DSTV na Error E16

Kilangi masanja

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
4,195
4,551
Ndugu wana tech habari yenu,

Juzi jioni nilifanya malipo ya package ya compat ya dstv 51000elfu na baada ya malipo kufanyika sikupata huduma ( picha) Nimewasiliana na customer yao zaidi ya mara 100 toka juzi majibu yao ni kua wanapitia changamoto ya huduma zao kua chini hivo tutapata huduma mda wowote.

Unachoambiwa n kuwasha dekoda yako na kisha uweke chanel namba 144, mara 118 bila mafanikio
Sasa kuna kitu kilichonitatiza niliuliza je endapo toka siku ya malipo sikupata huduma na mda unazidi kwenda je huduma zikirejea watafidia siku zilizopotea bila kupata huduma?Jibu la mtoa huduma lilikua lisilo na uhakika kwani alisema tu hana uhakika kama watafidia au laah.

Napenda kuuliza je kuna mtu mwingine aliefanya malipo ndani ya huu mda na amekumbana na hio changamoto, pia je endapo amepata changamoto hio ni nn mategemeo yake endapo wasipotoa fidia ya siku tulizopoteza? Nafikiria kutafuta mtu wa sheria niishitaki Dstv mahakamani.
 
Tumia Mydstv app ku fix hiyo error e16. Ni fasta tu. Leo nimelipia ikachukua kama dakika 15 iko na hiyo E16 nika fix kwa mydstv app. Au piga *150*53# utafata maelekezo.
 
Mkuu piga *150*53# then weka smart no yako, nenda option 2 fix error then no1 E16 ok. Hakikisha tv ipo on.

Next time unavonunua package hakikisha tv ipo on
Najua mzee hii ilikua shida yao tu dstv wenyewe kufix hio error najua bt haikufanya kazi
 
Back
Top Bottom