Dr. Slaa si wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa si wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PJ, Aug 2, 2010.

 1. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  BAADHI yetu hatuna kawaida ya kuunga mkono wanasiasa kwa kiwango tunachoonyesha sasa kwa Dk. Wilbrod Slaa.
  Wanasiasa ni vigeugeu; wengi ni wasanii na mafisadi. Watakutumia leo, watakutupa kesho.
  Lakini wanapotokea wanasiasa makini wa viwango vya Dk. Slaa, hatuzungumzi tena lugha ya kutumiwa. Tunajitumia.
  Hii ni zaidi ya kujitumia. Ni kuunga mkono, kuweka nguvu ya ziada katika harakati za ukombozi ambazo Watanzania wamekuwa wanalilia kwa miaka kadhaa sasa.
  Maana kama tumekuwa tunasikitika kwa kuendelea kuishi chini ya ombwe la uongozi na kivuli cha ufisadi kwa miaka yote hii, hasa mitano iliyopita, tunasubiri nini kumuunga mkono mtu ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwashika mashati bila woga mafisadi na wasanii wa kisiasa?
  Katika wimbi hili jipya la mageuzi lililoikumba Tanzania baada ya Dk. Slaa kutangaza kugombea urais mwaka huu, limeondoka ombwe jingine, ambalo rafiki yangu na mchambuzi wa kisiasa, Absalom Kibanda, amenieleza kuwa lilikuwa linaukabili hata upinzani wenyewe.
  Wapiganaji ni wengi, viongozi na wakosoaji katika kambi ya upinzani ni wengi; lakini wanaolingana na haiba ya Dk. Slaa ni wachache.
  Nataka kuamini kwamba sasa, wapinzani wameshapata mgombea mmoja wa kumkabili Rais Kikwete. Na dhana hii ndiyo iliyonifanya niandike Jumapili iliyopita kwamba wakati sasa umefika, wapinzani wamuunge mkono Dk. Slaa.
  Lakini wapo baadhi ya wasomaji makini wa safu hii ya Maswali Magumu ambao walinikosoa kwa haki kabisa, wakisema wanaopaswa kumuunga mkono Dk. Slaa si wapinzani, bali Watanzania wote.
  Sababu ni kwamba Dk. Slaa anazungumza lugha ya wote. Anatetea masilahi ya wote. Na Ingawa amekuwa mbunge wa Karatu kwa muongo mmoja na nusu, wananchi ni mashahidi kwamba amekuwa mwakilishi wa Watanzania wote.
  Kwa kutazama wimbi hili na mvuto alionao kwa wananchi, ni haki kabisa kusema kuwa ingawa ana wadhifa wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Slaa sasa si wa CHADEMA.
  Si makosa kusema kwamba ingawa anagombea urais mwaka huu kwa tiketi ya chama hicho, Dk. Slaa si wa CHADEMA tena. Ni Slaa wa Watanzania.
  Ukweli huu, ukichanganywa na historia ya utendaji wa Dk. Slaa, ndio ulimfanya mmoja wa wasomaji hao niliowataja hapo juu kuniandikia ujumbe huu:
  “Nionavyo mimi, mapambano si kati ya chama na chama, bali kati ya uadilifu na ufisadi; au kati ya walalahoi na walanchi. Tujuane kwa vitendo si kwa vilemba vya sare.”
  Itawauma kina Yusuph Makamba (Katibu Mkuu wa CCM) na Pius Msekwa (Makamu Mwenyekiti wa CCM- Bara); lakini Dk. Slaa anaungwa mkono hata na wana CCM wenyewe.
  Na wiki hii nikiwa mikoani, nimekutana na wana CCM wengi ambao walikuwa wanaendelea na michakato ya kuwapata wabunge na madiwani wa majimbo yao, lakini kura zao za urais wameshaamua watampa Dk. Slaa.
  Nimekutana na baadhi ya wana CCM ambao wamekuwa wanakerwa na mwenendo wa chama chao katika siku za hivi karibuni; kwa sababu hiyo walishaamua kutopiga kura mwaka huu. Dk. Slaa amewaamsha na kuwapa sababu ya kupiga kura.
