Dr. Ulimboka yupo mafichoni, kuzungumza wakati wowote!

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
  • YABAINIKA HAYUPO NYUMBANI, TAARIFA ZAKE ZAFANYWA SIRI, BABA, NDUGU, MARAFIKI WAGOMA KUZUNGUMZA

WINGU limegubika sakata la kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka siku moja baada ya kurejea nchini, huku watu wake wa karibu akiwamo baba mzazi, wakigoma kusema chochote kumhusu.

Dk Ulimboka alirejea nchini juzi akitokea Afrika Kusini alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu kwa takriban mwezi mmoja na nusu, baada ya kutekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo na Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu.

Ingawa wakati wa ugonjwa wake baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakitoa maelezo mbalimbali, jana wote waligoma kusema chochote, huku jitihada za gazeti hili kumpata nyumbani kwake zikigonga mwamba.

Baba mzazi wa Dk Ulimboka, Stephen Mwaitenda aliweka wazi kuwa ni vigumu kumwona daktari huyo jana.
Takriban watu wote waliofika nyumbani kwa Mzee Mwaitenda jana kumjulia hali Dk Ulimboka waliambiwa kuwa hayupo nyumbani.

Mwaitenda alilieleza gazeti hili kuwa ana furaha kuwa mtoto wake alirejea nchini salama licha ya kupelekwa Afrika Kusini akiwa taabani kutokana na kipigo.

Alipotakiwa kueleza juu ya kile kilichompata, mtoto wake huyo alisema: "Mungu na Steven mwenyewe (Dk Ulimboka) ndio wanaojua kilichotokea."

Aliongeza: "Kweli nimefurahi kwamba mwanangu amerudi, lakini siwezi kuelezea nini kilimtokea alipotekwa," alisema Mwaitenda.

Alisema Dk Ulimboka hayupo nyumbani na hajui kwamba angerudi wakati gani. "Hata kama angekuwapo, ni vigumu kumwona," alisema.

Kauli ya Katibu wa Madaktari
Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Edwin Chitage alisema madaktari walikuwa hawajaamua nini kingefuata baada ya Dk Ulimboka kurejea nchini.

Alisema hata hivyo, daktari huyo anahitaji muda wa kupumzika kwanza na familia yake.

"Aliporudi jana (juzi) alitumia muda wake kukaa na familia yake, mpaka sasa hatujajua hatua inayofuata. Dk Ulimboka atazungumza wakati mwafaka ukifika," alisema Dk Chitage.

Rais wa Chama cha Madaktari (MAT), Dk Namala Mkopi hakutaka kuzungumzia suala hilo akieleza kuwa alikuwa mkutanoni.

Dk Mkopi alitoa kauli hiyo baada ya daktari aliyemtibu Dk Ulimboka wakati wa tukio la kutekwa, Profesa Joseph Kahamba akiwa amesema yeye (Mkopi) ndiye angesaidia kupatikana kwa Dk Ulimboka ili azungumze na waandishi wa habari.

Dk Chitage alipoulizwa nini kinaendelea baada ya Dk Ulimboka kurejea nchini alijibu, "Hakuna kinachoendelea."

Aliendelea, "Leo hakuna kitu, tumepumzika na hata yeye tumemwacha apumzike na familia yake," alisema Dk Chitage.

Alisema Jumuiya hiyo na familia yake wanaandaa mazingira yatakayowezesha Dk Ulimboka kuzungumza na umma kupitia vyombo vya habari.

"Kuhusu hatua zitakazofuata tutaandaa utaratibu na tutawaarifu, juu ya hatua zipi tutachukua ikiwamo hili linaloumiza vichwa vya wengi la mazingira ya kutekwa kwake," alisema Dk Chitage.

Katibu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Rodrick Kabangila alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema yuko safarini na hajui kinachoendelea.

"Nipo Mwanza, nimesafiri na sijui kinachoendelea," alisema.

