Shukrani!
Huna haja ya kunieleza kuhusu heshima ya UDSM, ndipo nilipopatia shahada yangu ya kwanza, ninapaheshimu sana na nitaendelea kuwaheshimu wote walionipa taaluma yangu ya awali kutoka Mlimani. Nimeweza kuendelea kitaaluma kutokana na elimu yangu ya awali niliyoipata UDSM! Kwa taarifa yako zaidi, situmii aina yoyote ya kilevi!
Mzee wangu na Mkuu;
Mimi nimekusoma mwanzo mpaka mwisho nimekuelewa vizuri sana na yote uliyasema pale juu hayana hata chembe ya shaka kwani hali ya utoaji taaluma katika vyuo vyetu vikuu vya sasa na hasa kuanzia miaka ya 1990 to date si ya kufurahisha na kujivunia hata kidogo!!
Wapo vijana wengi sana product ya vyuo hivi ambao ukiwaleta katika mazingira ya halisi ya utendaji kazi wa kutumia elimu shahada utashangaa kwani hawafanani na kiwango hicho cha elimu ya chuo kikuu.Na ni ukweli ulio wazi kuwa wengi hata uwezo wao wa kujieleza na kupambanua mambo ni mdogo sana, na hii inapokuwa hivi ni lazima uwatilie shaka hata walimu wanaowafundisha na kuwapika vijana hawa na hili si kosa hata kidogo kuwa na mashaka hayo!!
Ni wazi pia kuwa hili si kwa walimu wote,ila wengi ndivyo walivyo wa hovyo wanasaliti taaluma zao na ndiyo wanaowapa shahada-first class baadhi ya wahitimu wa dizaini ya Mwigulu Nchemba kwa sababu walipewa kitu kidogo ili watoe hiyo favor iliyo na long term effects katika jamii na taifa letu. Ndiyo maana kuna degree zingine zinaitwa za "chupi" kwa sababu wenye nazo walizipata kwa kulazimika kutoa rushwa ya ngono kwa profesa au Dr mwalimu flani aliyemsimamia ktk programu yake!!...Na madhara ya haya ndiyo tunayoyaona leo kwa kuporomoka kwa maadili ya taifa,utendaji mbovu ulio chini ya kiwango katika maeneo yetu ya kazi ya uzalishaji ktk ofisi za umma kuanzia
Ikulu hadi
ofisi ya mtendaji wa kitongoji
Huyu ndugu yetu aliyekuita kuwa wewe ni mlevi kwa sababu tu ya kutoa maoni yako kwa namna unavyoona mambo yanavyokwenda siku hizi ni lazima yeye ndiye mlevi na actually labda ndiyo product ya UDSM ya siku hizi. Kwa sababu kila alifikiri kuwa angekuja na maoni yaliyojaa hoja ya kupinga hoja zako yeye akaishia kutukana bila hata kusema kuwa nakuita wewe mlevi kwa sababu moja, mbili , tatu na kuendelea
Na
Dr W .P. SLAA ninayemfahamu mimi wa tangu anaingia bungeni mwaka 1995 mpaka anaingia na kushiriki ktk kinyang'anyiro cha kugombea Urais ktk General election ya 2010, ni msomi kwelikweli wa enzi zenu, mtu aliyejipambanua kwa hoja zake na ni mtu ambaye ndiye pekee katika BIG polical figures mwenye msimamo wa kuturejeshea maadili haya yaliyopotea. Wahafidhina kwa namna yeyote hawawezi kumpenda mtu wa namna hii, kamwe hawawezi kukubaliana na na hoja yake yoyote hata iwe nzuri namna gani itapotoshwa tu
Pole sana kwa kutukamnwa mzee wangu, nakuita mzee kwa sababu kama shahada yako ya kwanza uliipata miaka ya 1980, basi lazima utakuwa umekulakula chumvi kidogo....na hakika utusamehe bure tu sisi vijana wa uzao wa ALLY H. MWINYI, BEJAMINI W. MKAPA na sasa JAKAYA M. KIKWETE......vijana wa uzao wa utandawazi na soko huria!!