  Nimekutana na wananchi wa kawaida wanaoamini kwamba CCM ni wezi wa kura, na kwamba hata wakimpigia Dk. Slaa zitaibwa; lakini wamedhamiria wampigie ili nyoyo zao ziridhike.
  Wapo pia ambao walishaona siasa, hasa za upinzani, hazina maana. Wamebadilika na kuamka upya, na sasa wako nyuma ya Dk. Slaa.
  Nimekutana na wana CCM wengine ambao wangependa rais ajaye atoke CCM, lakini wanapolinganisha haiba za wagombea waliopo, nafsi zao zinawasuta. Dk. Slaa amewavuruga.
  Na mmoja wa makada wa CCM mkoani Mwanza amenieleza kuwa alichokiona siku Dk. Slaa alipozuru Mwanza kuomba sahihi za wadhamini, ni ajabu ya kisiasa yenye wingi wa watu ambao aliuona mwaka 1990 Tanzania ilipotembelewa na Papa Yohane Paulo II.
  Nimewasikia baadhi ya makada wakuu wa CCM na mashabiki wakuu wa Kikwete wakitamka wazi kwamba, “Dk. Slaa asipodhibitiwa anaweza kuwa kama Obama.”
  CCM wana hofu ya kushindwa. Jeuri ya Ushindi wa kishindo imenyauka. Wamegundua kwamba hata kama wangetumaini kura za wanachama wao (wanajikadiria kuwa milioni nne), kama Watanzania wataamua kufanya kweli, hizo za wana CCM hazitatosha.
  Lakini ukweli ni kwamba wana CCM wote hawawezi kukipigia chama chao kura; maana hata huko Karatu na kwingine ambako vyama vya upinzani vimekuwa vinashinda, ni kura za wana CCM na wapinzani.
  Watanzania wanaangalia mgombea kwanza, chama baadaye. Ndiyo maana nasema kuwa unapowaweka katika ushindani wagombea wakuu wawili wa urais, Jakaya Kikwete na Dk. Slaa, unakuwa unawatega Watanzania.
  Wapo ambao itikadi inawaelekeza wampigie kura mtu wa chama chao, lakini akili timamu na utashi wa nafsi zao vinawatuma kuzingatia umakini, wanafikiri na kuwaza juu ya muono mpya wa Tanzania; wanakerwa na ufisadi na wanajua kuwa CCM ni chama kilichozeeka na kuishiwa nguvu na upya unaostahili. Hawa watakaa upande wa Dk. Slaa.
  Waliobaki – wanaochagua kwa kufuata fadhila, chai, pombe, khanga, kofia au fulana; au walio na udugu au ukaribu wa lazima kwa mgombea wa CCM; wanaotegemea ufisadi ili waweze kuishi, wasiokerwa na usanii wa kisiasa uliofanywa na watawala waliopo; wasio na upeo wa kuona uwezo mdogo wa Kikwete katika miaka minne iliyopita, walio sehemu ya ombwe la uongozi ambalo tumelijadili kwa miaka mitatu mfululizo, watakaa upande wake.
  Kampeni hazijaanza rasmi. Lakini zitakapokuwa zimeanza, tunajua kuwa utakuwa ushindani mkali wa nguvu hizi mbili za Kikwete na Dk. Slaa. Tutahitajika kuwapima kwa vigezo halisi kutokana na kazi walizofanya, uwezo na upeo wao.
  Tutasikiliza hoja zao jinsi watakavyofanya tofauti na kinachofanyika sasa; na tutapima dhamira zao na nia zao, kwa kuwatazama pia wale walio nyuma yao, wanaowasindikiza Ikulu.
  Tutahitaji kutafakari vema majibu ya maswali tutakayowauliza. Tutawatazama usoni bila soni na kugundua mkweli na mwongo; fisadi na adili; kiongozi na msanii wa kisiasa; anayependwa na anayekubalika; mlanguzi wa kura na mwombaji wa kura; mwenye jipya na anayerudiarudia mambo yaliyochoka na kupauka; mwoga na rafiki wa mafisadi na mpambanaji jasiri dhidi ya ufisadi, shujaa wa Watanzania.