Alisema MAT itakutana kujadili suala hilo wakati wowote na kwamba utaratibu utaandaliwa kwa Dk Ulimboka kuzungumza na vyombo vya habari.

"Unajua sisi tuliomba kibali cha kuandamana kushinikiza Serikali kuunda tume huru kuchunguza tukio hilo na kuwabaini waliohusika tukakataliwa. Lakini sasa yeye amerudi na anawajua waliomdhuru. Tutaandaa utaratibu, atazungumza nanyi ili watu wote wajue," alisema Dk Kabangila.

Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Ananilea Nkya, alisema hakuwa na mawasiliano yoyote na Dk Ulimboka wala hajui kinachoendelea baada ya kuachana naye juzi Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.

Polisi wazungumza

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza kupitia msaidizi wake, alisema kuwa suala la Dk Ulimboka limefungwa na hawezi kulizungumzia tena kwa kuwa lipo mahakamani.
"Kamanda alikwishasema kuwa suala hilo lipo mahakamani hivyo hawezi kulizungumzia," alisema msaidizi huyo.

Alipoulizwa iwapo polisi ilikubali maombi ya madaktari kutaka tume hiyo ivunjwe na iundwe nyingine huru alijibu, "Tume inaendelea na kazi."

"Tume inafanya kazi yake na polisi pia wapo katika kazi zao," alisema na kukata simu.

Wanasiasa watoa wito

NCCR-Mageuzi, CUF na Democratic (DP) vimemtaka Dk Ulimboka kuwataja watu waliomteka na kumpiga.

Wito huo ulitolewa jana kwa nyakati tofauti na Katibu Mkuu wa NCCR-, Samwel Ruhuza, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro na Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila.

"Atumie roho yake na dhamira yake kuwataja watu waliomfanyia unyama ule ili jamii ijue na pengine ndio utakuwa mwisho wa watu kufanyiwa vitu vya aina hii," alisema Ruhuza.

Ruhuza alisema kuwa kiongozi huyo wa madaktari amerejea huku akiwa na afya njema, lakini bado ana deni kwa watu wasiopenda vitendo vya unyanyasaji.

"Ndiyo maana nikasema azungumze jambo hili kutoka ndani ya moyo wake," alisema Ruhuza.

Mtikila alisema licha ya kwamba Dk Ulimboka anatakiwa kuwataja waliomfanyia vitendo hivyo, yaliyomkuta yanatakiwa kupelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu.

"Nimeshazungumza na mtu mmoja kutoka mjini London, Uingereza amesema kuwa jambo hilo linawezekana," alisema Mtikila.

Alifafanua kwamba, atafanya kila njia ili akutane na Dk Ulimboka na kumshawishi akafungue kesi katika mahakama hiyo ili liwe fundisho kwa wanaopenda kuwanyanyasa Watanzania wanaodai haki zao.

"Nitafanya kila njia ili nionane na Ulimboka, hili jambo ni lazima lifike katika mahakama ya kimataifa ya haki za binadamu…, pia anatakiwa kuwataja waliomfanyia unyama huu," alisema Mtikila.

Kwa upande wake, Mtatiro alisema kuwa Ulimboka anatakiwa kukutana na vyombo vya habari na kueleza mambo yote ili kufichua yaliyokuwa yakifichwa na vyombo vya usalama.

"Ukweli utamweka huru na utawaweka huru watu wengi ambao wanaweza kufanyiwa unyama siku zijazo. Ikiwezekana afungue kesi ili haki itendeke," alisema Mtatiro na kuongeza:

"Ulimboka anatakiwa kufahamu kwamba Watanzania hawakukubaliana na mateso aliyopewa, unyama aliofanyiwa unalaaniwa na kila mtu," alisema Mtatiro.


