Dr. W. Slaa anaondoka CHADEMA

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,429
Najua wapo watakaobeza na hata kutukana lakini napata ushujaa wa kuyasema haya. Dk. Slaa usiku huu anaingia makao makuu kukabidhi gari, kadi, walinzi na cheo. Anajitoa CHADEMA. Naomba uzi huu uachwe hapa hapa ili baadaye nihukumiwe kwa haki.

Chanzo: Mimi mwenyewe.
Mtu aitwae #Manyerere Jackton ameandika mambo yasiyofanana na chembe ya ukweli kuhusu KM Dk. Slaa.

Bado tuko Ofisini. Kazi zinaendelea.

Hicho alichokiandika labda kama kinatokea kwenye ofisi ya chama kingine anachokijua Manyerere na kwa mtu mwingine tofauti na Dk. Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Nimuombe Jackton Manyerere, mpiganaji ambaye anapaswa kuwa na heshima yake kwenye tasnia ya habari afanye atimize wajibu wa kitaaluma katika kukusanya na kupasha habari badala ya uzushi na maneno haya yasiyo ya kweli.

Labda kama wameanza tena kufanya Kazi ile ile waliyokuwa mwaka 2010 ambako walimzushia Katibu Mkuu Dk. Slaa kila aina ya uzushi ambao Watanzania waliukataa.

Habari hizi za kuzusha na kutengeneza ndizo zilizotumika pia katika kampeni za mwaka 2005 ambapo hawa wanaozizusha leo mitandaoni walikuwa ndiyo timu ya utawala huu ulioshindwa. Wakimpamba mfalme kuwa amevaa nguo wakati yu mtupu. Kwa kila mapambo kuficha uvundo uliokuwa ndani ambao hatimaye leo unanuka (kushindwa) kila mahali.

Makene

 
Huyo Ndiyo Mwanaume na siyo wale akina Mbowe, Tundu Lisu,Lowasa &Co.!

Ndiyo Slaa wewe ndiyo ulipikwa na ukapikia na Unasimama kwa kile unachokiamini na siyo kuyumbishwa na kununulika Fedha, Mungu akutangulie kwenye safari yako, mchango wako unajulikana, na hakuna takataka yoyote yule atakayeweza kulifuta Hilo!

.
.
.
Respect!

 
Mod, najua wapo watakaobeza na hata kutukana lakini napata ushujaa wa kuyasema haya. Dk. slaa usiku huu anaingia makao makuu kukabidhi gari, kadi, walinzi na cheo. Anajitoa chadema. Naomba uzi huu uachwe hapa hapa ili baadaye nihukumiwe kwa haki.
Chanzo: mimi mwenyewe.
Na wewe umeanza kuwa muhuni au mabange umeanza kuvuta
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom