DSTV na AZAM kuna nini

DSTV na AZAM kuna nini

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2008
Posts
3,173
Reaction score
486
Wakuu habari
Mimi sio mtaalamu wa Dish wala mambo ya tv
Nilikuwa na DSTV lakini kwa kuwa ni mpenzi na shabiki wa michezo nikashawishika kufunga pia AZAM! Nina kama week moja hivi. Kwa kweli resolution ya AZAM iko bomba sana. Tatizo limejitokeza jana na leo! Maeneo niliyoko mvua zinanyesha sana! Cha ajabu ni kuwa mvua zikinyesha na madishi haya hayaonyeshi kabisaaaa. Kitaalamu nn shida. Nifanyeje kuzuia haya yasijitokeze?
Msaada please!
 
Anga likichafuka mawasiliano yanakua mabovu kati ya dish lako na satelite lengwa....
May be kuna extra solution kama kuongeza kifaa cha kuboost signal za LNB yako ...
Ila nijuavyo mimi hamna solution kwa the same size of dish.......
Just wait mvua iishe ule mambo...
 
mmmh! kumbe nalo hovyo! hii elimu ikiwekwa hapa nitaamua nichukue lipi manake startimes inanipa gonjwa la moyo na uzee huu!
 
ninachojua ni kwamba upepo unapovuma ndipo connection upotea ila mvua sina uhakika coz aijawahi nitokea hayo maelezo ni kwa DSTV coz AZAM ata sijui ikoje.
 
Wakati mwingine angalia kama mfungaji alikaza vinzuri, maanainawezekana ikinyesha mvua linayumbayumba hivyo kupoteza position yake.
 
Hivi Azam TV inaonekana Dar tu au na mikiani imeshafika??
Ina Channel zinazoonyesha English premier league au hamna.
 
ninachojua ni kwamba upepo unapovuma ndipo connection upotea ila mvua sina uhakika coz aijawahi nitokea hayo maelezo ni kwa DSTV coz AZAM ata sijui ikoje.

Mie ilikuwa inanitokea ila nikagundua fundi hakukaza wakati anafunga hivyo ikabidi kulikaza vinzuri. Baada ya hapo tatizo likaisha kabisa.
 
Mkuu nikwambie tuu hii ndo kitu ya kwanza kufanya jana na nilikuta liko very stable. Lakini leo imerudia tena
 
Du hapo mkuu inabidi niwaachie wataalamu wa haya madude

kitaalam ilo tatizo linaitwa rain feud/kama sijakosea mana nikitambo sana hayo mambo,ila tatizo lipo,na hauwezi kulikwepa ila kupunguza inawezekana,kosa la azam ni kwamba signal zao ziko chini sana,ikinyesha kidogo lazma ziteteleke,chamsingi kaza vizur dish,mvua ikiisha kula burudani.
 
Wakuu habari
Mimi sio mtaalamu wa Dish wala mambo ya tv
Nilikuwa na DSTV lakini kwa kuwa ni mpenzi na shabiki wa michezo nikashawishika kufunga pia AZAM! Nina kama week moja hivi. Kwa kweli resolution ya AZAM iko bomba sana. Tatizo limejitokeza jana na leo! Maeneo niliyoko mvua zinanyesha sana! Cha ajabu ni kuwa mvua zikinyesha na madishi haya hayaonyeshi kabisaaaa. Kitaalamu nn shida. Nifanyeje kuzuia haya yasijitokeze?
Msaada please!

Hilo ni tatizo ambalo ni gumu kulikwepa mkuu, maana mvua au maji na bad reflector ya signal yako.
maana pale tunahitaji signal ipate reflection kwenye dish ndio uone kwenye tv yako.
Hii inatokea kwa dish nyingi tu hata zile za wavu huwa tatizo hili linatokea mvua inaponyesha, si DSTV wala AZAM TV zote shida inatokea muda huo.
 
Ku Band ni nzuri kwa kuwa inaaccomodate channels nyingi ukilinganisha na C Band.Ila tatizo lake inabumbuliwa sana na mabadiliko ya hali ya hewa ukilinganisha na C Band.Kwa hiyo itabidi tu uwe mpole ndugu yangu.Hii mi naweza sema hata kwa signal strength ya kawaida tu,mvua ikinyesha Ku lazima inasumbua.May be upate Ku yenye nguvu sana,ambayo kwa hakika sijui kama inapatikana kirahisi ktk soko la hapa kwetu.
 
Hivi Azam TV inaonekana Dar tu au na mikiani imeshafika??
Ina Channel zinazoonyesha English premier league au hamna.

Ni satellite decorder so inapatikana kote kote. Mpaka Murongo kule wanaipata tu! Inaonesha mechi za VPL, kule kwingine ni chache tu. Bundle kwa mwezi ni 12k.
 
Wakuu habari
Mimi sio mtaalamu wa Dish wala mambo ya tv
Nilikuwa na DSTV lakini kwa kuwa ni mpenzi na shabiki wa michezo nikashawishika kufunga pia AZAM! Nina kama week moja hivi. Kwa kweli resolution ya AZAM iko bomba sana. Tatizo limejitokeza jana na leo! Maeneo niliyoko mvua zinanyesha sana! Cha ajabu ni kuwa mvua zikinyesha na madishi haya hayaonyeshi kabisaaaa. Kitaalamu nn shida. Nifanyeje kuzuia haya yasijitokeze?
Msaada please!
Ama kweli duniani tupo tofauti, yaani azam iwe bomba kuliko DSTV? anyway kiukweli Azam sijui, hata hivyo nadhani ni swala la hobby tu.
 
Sasa mkuu km Azam huijui Kwa nini hukubaliani na jamaa au ni hisia tu? Amesema resolution kwake ni nzuri binafsi nakubaliana nae, lkn pia amefunga azam Kwa sababu ya michezo akimaanisha Ligi ya Bara na sio EPL.
 
Mkuu, nimejaribu kuwa mkweli hapa kuwa Azam siijui totally (cause mi nipo Aru, ye yupo Dar), na nikaongeza kila mtu anacho kile anachokipendelea(hobby). na dhani umeainisha vizuri kama alivyosema. thats why nikaheshimu maamuzi yake mkuu.:A S thumbs_up:
tuko pamoja.
 
Back
Top Bottom