Polisi: Tuko tayari kumlinda Ulimboka
Wednesday, 15 August 2012 07:27

Waandishi Wetu

JESHI la Polisi limesema liko tayari kumlinda kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka iwapo atahitaji ulinzi huo.Kauli hiyo imekuja siku mbili tangu daktari huyo wa magonjwa ya binadamu arejee nchini, huku usiri ukiwa umetawala taarifa zake kutokana na kutokuwapo kwa ndugu, jamaa au rafiki aliyekuwa tayari kusema chochote kumhusu.

"Nitachoweza kusema ni kwamba nashukuru mwanangu amerejea salama, lakini siwezi kusema chochote kuhusu mambo yanayomuhusu yeye," alisema baba mzazi wa Dk Ulimboka, Mzee Mwaitenda.

Tofauti na juzi ambapo nyumbani kwake kulikuwa na watu kadhaa akiwamo Mweitenda, jana mageti yote ya nyumba hiyo iliyoko eneo la Kibangu, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, yalifungwa na hapakuwa na mtu yeyote ndani.
Katikati ya hofu hiyo ya usalama, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema Jeshi lake haliwezi kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka bila yeye mwenyewe kuomba.

"Kwanza walishaamua (madaktari) kuchagua ulinzi, sisi tufanyeje? Atakapoona kuna ulazima atatujulisha," alisema Kenyela na kuongeza;

"Hatuwezi kupeleka askari bila kuombwa. Ukipeleka halafu akasema hawahitaji, itakuwa embarrasing (fedheha) sana. Sisi tunajua amerudi na tunamtakia heri aendelee vizuri, apone na aungane na wenzake,"

Kamanda Kenyela alifafanua kuwa nyumbani kwa mtu ni eneo la faragha ambalo polisi hawawezi kwenda bila kuombwa na kufanya hivyo, ni kitu kisichokubalika.

"Mimi kama kamanda sijapokea ombi lolote kutoka kwa Ulimboka wala kusikia tishio lolote dhidi ya usalama wake. Akiona kuna haja ya kulindwa, aseme tutakwenda," alisema.

Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova alisema hawezi kuzungumzia ulinzi wa Dk Ulimboka kwa sababu tayari madaktari waliomba ulinzi UN.

UN wagoma kuongea
Msemaji wa Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Hoyce Temu hakutaka kueleza endapo taasisi hiyo ya kimataifa ilikubali ombi hilo au la akisema, suala la ulinzi halipaswi kuwekwa hadharani.

Alifafanua kuwa iwapo suala hilo litawekwa hadharani ni sawa na kuwapa nafasi maadui kujua namna mipango ya ulinzi ilivyopangwa.

"Suala la security (usalama) kama lilivyo si suala la kuwekwa wazi kwa public (umma)," alisema Temu.

Mwanzoni mwa Julai mwaka huu, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kiliomba ulinzi kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) jijini Dar es Salaam kikieleza kuwa hakina imani na polisi.

Chama hicho kiliomba ulinzi huo baada ya kuwapo na madai kwamba kuna kikundi cha watu kimekusudia kumuua Dk Ulimboka wakati akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Katibu Mkuu wa MAT, Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa endapo UN ilikubali kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka alijibu "haikuwa lazima kwa UN kutujibu."

Aliongeza, "Sisi tuliwasilisha barua, tukitoa malalamiko yetu, namna gani watafanya kazi ya ulinzi siyo lazima watujibu, wao wanataratibu zao za kufanya kazi."

Daktari wake anena

Profesa Joseph Kahamba alisema hajaonana na Dk Ulimboka tangu arejee nchini Jumapili ila anaamini anaendelea vizuri.

Alipoulizwa imekuaje hajaonana na mgonjwa wake wakati yeye ndiye aliyemwandikia rufaa ya kutibiwa nje ya nchi alisema, "Siyo ajabu".

Alisema siyo lazima daktari aliyemwandikia mgonjwa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kuwasiliana naye anaporudi kwa kuwa hili linategemea hali aliyonayo mgonjwa husika.