  Hapa hakuna la CHADEMA. Ni Utanzania. Na hii ndiyo bendera ambayo baadhi yetu tunataka ipeperushwe na Dk. Slaa. Tusisite, tusione aibu kutetea kitu chema. Watanzania muungeni mkono.  Source: By Ansbert Ngurumo Tanzania Daima
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,228
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Tunatamani yatokee haya na tuweke historia mpya. Zanzbar wameshaanza na mseto
   
 3. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  true that.
   
 4. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Go go Dr Slaa,
  I am just behind your knee
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,830
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  najua huyu ndo rais wangu.ujumbe wangu kwa wana jf, shawishi watu kumi na zaidi hakikisha wanapiga kura oct 31 kura yao iwe kwa chadema yaani rais dr slaa na mbunge wa chadema wa jimbo lako.
   
 6. bishoke

  bishoke JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante PJ kwa makala iliyokwenda skuli. Natamani makala hii ingesomwa na watu wengi zaidi ingeleta mabadiliko ya kifikra na kimtazamo pia. Kila la kheri Dr Slaa na kikosi chako.
   
 7. K

  Kijunjwe Senior Member

  #7
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 3, 2007
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kuna mambo ya kuzingatia katika kuchagua wabunge, kwa mtazamo ulionao CHIMUNGURU nadhani sio sahihi. Kikubwa nadhani tuchague wabunge wanaostahili kwenda bungeni kwa manufaa ya nchi. Hivyo basi, tunahitaji bunge lenye mchanganyiko wa wabunge na si bunge la chama kimoja(wabunge wengi toka chama kimoja) kama lilivyo sasa.
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  Aug 2, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,975
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  E bwana,CHADEMA ni vema.Amen!!!
   
 9. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ngurumo umeunguruma kwelikweli..! ni dhahiri kuwa Dr.Slaa anahitaji pia kura za wana CCM na wanachama wa vyama vingine kama anataka kushinda, hivyo basi itakuwa jambo la busara akijinadi kama mgombea wa watanzania wote zaidi ya kuwa mgombea wa CHADEMA pekee.
   
 10. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,358
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Tunaomba kura yako mkuu; soma alama za nyakati, si umeona ZNZ?
  Acha mapenzi yasiyo na muelekeo mkuu!! Vote for Dr. Slaa.

  Go Slaa Go...
   
 11. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ngurumo amepeleka ujumbe mzito kwa kweli.
  Watanzania wenzangu, bila kumsahau MS, tuitumie hii fursa jamani kuleta mabadiliko.
  Tuna kiu ya mabadiliko na mtu pekee wa kuyaleta kwa sasa ni Dr. Slaa
   
 12. C

  Chuma JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ...Ngurumo amepika hizo data? hujawai kuwa ktk newsroom? kuona namna waandishi wanavyopika data ili kujenga misimamo yao?....By the Way Slaa hawezi kuwa mgombea wa watanzania...bado ni Mgombea wa Chama chake...ready Vyama vingine vina wagombea wake tena makini kuliko SLAA...akishinda Urais ndio anaweza kuwa Rais wa Watanzania...waache watanzania wachague...!!
   
 13. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,813
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  "Nionavyo mimi, mapambano si kati ya chama na chama, bali kati ya uadilifu na ufisadi; au kati ya walalahoi na walanchi. Tujuane kwa vitendo si kwa vilemba vya sare.”
  Nimeipenda sana hiyo senteso! Dr Slaa ameweza kusimamia haki bila kujali vitisho na ameweka masilahi ya nchi mbele siku zote bila kuteteleka kwa hiyo ni wajibu wetu kumuunga mkono bila kujali itikadi za kivyama! Umefika wakati wa kuwapima viongozi wetu kile wanachokifanya ndani ya vipindi vyao vya uongozi si kwa sura zao wala ushabiki wa kichama! Miaka 5 ni kuguu na njia mpaka sole za viatu ziaisha kazi kutembeza bakuli huku mafisadi wakihamisha ni kejeli kubwa sana kwa nchi yenye rasilimali kiasi hiki! SASA USINGOJE KESHO, VOTE FOR DR SLAA
   
 14. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wagombea wanaweza kuwa wengi, wala usijali!! Lakini wengine wanaweza kuwa wagombea wa mafisadi, wagombea vibaraka, wagombea wa vyama na akawepo mgombea wa Watanzania!

  Piga kura kwa DK. Slaa
   
 15. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ngurumo kasema kweli, Slaa akiwa Rais watanzania wote mambo yetu yatakuwa poa. Hata marekani na ulaya watakuwa nyuma yetu. Watajifunza na kuiga kutoka kwetu. uchumi wetu utapanda kama ndege inavyopaa kuelekea angani na wote tutaishi si chini ya dola 10 kwa kila mtz kwa siku. Kwani Slaa ni sawa na mungu hatutahitaji kulima na tutakuwa tunakula asali na manna kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel. Tutawazidi hata majirani wetu ambao wao walichagua upinzani kama vile kenya, malawi, zambia na kwengineko kwani sisi ni kisiwa cha watu tufauti kabisa na hawa wengine. Itabidi tuamini hivyo ili tuwafurahishe wengi humu jf. viva oct 31, 2010.
   
 16. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kuanzia leo unapandishwa cheo na kuwa kingwendu badala ngwendu kwa post yako ya kuudhi wengi humu Jf
   
 17. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hizi siasa kwa kweli zina shida sana. Sasa huyu bwana anasema ukifananisha Slaa na JK, Slaa ana haiba sana na mvuto kwa watu. Hii inaleta mantiki kuwa Slaa akishinda anakuja kuongoza nchi hii peke yake? Unaposema watu wanachangu mtu na si chama, unataka kusema kuwa Freeman Mbowe hakuwa na mvuto mara zote alizogombea Urais na ndiyo maana akapigwa na chini. Sasa, wakati huo huo huyu Slaa akija kuwa rais wa nch,i ni nini position ya Freeman Mbowe na wasanii wengine wa chama chake ambao ni kibao?

