na sala iliyoanza kwa sala itakayofata.
Kila elimu ina misingi yake na ukinyimwa misingi ujue umenyimwa elimu husika. Mathalani leo hii hukuti aya wala hadithi inayosema madawa ya kulevya yamekatazwa,ila katika misingi ya sheria ni kweli kwamba madawa ya kulevya ni haramu,hii ni kwa sababu asili ipo ambayo ni uharamu wa pombe,uharamu wa madawa ya kulevya unaingia katika kipengele cha tawi kisha dosari inaingia katika kipengele cha ila yaani kudhuru akili,ndio maana nayo ni haramu.