"Hapa kuna mambo mawili; kuna kurudi akitakiwa tena kulazwa na kurudi kwa maana ya kupona," alieleza Profesa Kahamba baada ya kuulizwa kama ni lazima daktari aliyetoa rufaa awasiliane na mgonjwa baada ya kurudi kwenye matibabu.

Aliendelea "Angerudi (Dk Ulimboka) kwa state (hali) ya kulazwa, lazima angefikia kwangu nimwone, lakini kama amepona, anaweza kwenda kusalimia ndugu na kunywa bia kwanza halafu baada ya siku, wiki au mwezi akaja nikaonana naye."

Profesa Kahamba alieleza "Tangu Ulimboka arudi sijaonana naye zaidi ya kufanya mawasiliano na wenzake kwenye simu ila amepona kwa kuwa hajarudi kwangu."

MAT: Mwacheni apumzike

MAT kimewataka waandishi wa habari kutoendelea kumfuatilia Dk Ulimboka ambaye ni kiongozi wa jumuiya hiyo kwa kile walichoeeleza anatakiwa kupata fursa ya kupumzika.

Makamu wa Rais wa MAT, Dk Prinus Saidia alipotakiwa kueleza ni lini atajitokeza hadharani kufuta kiu ya Watanzania kuhusu kilichomsibu, alisema:

"Yeye mwenyewe ametuomba tumwache apumuzike kwa muda na sisi tumeona hili ni sahihi. Tumemwacha kwanza hadi hapo atakapotuambia kuwa yuko tayari kuungana nasi."

Dk Saidia alisema madaktari kwa umoja wao wamefurahi kuona Dk Ulimboka amerejea akiwa mzima na kwamba hilo ndilo jambo bora zaidi kuliko kitu kingine chochote kwa sasa.

"Tunamshukuru Mungu Dk Ulimboka amerudi akiwa mzima, hili ndilo lilikuwa la msingi. Hata hivyo, suala liko wazi mgogoro baina yetu (madaktari) na Serikali haujafikia mwafaka. Inatakiwa pande zote zikae na kukubaliana na si upande mmoja kutumia nguvu," alisema Dk Saidia.

Katika hatua nyingine habari kutoka ndani ya MAT zinasema viongozi wake wamekuwa wakifanya vikao vya ndani tangu juzi kujadili mambo mbalimbali likiwamo la kuandaa mazingira yatakayomwezesha Dk Ulimboka kuzungumza hadharani.

"Kuna vikao vinaendelea tangu jana (juzi), viongozi wanakutana kujadili mambo mbalimbali likiwamo namna Dk Ulimboka atakavyopata fursa ya kuzungumza," kilisema chanzo hicho.

Dk Ulimboka alitekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu.

 
Mi namsaidia kutaja wawili kama anaogopa...
Ramadhan Ighondu na Hemed Msangi.

Dr Uli ajue fika kuwa watanzania tunaijua picha ila kwa kuwa udhalimu umefanywa na serikali dhaifu ya CCM tunasubiri wakati muafaka after 2015 hawa madhalimu wote watinge kwa Pilato.

What goes around comes around. Kwa sasa hata suala likipelekwa mahakamani Ikulu itaelekeza aina ya hukumu ya kutoa. Kama ilivyoelekeza gazeti la Mwanahalisi lifungiwe milele
 

Tight security at Ulimboka's home, media kept at bay
Monday, 13 August 2012 22:36
By Mulemwa Mulemwa and Fariji Msonsa,
The Citizen Reporters
Dar es Salaam.

Security has been tightened at the home of Dr Steven Ulimboka, the chairperson of the Doctors Strike Steering Committee, who returned from South Africa on Sunday where he had been referred for treatment.

Dr Ulimboka was flown to South Africa six weeks ago after unknown people kidnapped him at gun point, tortured and left him for dead at Mabwepande forest in the outskirts of Dar es Salaam, off the Bagamoyo Road.Efforts by The Citizen to contact Dr Ulimboka at his Ubungo Kibangu home yesterday failed after relatives cordoned off the house making it hard for unauthorised persons to enter.

