DRC yaahirisha kampeni ya chanjo ya AstraZeneca

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,008
9,873
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeahirisha kampeni ya kutoa chanjo ya AstraZeneca. Taifa hilo limepokea dozi milioni 1.7 ya chanjo hiyo dhidi ya Covid-19 na ilitarajiwa kuanza zoezi la kuchanja watu mnamo machi 15.

Waziri wa Afya Eteni Longondo amesema wameamua kuahirisha tarehe ya uzinduzi wa chanjo hiyo kama hatua ya tahadhari, baada ya nchi nyingine kadhaa kufanya uamuzi kama huo. Waziri huyo amesema tarehe mpya ya uzinduzi wa chanjo hio itatangazwa baada ya uchunguzi wa kiserikali na wa Kimataifa.

Denmark, Norway, Bulgaria na Iceland zimesimamisha utoaji wa chanjo hiyo juu ya hofu kuwa inasababisha kuganda kwa damu, na India imesema itafanya uchunguzi wa kina juu ya athari za baada ya chanjo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) hata hivyo limesema chanjo hiyo ni salama na hakuna ushahidi kuwa inasababisha madhara hayo.
 
Halafu hio chanjo si ndo ikapitishwa na WHO kwa ajili ya msaada kwa nchi masikini.....loh. vya bure sio
 
Naona ile ya Johnson and Johnson ndio kidogo afadhali daa kazi tunayo maana kuchanja kwa wasafiri ni lazima ila kwa wanaojifungia bandani hakuna ulazima kwa kweli ...
 
Behaviourist
King Kong III
brazaj

Hebu njoeni mchangie kidogo inakuaje serikali inaamua tu kusitisisha zoezi la chanjo ambazo zimethibitishwa na WHO,si wangeacha wenye kutaka kuchanjwa wachanjwe,au nasema uongo ndugu zangu?
 
we inaonekana ni mpinga sayansi, endelea kutumia uganga hta ukiugua usiende hospital. Afu kuhusu chanjo mataifa mengi sana yanaendelea kuitoa kama Marekani, Canada, Ujerumani, South Africa, Russia.. yani ni mengi sana hta siwez yataja yote
 
Sijajua tatizo langu lipi hadi uniandikie yote hayo? Nimeuliza tu inakuaje nchi inasitisha matumizi ya chanjo wakati WHO imeipitisha na inasisitiza kuwa ziendelee kutumika hazina tatizo? Ajabu unaniambia et napinga sayansi,sasa ni jambo lipi hapo la sayansi nililopinga?
 
DRC wamesitisha uzinduzi wa siku waliyopanga kuanza chanjo,watatangaza tarehe nyingine.

"Waziri wa Afya Eteni Longondo amesema wameamua kuahirisha tarehe ya uzinduzi wa chanjo hiyo kama hatua ya tahadhari, baada ya nchi nyingine kadhaa kufanya uamuzi kama huo. Waziri huyo amesema tarehe mpya ya uzinduzi wa chanjo hio itatangazwa baada ya uchunguzi wa kiserikali na wa Kimataifa."

Zingatia hapo baada ya uchunguziwa kiserikali na wa Kimataifa.
 
mwambie uyo mpinga chanjo, hajui lolote kuhusu sayansi
Sayansi sio imani mkuu kama unavyodhani na ndio maana hizo nchi zimeamua kusitisha ili kufanya uchunguzi pamoja na kwamba nchi zengine zinaendelea kutumia hizo chanjo na WHO inasema hazina tatizo,sasa kama unajiona wewe ndio unaijua sana Sayansi kuliko hizo nchi zilizositisha basi sawa.
 
Sayansi sio imani mkuu kama unavyodhani na ndio maana hizo nchi zimeamua kusitisha ili kufanya uchunguzi pamoja na kwamba nchi zengine zinaendelea kutumia hizo chanjo na WHO inasema hazina tatizo,sasa kama unajiona wewe ni unaijua sana Sayansi kuliko hizo nchi zilizositisha basi sawa.
Inabidi uelewe kuwa hakuna njia yoyote ya kumaliza ugonjwa wa Covid 19 zaidi ya chanjo. Mi nashangaa unavoonekana kufurahia chanjo kuzuiwa wakati watu wanakufa kila siku kwa corona. Halafu iyo chanjo ya Astrazeneca imeshatolewa kwa zaidi ya watu millioni 17 duniani, na kati yao ni 30 tu ndo wamepata changamoto. Huoni utofauti apo?
 
Kipi kilichokufanya useme nafurahia? Inaonesha mkuu umesikitishwa na hizi taarifa za baadhi ya nchi kusitisha matumizi ya hizi chanjo,wacha wafanye uchunguzi na matokeo yatakuwa ni faida kwa wote.
 
Oxford itashushwa vyeo maana hii chanjo yao kila mahali inakataliwa sio sawa na chanjo nyingine
 
Oxford itashushwa vyeo maana hii chanjo yao kila mahali inakataliwa sio sawa na chanjo nyingine
Sasa ikitokea ikapigwa chini hii chanjo sijui hali itakuaje kwa wale watu ambao wamekwisha chanjwa chanjo hii?
 
"Waziri wa Afya Eteni Longondo amesema wameamua kuahirisha tarehe ya uzinduzi wa chanjo hiyo kama hatua ya tahadhari, baada ya nchi nyingine kadhaa kufanya uamuzi kama huo. Waziri huyo amesema tarehe mpya ya uzinduzi wa chanjo hio itatangazwa baada ya uchunguzi wa kiserikali na wa Kimataifa."

Zingatia hapo baada ya uchunguziwa kiserikali na wa Kimataifa.

WHO ina wataalamu wa ukweli kuliko hao waganga wa kienyeji kutoka serikalini....Kama WHO washasema haina madhara na wanaendelea na uchunguzi wao hao waganga ni nani? Kama waganga wao wa kienyeji ni wazuri basi wangeteneza astazeneca ya kutumia kwao ambayo wataiamini....Dawa zozote au chanjo zina side effects kwa baadhi ya watu ,nasema side effects ,narudia tena SIDE EFFECTS....Wataalmu wa WHO wanaangalia positive results na ndio maana walisema hiyo chanjo effective rate yake ni juu ya 85%.
 
Back
Top Bottom