Kabla ya jambo kubwa kama hili Mwenyekiti na Katibu walipaswa kukubaliana na kuafikiana, na ikishindikana kukubaliana na kama ni lazima Lowassa aingie basi walipaswa in advance waamue namna nzuri isiyowapa wasiwasi wananchi ya wao kufanya kabla ya Lowassa kuingia.Ata haikupaswa sasa wakati fomu zinatolewa ndio wawe wanaongelea hilo.
Bila shaka kuna tatizo Chadema kwenye hili, maana kwenye tukio la kutoa fomu kwa mgombea urais Dr Slaa kama katibu ndiye alipaswa kumpa fomu mgombea urais, hakuwepo. Tafadhari sasa watani zangu Chadema yamalizeni na Dr Slaa, mkiharibu hapa mtakuwa mmeharibu moja kwa moja.Mtakwenda kwenye uchaguzi mkiwa majeruhi na mtapigwa vibaya sana.
Wahenga walisema usiache mbachao kwa msala upitao, Lowassa atakuwa mtaji kama tu kama Chadema itabaki kama ilivyokuwa, lakini Chadema ikigawanyika basi Lowassa atakuwa ni mkosi, itatafsiriwa kuwa Lowassa kweli kainunua Chadema kwa pesa na sasa ndio makao salama ya mafisadi.Lifanyieni kazi haraka sana hili kama kweli lipo, Dr Slaa katu hampaswi kumpoteza sasa.