Dr. Wilibrod P. Slaa: Special Thread

Dr. Wilibrod P. Slaa: Special Thread

kelele za chura......machozi ya samaki.....mbio za panya....na urais kwa chadema utaishia midomoni na kwenye maandamano

slaaa ndiyo kiboko yenu mafisi.Maccm yanaruka na kukanyagana kuelekea kuzimu
 
kwa taarifa yako....uchaguzi mwakahuu ccm haina mpinzani....ila vyama vya upinzani ndio vinapingana so kuna upinzani kati ya ACT na UKAWA
 
Huyu ndiye katibu mkuu makini kuwahi kutokea katika siasa za Afrika Mashariki na Kati
 
kwa taarifa yako....uchaguzi mwakahuu ccm haina mpinzani....ila vyama vya upinzani ndio vinapingana so kuna upinzani kati ya ACT na UKAWA

wewe huna akiri timamu au unaongelea matakoni mwa fisadi lowasa
 
thats positive mind mleta mada, nakupa heko mkuu.
 
Tuache ushabiki wa kisiasa kati waliotangaza nia za kugombea uraisi kupitia ccm wapo karibu 30 ni mgombea yupi mwenye CV inayozidi Dr.Slaa ?
watanzania wanayo haki ya kuwaangalia kwa makini hawa wagombea uraisi kupitia ccm kwani wengi wao wanakuja na sera ambazo wameshindwa kuzitekeleza wakiwa ndani ya serikali wanasubiri waje wapewe uraisi ndo waje kutuleta maendele huo ni usanii .
Kama ccm wameongoza kwa miaka 53 wameshindwa kutuletea maendeleo mpaka huduma za kijamii kama maji,zahanati ,shule n.k zimekuwa ni tatizo kubwa sana .
Waliotangaza nia za kugombea uraisi ndani ya ccm hakuna mwenye uwezo wa kuwaletea watanzania maendeleo .maendeleo yataletwa na utawala mpya wa UKAWA .Ndo maana hata ukiangalia waliotangaza nia za kugombea uraisi kupitia ccm hakuna mwenye CV inayomshinda Dr.Slaa hizo ni dalili tosha na salamu ccm wanapoteza muda wao bure hatuwezi kuwaamini tena .
View attachment 258826View attachment 258827
 
Tuache ushabiki wa kisiasa kati waliotangaza nia za kugombea uraisi kupitia ccm wapo karibu 30 ni mgombea yupi mwenye CV inayozidi Dr.Slaa ?

CV ndio inampa mtu uwezo wa kuongoza?
Mahiga unamfahamu?
Kama watanzania tutafuata maujinga kama haya na kuchagua viongozi wetu kwa vigezo vya anayejua kuongea kwenye midahalo,mwenye CV sijui ya aina gani,basi tutaendelea kuwa maskini kwa miaka mingi ijayo.
 
kwa hiyo unataka tuongozwe na mbunge mwenye CV kama Lusinde hajui hata kiingereza .
 
Habari Wakuu.Ninaleta kwenu Dr.W.P Slaa The Special Thread.Uzi huu una malengo makubwa mawili
  1. Kumshawishi Dr.Slaa aone umuhimu wa kuomba ridhaa ya kugombea urais kupitia UKAWA.Na vilevile kuwashawishi UKAWA waone busara ya kumptisha Dr.Slaa kupeperusha bendera ya UKAWA.
  2. Kuweka pamoja katika JF harakati za Dr.Slaa(kama atapitishwa) kuanzia kuchukua fomu,harakati zote za kipindi cha kampeni mpaka kusimikwa na kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
View attachment 258204View attachment 258206
Dr.W.P Slaa

View attachment 258227
Mama Maria Nyerere akimsihi jambo Dr.Slaa
Mambo 10 Kuhusu Dr.Wilbroad Slaa
1. Anachokisimamia

Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, umakini na uwajubikaji katika uongozi wa nchi na utendaji serikalini.
Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzania wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti.

2. Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Dk. Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

3. Mafanikio ya DK. Slaa kielimu na Kitaaluma

Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.

4. Mafanikio ya Dk . Slaa kikazi na kitaalamu

Dk. Slaa amefanya kazi katika maeneo na sehemu mbalimbali. Baadhi ya nyadhifa alizoshika na kazi alizofanya ni hizi zifuatazo:
Mkurugenzi Mtendaji, Chama chaü Wasioona Tanzania, 1992 – 1998
Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzaniaü (TEC), 1985 – 1991
Mkurugenzi wa Maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu), 19977ü – 1979 na 1982 – 1985
Padri wa Kanisa Katoliki kuanzia 1977 hadiü 1991

5. Vitabu alivyoandika

Utimilifu wa Msichana (1977) na Utimilifu wa Mvulana (1977)
Expediency and Exigency Liturgical Legislationü (1981)

6. Ufasaha katika lugha nane (8)

Dk. Slaa anajua kuzungumza na kuandika lugha nane za kimataifa zifuatazo:
Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.

7. Uzoefu wa Dk. Slaa Kisiasa

Dk. Slaa ana uzoefu wa musa mrefu katika shughuli za kisiasa. Baadhi ya nyadhifa alizoshika ni hizi zifuatazo.

Mbunge wa karatu kwa miaka 15 kutoka 1995 hadi 2010

Katibu Mkuu wa CHADEMA, 2002 hadi sasa
Makamu Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, 1998 – 2002

Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu wa CHADEMA kutoka 1995 hadi sasa

8. Uzoefu wa Dk. Slaa KItaifa na Kimataifa

Dk. Slaa ana uzoefu mbalimbali kitaifa na kimataifa kama ifuatavyo.

