Dreamliner Boeing 787 yaanza safari za nje, yapeleka nyama ya mbuzi Dubai

Ikibeba majeneza ya wafu, maua toka Kilimanjaro sio cargo plane. Ikibeba container za nyama ya mbuzi inakuwa cargo plane!!!. Mpaka leo kuna wadanganyika hawajui ndege ya abiria ina tumbo kubwa la kupakia mzigo.
Sidhani kama inasehemu ya mzigo kubwa kubeba shehena kubwa usituhadae mkuu
 
kuna umuhimu wa business plan kabla ya kukurupuka kumwaga cash. lakini sio jambo jipya kwa maana watu fulani wakipata vihela tu basi hukimbilia minadani kununua radio kubwa mbilimbili na vitu vingine colourful bila plan yoyote (no offense)
Hahahahhahvumetisha nawajua hawa jamaa. Huwa nawaona mnadan wamevaa mashuka na but zilizofungwa na shanga ahahhahha

Sent using samsung galaxy grand prime pro
 
Nyinyi ndio ambao shuleni mnafuata ujinga. Ndege hiyo hiyo inabeba abiria na chini ya eneo wanalokaa kuna sehemu za mizigo.

Mkuu mjini umekuja na fuso ya viazi au yale malori ya kubebea ngombe?. Mambo madogo sana haya.
Hatukatai ndege kubeba nyama ya mbuzi kwenye buti,ila huwezi ukajaza basi mabegi kwenye buti then ukaikurupusha kwenda mwanza,kama ni mabegi tu yanasafirishwa si utatafuta lori tu linabeba,why utumie basi ya abiria kubeba mizigo-hata Tanroads hawatakuruhusu
 
Hii ni ya Tanzania tu under ccm,.Airline nyingine zote duniani wana cargo plane na hata siku moja wahawegeuzi passenger plane kuwa cargo plane,sasa kama ni hivyo wale waliobadirisha malori kuwa mabasi mbona mliwashughulikia-hii sina hakika hata kampuni ya boeing wataikubali maana ni kuwaharibia biashara in case of anything
Air meee
 
Ndege zote kubwa zina sehemu ya cargo kubwa sana ambayo kubeba mbuzi wengi ni rahisi sana.

Nadhani mngesoma japo kidogo kuhusu ndege na usafirishaji wa ndege.

Ikiwa mabasi tu ya siku hizi yanategemea sana cargo kuliko abiria, vipi kuhusu ndege? Fikiri.
Tusaidie ni shirika gani lingine liliwahi kubeba mizigo tu kwenye buti while siti zote ziko wazi then likafly to Dar or from Dar? wewe hujui unachoongea au unajitoa ufahamu tu
 
Hatukatai ndege kubeba nyama ya mbuzi kwenye buti,ila huwezi ukajaza basi mabegi kwenye buti then ukaikurupusha kwenda mwanza,kama ni mabegi tu yanasafirishwa si utatafuta lori tu linabeba,why utumie basi ya abiria kubeba mizigo-hata Tanroads hawatakuruhusu
Una uhakika upi kwamba ndege hiyo haikuwa na abiria ila ni mbuzi pekee?. Kosa ni la mleta uzi ambaye amepotosha watu kwa kuandika kana kwamba ni mbuzi pekee waliosafirishwa, na hili sio kosa la bahati mbaya ni kitu kimefanywa kwa makusudi ili mradi tu jamii ipate ujumbe hasi juu ya matumizi ya ndege.
 
Hii ndege imeshuka hadhi mpaka sasa kwa haya mambo!
Kwa ujinga tu wa watu. Mbona ni kawaida sana ndege kupakia wanyama. Nenda airpot upande wa cargo ukaone.

Hujamsikiliza vizuri mfanya biashara huyo wa Dubai? Walikuwa wanawaleta hao mbuzi Dar kwa masaa kumi na saba kabla ya kuwapakia kwenye ndege kwenda Dubai. Unafikiri walikuwa wanatumia ndege za mashirika yepi kuanzia hapo Dar? Of course itakuwa Emirates. Unajuwa midege ya Emirates kuwa ni luxurious zaidi na mikubwa zaidi lakini inapakia na hao mbuzi. Au ulikuwa huelewi hilo?

Mbuzi hawajaanza kusafirishwa leo kwa ndege kutokea Tanzania. Ethiooia ni biashara yao kubwa hiyo. Na walaji wa nchi za Gulf wanataka kitu fresh kwa fedha yao, kwanini tusiwape na sasa uwezo wa ndege tunao?
 
Una uhakika upi kwamba ndege hiyo haikuwa na abiria ila ni mbuzi pekee?. Kosa ni la mleta uzi ambaye amepotosha watu kwa kuandika kana kwamba ni mbuzi pekee waliosafirishwa, na hili sio kosa la bahati mbaya ni kitu kimefanywa kwa makusudi ili mradi tu jamii ipate ujumbe hasi juu ya matumizi ya ndege.
Habari hii imepotoshwa makusudi na kama kawaida nyumbu wamekurupuka bila kujali mtoni kuna mamba.
 
Kwa ujinga tu wa watu. Mbona ni kawaida sana ndege kupakia wanyama. Nenda airpot upande wa cargo ukaone.

Hujamsikiliza vizuri mfanya biashra huyo wa Dubai? Walikuwa wanawaleta hao mbuzi Dar kwa masaa kumi na saba kabla ya kuwapakia kwenye ndege kwenda Dubai. Unafikiri walikuwa wanatumia ndege za mashirika yepi kuanzia hapo Dar? Of course itakuwa Emirates. Unajuwa midege ya Emirates kuwa ni luxurious zaidi na mikubwa zaidi lakini inapakia na hao mbuzi. Au ulikuwa huelewi hilo?

Mbuzi hawajaanza kusafirishwa leo kwa ndege kutokea Tanzania. Ethiooia ni biashara yao kubwa hiyo. Na walaji wa nchi za Gulf wanataka kitu fresh kwa fedha yao, kwanini tusiwape na sasa uwezo wa ndege tunao?
Then wakisha pakia mbuzi wanafly to dubai bila abiria?
 
Tusaidie ni shirika gani lingine liliwahi kubeba mizigo tu kwenye buti while siti zote ziko wazi then likafly to Dar or from Dar? wewe hujui unachoongea au unajitoa ufahamu tu
Mpotoshaji ni aliyeupandisha uzi jukwaani, hakujiuliza kutaka kujua kuwa zaidi ya nyama za mbuzi nini kingine kilichosafirishwa ndani ya ndege hiyo.
 
Bei ya mbuzi UAE
Seven months ago Kashmiri sheep were sold at Dh400 but now they are priced at Dh600 to Dh650, Mr Yousuf said. The same goes for Somali goats, which used to cost Dh450 but now cost Dh600 for a 12-kilogram animal. “On Saturday I was in Dubai market and traders quoted me a price for two Somali goats at Dh1,400.
 
Back
Top Bottom