Mkuu kuna baadhi ya fatwa nilizipitia za wanazuoni nyakati fulani nikaona wamegawa makundi mawili.
Kuna ambao wanasema wafuate nyakati za saudi arebia,kwa maana saudia wakifunga na kufungua na wao wafuate huko huko.
Alafu pia kuna wanaosema kwamba wafuate nyakati za nchi zao za jirani wanafungua vipi nao watafungua kwa kufuata nyakati za nchi jirani.
Kwa maana nyingine kwamba wanatakiwa wakadirie muda kama ambavyo wanatakiwa wakadirie muda wa kusali zile sala tano.
Kwa sababu kuna athari ilionekana kutoka kwa Mtume alisema..
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia Maswahaba wake wake kuhusu Dajjaal. Akaulizwa ni muda gani atakuwa juu ya ardhi, akasema, “Siku arobaini, siku moja itakuwa kama mwaka, siku moja itakuwa kama mwezi, siku itakuwa kama wiki na zinazobaki itakuwa kama siku zenu.” Kukasemwa, “Ee Mtume wa Allaah, siku ambayo itakuwa ni kama mwaka, je, swalah ya siku moja itatutosheleza juu yetu [kwa hiyo siku moja]?” Akasema, ”Hapana, mtu atazikadiria.”
Kwa maana suala hilo la siku kuwa ndefu ni suala ambalo sio la kawaida hivyo nyakati za sala zitakadiriwa kwa uzoefu wa yale masiku ya kawaida.