Mjumbe w akuwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la Afrika,Carribean na Pcific-FU (ACP-EUC Joint Assembly), 1996 – 2000.

Mjumbe kamati ya Uongozi (ACP-EU Joint Assembly)

Mjumbe katika Bunge la SADC kutoka 1998 hadi 2010

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge la SADC(Interü Parliamentary Cooperation and Capacity Building Committee) kutoka 1998 hadi 2010.

Nibu kiongozi wa kamati ya Upinzani Bungeni, 2006-2010

Mwenyekiti Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Bunge la Tanzania 2008-2010

9. Mafanikio kisiasa na kiutendaji

Dk. Slaa amekuwa mbunge wa karatu kwa miaka 15 mfululizo.
Karatu ni moja ya wilaya hapa nchini zenye maafanikio makubwa ikiwamo miundo mbinu bora, maji na huduma nyingine za kijamii, Dr. Slaa anataka kutumia uzoefu wake wa miaka 15 ya ubunge wa Karatu na uongozi madhubuti wa ukatibu mkuu CHADEMA, kwa ajili ya taifa zima.

Ndiye katibu Mkuu aliyefanikiwa zaidi kuijenga CHADEMA kwa kushirikiana na viongozi wengine ameweza kuipitisha CHADEMA katika changamoto mbalimbali na kukifanya kuwa chama kilicho tayari kushika uongozi wa taifa.

Bila kujali vitisho vya watawala aliibua rasmi kafsha za ufisadi mbaya kuliko zote zilizowahi kutokea hapa nchini zikihusisha wizi wa fedha za umma katika Benki kuu. Madai yake mazito Bungeni yalimlazimisha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu nchini kutoroka nchini.

10.Zaidi ya yote Dr.Slaa anajua maisha ya watanzania wa kawaida na mateso yao ya kila siku

Kuhusu List of Shame

Karibuni

.Dr Slaa ndio mtanzania pekee anaweza kufumua mfumo huu wa utawala uliofeli kutatua kero za watanzania na kubadili maisha ya watanzania. Dr Slaa anaweza kumaliza vita ya ufisadi, umaskini, rushwa, uchumi mbovu na tegemezi, yfukara. Dr Slaa anaweza kutuletea rasimu ya warioba kuhakikisha miiko ya uongozi na uwajibikaji na uadilifu. Dr Slaa ni hazina kwa watanzania na Taifa hili
 
familia tu hawezi kutunza sembuse urais...mpeni urais miaka miwili tu mtarudi mnalia Humu.....God forbid!!
 
CV ndio inampa mtu uwezo wa kuongoza?
Mahiga unamfahamu?
Kama watanzania tutafuata maujinga kama haya na kuchagua viongozi wetu kwa vigezo vya anayejua kuongea kwenye midahalo,mwenye CV sijui ya aina gani,basi tutaendelea kuwa maskini kwa miaka mingi ijayo.
CV ni zaidi ya shule.nini ilikuwa msimamo wa Mahiga tulipopitishwa na CCM kwenye EPA,Richmond,Wizi wa tembo,Katiba Mpya na Escrow?!
 
Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Willibrod Slaa
ameanza ziara ya siku nane
barani Ulaya ambako atashiriki
mijadala kuhusu hali ya
demokrasia na kukutana na jopo
la wataalamu wa masuala ya
uchumi kwa lengo la
kubadilishana uzoefu katika
kupata mifumo sahihi na
kujenga taasisi za kusaidia
uwajibikaji na kusukuma
maendeleo ya watu.
Katika ziara hiyo ya tatu baada ya
mbili alizofanya Marekani, Dk Slaa
anatarajiwa kukutana na kufanya
mazungumzo na viongozi
mbalimbali wa Umoja wa Ulaya
(EU) kuhusu hali ya demokrasia,
utawala bora na hali ya haki za
binadamu nchini hasa kwa
kipindi hiki ambacho Watanzania
wanaelekea kwenye Uchaguzi
Mkuu.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu
wa Idara ya Mambo ya Nje na
Uhusiano wa Kimataifa wa
chama hicho, Deogratias Munishi
ilisema: “Katika ziara hiyo,
viongozi hao wa Ulaya watapata
fursa ya kujadiliana na Dk Slaa
hali ya siasa kwa ukanda wa
Afrika Mashariki.”
Dk Slaa ambaye aliondoka
Jumamosi iliyopita,
ameongozana na Mkurugenzi wa
Bunge na Halmashauri wa chama
hicho, John Mrema na Mkuu wa
Idara ya Habari na Mawasiliano
wa Chadema, Tumaini Makene,
ameanza ziara akiwa ametoka
katika mikoa ya Kagera, Mbeya,
Rukwa na Katavi akikagua
uandikishaji wapigakura kwenye
kwa mfumo wa BVR na
kuhamasisha wananchi wenye
sifa kujiandikisha
 
Hizi ni takwimu za kura tulizopiga humu JF.Dr.Slaa amemfunika vibaya Lowasa "anayesafiri kwa matumaini" This poll will close on 2nd April
2016 at 12:35
Edward Lowassa 83 11.04%
Dr. Willibrod Slaa 623 82.85%
Wote hawafai/sijaamua 46
6.12%
Voters: 752.
 
Back
Top Bottom