DSTV Tanzania Wanisababishia Uharibifu Nyumbani

hunchback

JF-Expert Member
Nov 10, 2014
658
289
Wanajukwaa wote nakuja kwenu kwa ushauri nichukue hatua gani.
Niliomba fundi kufanya decoder installation mwezi wa tano kutoka kitengo cha huduma kwa wateja. Nikaletewa fundi, wakaja wawili bwana.

Wakafunga decoder, wakati wa kufunga miguu ya tv, tv ikavunjika.
Wakiwa pale mafundi wakaniambia Tv za kisasa zina tabia ya kufanya self diagnosis hivyo nisijali tv itakaa sawa (ilikuwa inaonesha, ile pembeni kumepiga mstari kidogo).

Baada ya wao kuondoka nikaona tatizo linazidi ikabidi nipige simu huduma kwa wateja kuelezea.
Nikapewa ushirikiano ikiwemo wao kukiri kosa lilofanyika na kwamba watalifanyia kazi
(Ushahidi ninao wa maongezi yote).

Baada ya siku kadhaa nikaona nazungushwa, nikipiga simu sipati ushirikiano wa kutosha.
Baadaye wamekuja kuniambia kampuni haitahusika na uharibifu badala yake nimpeleke fundi mahakamani ili anilipe (fundi alikuja na mwenzake wakashirikiana kufanya kazi nilikuja kujuabaadaye kuwa siyo muajiriwa ni bodaboda).

Kiukweli hii imeniumiza sana, maana tv ilikuwa ni mpya (Hisense 58') na uzembe umefanyika ila Dstv Tanzania wanaruka kihunzi wakati wao ndio waliniletea mafundi.
 
Wewe nae ulizidi uzembe,wacha upate faida ya uzembe wako.
Hao DSTV hukufahamu Ofisi zao zilizpo baada ya hao vijana kuharibu hiyo TV yako.
 
Kwani ndugu ofisi ni lazima uende kimwili, kama napiga simu naongea na wahusika na wananihakikishia tatizo limepokelewa na linafanyiwa kazi (na ushahidi ninao) uzembe uko wapi?
 
Wanajukwaa wote nakuja kwenu kwa ushauri nichukue hatua gani.

Niliomba fundi kufanya decoder installation mwezi wa tano kutoka kitengo cha huduma kwa wateja. Nikaletewa fundi, wakaja wawili bwana. Wakafunga decoder, wakati wa kufunga miguu ya tv, tv ikavunjika.

Wakiwa pale mafundi wakaniambia Tv za kisasa zina tabia ya kufanya self diagnosis hivyo nisijali tv itakaa sawa (ilikuwa inaonesha, ile pembeni kumepiga mstari kidogo).

Baada ya wao kuondoka nikaona tatizo linazidi ikabidi nipige simu huduma kwa wateja kuelezea. Nikapewa ushirikiano ikiwemo wao kukiri kosa lilofanyika na kwamba watalifanyia kazi (Ushahidi ninao wa maongezi yote).

Baada ya siku kadhaa nikaona nazungushwa, nikipiga simu sipati ushirikiano wa kutosha. Baadaye wamekuja kuniambia kampuni haitahusika na uharibifu badala yake nimpeleke fundi mahakamani ili anilipe (fundi alikuja na mwenzake wakashirikiana kufanya kazi nilikuja kujuabaadaye kuwa siyo muajiriwa ni bodaboda).

Kiukweli hii imeniumiza sana, maana tv ilikuwa ni mpya (Hisense 58') na uzembe umefanyika ila Dstv Tanzania wanaruka kihunzi wakati wao ndio waliniletea mafundi.
fuata utaratibu Boss,andika malalamiko yako na upeleke ofisini kwao ukiambatanisha vivuli vya vielelezo vya wao kukupa mafundi wa kukufungia kingamuzi,risiti ya kununua kingamuzi husika pamoja na vielelezo vingine,huku ukiwapa muda wa wao kulifanyia kazi tatizo lako kabla hujafuata tartibu zingine.
 
Wanajukwaa wote nakuja kwenu kwa ushauri nichukue hatua gani.

Niliomba fundi kufanya decoder installation mwezi wa tano kutoka kitengo cha huduma kwa wateja. Nikaletewa fundi, wakaja wawili bwana. Wakafunga decoder, wakati wa kufunga miguu ya tv, tv ikavunjika.

Wakiwa pale mafundi wakaniambia Tv za kisasa zina tabia ya kufanya self diagnosis hivyo nisijali tv itakaa sawa (ilikuwa inaonesha, ile pembeni kumepiga mstari kidogo).

Baada ya wao kuondoka nikaona tatizo linazidi ikabidi nipige simu huduma kwa wateja kuelezea. Nikapewa ushirikiano ikiwemo wao kukiri kosa lilofanyika na kwamba watalifanyia kazi (Ushahidi ninao wa maongezi yote).

Baada ya siku kadhaa nikaona nazungushwa, nikipiga simu sipati ushirikiano wa kutosha. Baadaye wamekuja kuniambia kampuni haitahusika na uharibifu badala yake nimpeleke fundi mahakamani ili anilipe (fundi alikuja na mwenzake wakashirikiana kufanya kazi nilikuja kujuabaadaye kuwa siyo muajiriwa ni bodaboda).

Kiukweli hii imeniumiza sana, maana tv ilikuwa ni mpya (Hisense 58') na uzembe umefanyika ila Dstv Tanzania wanaruka kihunzi wakati wao ndio waliniletea mafundi.
kwa ninavyojua, dstv hawana mafundi, wanatuma aliyekaribu na eneo lako
 
Back
Top Bottom