Spot checks established that the family reinforced the house fence by fixing a new gate, apparently to heighten security and keep unwanted persons out.The Citizen reporters were told that Dr Ulimboka was not at home and their efforts to seek permission to enter the home and talk to some of his relatives failed. Multiple phone calls to Dr Ulimboka went unanswered as well.

But this paper spoke to a person identified as Dr Ulimboka's father, Mr Steven Mwaitenda, who said he was happy that his son was back. However, when asked to comment on the brutal beatings which his son received after being abducted, he declined to comment.

"I rejoice that my son is back, but I have nothing more to say about the issue because I do not know what exactly he went through when he was abducted. It's only him and God who know what really happened," said Mr Mwaitenda.When asked to enquire from his son on behalf of the reporters what happened, Mr Mwaitenda insisted that his son was not at home at the time."But even if he was here you would not be permitted to see him because he needs time to rest," he warned.

 
Mkuu Ritz, nimeamini intelijensia ya Chadema inafanya kazi kama mpiga bao hivi kweli Tanzania kuna mafichoni? Mtu anayetaka kujificha anapokelewa kwa maandanamo? au ndio habari za kuuzia gazeti dada la mwanahalisi?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Ningekuwa mimi ningewataja wote hao mafirauni.

Alipofikia Ulimboka ni hakuna kurudi nyuma kwani kurudi nyuma ni kuwapa ushinda hao wadhalimu.

Nakubaliana nawe NN, kwa unyama waliomfanyia hakuna sababu ya kuogopa kuwataja wahusika wote hadharani na kusema kila kitu kilichojiri. Hata mimi kama ningefanyiwa unyama kama aliofanyiwa Dr Ulimboka ningesema kila kitu bila kuacha chochote kile kilichofanywa na hii Serikali dhalimu.
 
Ulimboka taja wote hao..una ulinzi mkubwa maana ukiguswa hata na jani wanatetemeka wakidhani watahisiwa.ITISHA MEDIA AFTER THAT UINDE UHAMISHONI SWIRTZERLAND.
 
YABAINIKA HAYUPO NYUMBANI, TAARIFA ZAKE ZAFANYWA SIRI, BABA, NDUGU, MARAFIKI WAGOMA KUZUNGUMZA
WINGU limegubika sakata la kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka siku moja baada ya kurejea nchini, huku watu wake wa karibu akiwamo baba mzazi, wakigoma kusema chochote kumhusu.
Dk Ulimboka alirejea nchini juzi akitokea Afrika Kusini alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu kwa takriban mwezi mmoja na nusu, baada ya kutekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo na Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu........
Ni vema akazungumzia ushiriki wa KUBENEA na Dk. DEO katika sakata la kutekwa kwake ili kukomesha tabia ya uchochezi ambayo inaweza kuhatarisha mshikamano wa Watanzania.
 
Ulimboka taja wote hao..una ulinzi mkubwa maana ukiguswa hata na jani wanatetemeka wakidhani watahisiwa.ITISHA MEDIA AFTER THAT UINDE UHAMISHONI SWIRTZERLAND.
Anaujua ukweli ndiyo maana nadhani kuwataja inakuwa vigumu, naye anaogopa. Kwanza watu wengine na vyombo vya habari vimeshatabiri waliohusika na inawezekana ni tofauti na anavyojua.

Inawezekana pia anaogopa kwa vile anajua waliomdhuru ni waathirika wa mgomo wa madaktari au hata maadui aliokuwa nao kabla ya mgomo wa madaktari.
 
Hata ajifiche wapi wakina zoka lazima wanajua yupo wapi ni vizuri aje awataje haraka haraka kiishe kwani issue yake imesababisha kufukunzwa kwa maofisa 30 wa Tigo
Kwa hiyo, mkuu unataka kusema wale waliofukuzwa Tigo nao sasa ni maadui zake? kaz kweli kweli.
 
Back
Top Bottom