Draw ya makundi Caf Champions league: Simba ndani ya chungu namba 2, Yanga ndani ya chungu namba 3

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,664
18,039
CAF hufanya draw ya makundi kwa kuzigawa timu kwenye pots/vyungu 4 kwa kigezo cha ubora wao.

Pot no. 1: Al Ahly, Wydad WC,Esperance, na Mamelodi Sundowns.

Pot no 2: Simba, CR Belouizdad, Pyramids na Petro de Luanda.

Pot no.3: TP Mazembe, Al Hilal, ASEC Mimosa, na Yanga.

Pot no. 4: Etuile du Sahel, Jwaneng Galaxy, Nouadhibou na Medeama.

Kila kundi litakuwa na timu moja kutoka kila pot. Timu kwenye pot moja haziwezi kuwa kwenye kundi moja, bali timu kwenye pot tofauti zinaweza kuwa kundi moja. Kwa hiyo kuna uwezekano wa Simba na Yanga kuwa kwenye kundi moja!!

SWALI: Je mashabiki wa simba na Yanga wangefurahi kuwa kwenye kundi moja? Karibuni mtoe mawazo yenu hapa!!
 
Kwakua Simba wamekua wakilalamika Yanga wanabahati ya kukutana na vibonde, ingekua Jambo la maana Caf draw itengenezwe ata ki mchongo ili Simba na Yanga wawe kundi mmoja.

Hii itapunguza yale maneno ya kundi la vibonde.
 
SWALI: Je mashabiki wa simba na Yanga wangefurahi kuwa kwenye kundi moja? Karibuni mtoe mawazo yenu hapa!!
Kabla ya michezo ya raundi ya nne ya Ligi kuu ya NBC kufanyika, mashabiki wa Yanga walikuwa hawana hofu kupangwa kundi moja na Simba. Kwa sasa mawazo yao yamebadilika kabisa
 
Mamelodi Sundowns
Pyramid
Yanga
Etuile du Sahel

Esperance
Simba
Al Hilal
Medeama
 
Back
Top Bottom