  Makala kama hizi mwandikaji lazima awe anaweza sasambua sana hoja na si kuzizunguka. Inatakiwa kundwa hoja ya nguvu sana na si kusukuma hoja. Hadanganywi mtu hapa. Nakuhakikishia utawapata wachache sana hapa.....
   
 18. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #18
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ilirithi mdumo wa Uingereza, ambapo vyama vya siasa vimejigawa ki-itikadi. Conservative (Torries) - wenye navyo (viwanda, business na aridhi); Labour (Whigs) - wenye kuuza jasho lao ili waishi...wenye kuvaa ma-dangrees wakienda kazini; na Liberals (popo) kati ya vyama vya kwanza.

  Kiongozi wa chama hu-evolve kutokana na "mass" ya wanachama (prima inter pares) - wa kwanza kushinda wanachama wengine. Lakini siku za hivi majuzi, wa-Uingereza wamekuwa na dalili ya kuachana na vyama vikongwe na kujaribu kuunda mfumo wa vyama vipya - vilivyojikita katikati ya itikadi hizo!

  Baada ya kiongozi wa chama ku-evolve, ndiye anawekwa mbele kugombea wadhifa wa Waziri Mkuu. Kila chama huwa kinappaswa kuunga mkono hoja za chama chake huko Bungeni. Na wakati wa kura, ni lazima wa-Bunge wajikite ki-chama; hata kama m-Bunge ni mgonjwa hospitalini atapelekewa ambulensi aletwe ili apige kura!

  Zamani (miaka ya mitano ya muongo wa 1960), SISI TULIOPITIA High School ya wakati huo, husuasn wale tuliochukua somo la British Constitution, tulikuwa tunajadaili suala hili:

  I could vote for a pig if the party chose one. Hii ilionyesha kuwa itikadi ilikuwa na uzito mkubwa kwa wa-Uingereza kuliko "personality "ya mgombea, ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa chama cha siasa!

  Lakini uchaguzi wa wa-Uingereza uliopita umeingiza suala la "personality" na kuingiliwa sana na electronic media television).

  Huko ni Uingereza na hna hayo yao ya itikadi ndiyo tuliyorithi...lakini leo hii vyama vya siasa Tanzania havigawanyiki ki-itikadi!!!!!!!!!!!!!!!

  Vyama vinadai kuwa na itikadi: Eti, CCM ni ya Ujamaa na hata inalalia KATIBA ya nchi itamke hivyo! Wanamdanganya nani? Hivi wako wapi wanasheria wetu kukataa hayo...ama wao ni kutetea mafisadi tu ili wale vinavyoanguka chini mavumbini?

  Hivi what are the fundamental differences kati ya CHADEMA na CCM au CUF, katika eti dunia ya utandawazi? CHADEMA ni karibu ba rafiki zake Torries wa Uingereza na Republican wa Amerika...lakini kila mara hujinukiza na harufu ya waridi ya Nyerere Mjamaa aliyekuwa karibu na Whigs wa Uingereza!

  Tanzania itazidi kuyumba kisiasa endapo haitajifunga ki-itikadi!

  Mwisho, so long as u-Bunge ni kutengeneza mamilionea, kila mtu atautafuta! Matokeo yake: Tutakuja kuuana bure! Dawa, punguza mishahara na marupurupu ya wa-Bunge ili wenye moyo ndio watuongoze, kama ilivyo huko Ubelgiji au Uingereza, sio wenye kulilia kuwa mamilionea!

  Narudia tena, hayo mamilioni ndio yana-pollute the political environment ya Tanzania! Na TAKUKURU yaitayamaliza!

  Safari hii, tumeona wagombea hata wa chama kimoja wakiptwangana ngumi! Rushwa imatapakaa! Itakapofika kwa wapiga kura, Tanzania ijiandae, pengine, kwa kumwaga damu…and I am not an alarmist...
   
 19. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,020
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  We are together but lets play our part. PIGA KURA TAREHE 31 OCTOBER
   
 20. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,020
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mh, Hilo nalo kubwa!
  I think watanzania wataingia huko hata bila wao kujua wanakoelekea. Hali siyo nzuri maana rushwa haiwezi kuhalalishwa namna hii.
  Lets hope FOR CHANGE!
   
Loading...