Dr. W. Slaa anaondoka CHADEMA

Dr. W. Slaa anaondoka CHADEMA

Binafsi nitamfuata Dr. Popote atakapo kwenda kwa maana huyu ndiyo rais wangu!
 
Kwanini ayafanye hayo usiku? Ofisi gani inafanya kazi usiku? kwani imekuwa kituo cha polisi?
Tulia dawa ikuingia mbona umepagawa Dr.Slaa anaenda kumuangukia Zitto sijui mtafanyaje mtabakia na fisadi Lowassa wasiwasi wa nini.
 
Ametengewa 10 Billion ili aondoke movie iendelee chadema kuna mpasuko.... Sisiem ndo kazini
 
mkuu Yericko Nyerere wajulishen wasemaji wa cdm waje walitolew tamko hili maana tumechoshwa na ukimya wao wakati lumumba wapo kazin
Mkuu mambo mengine huwa hayatolewi matamko. Wangetoa tamko kwa nini Dr. hajaonekana kwenye matukio ya CHADEMA yanayomhusu EL.

Walishindwa kutoa tamko kuhusu tuhuma kwamba EL alitoa 10 billion kujiunga na CHADEMA
 
Tulia dawa ikuingia mbona umepagawa Dr.Slaa anaenda kumuangukia Zitto sijui mtafanyaje mtabakia na fisadi Lowassa wasiwasi wa nini.

attachment.php
 
Kama si kweli mods naomba muifute a/c yangu, humu kutakuwa hakuheshimiki tena
 
Siwezi kumpigia kura yangu fisadi, Kama mbwai na iwe mbwai!
 
Nyie ni wale mkikaa mnaangalia 'movie' unakua unatafsiri matukio, ....."ona Rambo atamchapa kofi, subiri utaona.....!" Kwa nini msiache vitetesi, mtuache tuipate hiyo 'sapraizi' live????!!!!

sasa mtu unaangalia nae mkanda amekomaa tu "eti hapo rambo atakufa??" "hapo komando john hilo gari litamgonga?" yaani ni midadi tu 101,, inabidi tu umsimlie movie nzima
 
huyu kesha kula hela za maCCM kwahio ban kwake sio ishu.
 
Kabla ya jambo kubwa kama hili Mwenyekiti na Katibu walipaswa kukubaliana na kuafikiana, na ikishindikana kukubaliana na kama ni lazima Lowassa aingie basi walipaswa in advance waamue namna nzuri isiyowapa wasiwasi wananchi ya wao kufanya kabla ya Lowassa kuingia.Ata haikupaswa sasa wakati fomu zinatolewa ndio wawe wanaongelea hilo.

Bila shaka kuna tatizo Chadema kwenye hili, maana kwenye tukio la kutoa fomu kwa mgombea urais Dr Slaa kama katibu ndiye alipaswa kumpa fomu mgombea urais, hakuwepo. Tafadhari sasa watani zangu Chadema yamalizeni na Dr Slaa, mkiharibu hapa mtakuwa mmeharibu moja kwa moja.Mtakwenda kwenye uchaguzi mkiwa majeruhi na mtapigwa vibaya sana.

Wahenga walisema usiache mbachao kwa msala upitao, Lowassa atakuwa mtaji kama tu kama Chadema itabaki kama ilivyokuwa, lakini Chadema ikigawanyika basi Lowassa atakuwa ni mkosi, itatafsiriwa kuwa Lowassa kweli kainunua Chadema kwa pesa na sasa ndio makao salama ya mafisadi.Lifanyieni kazi haraka sana hili kama kweli lipo, Dr Slaa katu hampaswi kumpoteza sasa.
 
Kuna dalili za mpasuko huenda Dr slaa akazira. Illa wanajitahidi kuweka hali sawa wana chadema. Kwa sasa mambo sio mazuri huenda akaondoka. Elements zoote zinaonyesha kuna jambo. But time will tell.
 
Lengo halikuwa kumtoa kenge ukamuweka mamba! Fikiria kabla hujafanya maamuzi ya kuleta mawazayako hapo
...we ni kati ya wale wenye mawazo/fikra sizizokubali kubadilika....na wala sikushangai maana wabongo wengi mko hivyo....kwa fikra kama zako kule kenya (mfano) hadi leo ungeikuta KANU madarakani...maana kule wenzetu walizikubali tofauti zao wakaungana na kuwa kitu kimoja na kufanya yaliyotokea.....we naona huamini kuwa hata fisi anaweza kulishwa nyama na binadamu na hata kuwa rafiki yake ...kwa fikra zako sahau mageuzi nchi hii..maana huamini kwenye reconciliation...nyie ndio mkipewa nchi mnawageukia maadui zanu na kuwaangamiza.....acheni roho mbaya bana....
 
Back
Top Bottom