Dr. Slaa si wa CHADEMA

Kwa knowledge yangu ndogo ya IT, kuna kila dalili kwamba Malaria Sugu ni moja kati ya Mods humu. Naombeni nisishughulikiwe.
 
...Ngurumo amepika hizo data? hujawai kuwa ktk newsroom? kuona namna waandishi wanavyopika data ili kujenga misimamo yao?....By the Way Slaa hawezi kuwa mgombea wa watanzania...bado ni Mgombea wa Chama chake...ready Vyama vingine vina wagombea wake tena makini kuliko SLAA...akishinda Urais ndio anaweza kuwa Rais wa Watanzania...waache watanzania wachague...!!

Nadhani unatania tu. Hao wagombea wa upinzani wanaokimbilia Ikulu ni wa kuogopa kama ukoma. Dr Slaa ameombwa kwenda Ikulu na watanzania. CCM wenyewe wanalijua hilo, ni Slaa pekee tishio lao. Ulisikia jana JK na Makamba wanavyolalamika kwa wanachama wao na kumtaja Slaa? kwa nini wengine hawatajwi? SONGA MBELE SLAA, WATANZANIA WANAKUOMBEA NA WANAKUPENDA, KWANI UNARUDISHA MATUMAINI YALIYOPOTEA.
 
good lkn wanaosoma maelezo yako haya ni wasomi tu,je ikuwaje kwa wale wa chini haswa kina mama wanaopewa 2500 na kuridhika na kutoa kura yake kwa huyo mtu? bado tuko mbali ila nakubali kutakuwa na changamoto kubwa kwa siasa za nchi hii,lingine wapizani wa nchi hii wengi ni mapandikizi na ndo maana hawataki kuungana,
 
tufikie mahali tuongee kidogo..tutende zaidi...maelezo na makala ni nzuri sana na zimejaa ujumbe mzito ila kuna kitu cha muhimu zaidi kuliko hizi mkala yaani..............TWENDENI SASA TUKAMPIGIE KURA YA NDIO DR.SLAA NA KUWASHAWISHI NDUGU,JAMAA,MARAFIKI ZETU WENYE MAPENZI MEMA NA NCHI HII wampe kura yao Dr.Slaa
Pamoja tutashinda na saa ya ukombozi ndiyo hii.
Amen
 
Hizi siasa kwa kweli zina shida sana. Sasa huyu bwana anasema ukifananisha Slaa na JK, Slaa ana haiba sana na mvuto kwa watu. Hii inaleta mantiki kuwa Slaa akishinda anakuja kuongoza nchi hii peke yake? Unaposema watu wanachangu mtu na si chama, unataka kusema kuwa Freeman Mbowe hakuwa na mvuto mara zote alizogombea Urais na ndiyo maana akapigwa na chini. Sasa, wakati huo huo huyu Slaa akija kuwa rais wa nch,i ni nini position ya Freeman Mbowe na wasanii wengine wa chama chake ambao ni kibao?

Makala kama hizi mwandikaji lazima awe anaweza sasambua sana hoja na si kuzizunguka. Inatakiwa kundwa hoja ya nguvu sana na si kusukuma hoja. Hadanganywi mtu hapa. Nakuhakikishia utawapata wachache sana hapa.....

Mimi kinachonichekesha na kunishangaza ni kuwa humu jf wanataka tuamini kwamba slaa atakuwa ndo suluhisho la kila kitu wakati watanzania ni walewale, shule yao ndogo na wasomi wanaotumika sasa ni haohao atakaowatumia au atashuka na wake toka mbinguni! Bila shaka wengi mliopo humu siajabu hamna uzalendo wa kweli bali mna viahadi vya maslahi ndo maana hamtaki kuandika na kusema ukweli. Ubnafsi umewajaa. Umimi umewajaa. Ndo maana hata ukileta wazo la chama kingine cha upinzani utaishia kutukanwa tu humu. Ngoja niseme ukweli tu japokuwa wengi JF mtachukia, mtatamani hata kuning'ata, buy yes ngoja niseme ukweli. Nashauri kama ingewekwa wazi tu kuwa hii ni Chadema forum. Bila shaka isingekuwa tatizo kwa wachangiaji wengine wasiokuwa wanachadema hata kama ni wapinzani wachama tawala. Na pia nchi haiongozwi na ntu mmoja na urais ni taasisi. Tumeona mabadiliko sehemu nyingi sana sehemu mbalimbali na hata majirani zetu hapa, nani anaweza kutuambia ninini hasa cha maana walichofanya. Mwai Kibaki kati anaingia madarakani alisema kuwa atabadilisha katiba ndani ya siku 90, mpaka uchaguzi mwengine ulifika hajafanya lolote.
Kwa hiyo tuache kuongopena, Slaa hajawahi kuwa hata mkuu wa mkoa/wilaya, hakuna anayejua utendaji kazi wake zaidi ya kuongea bungeni. Akina Brown hivyo hivyo, walikuwa watendaji wazuri sana chini ya akina Bliar lakini sote ni mashahidi jinsi alivyochemsa. Haya hayatoshi tu kuwa somo kwetu? au tunasubiri mwalimu aje na chaki ubaoni ndo tujue?
Lets we be realistis, kama unamasilahi labda ya ahadi za uwaziri kitu ambacho naamini Zito atakuwa nacho dhena leta sifa kama za Ngurumo, lakini kama wewe ni mwenzangu na mimi just write the reality, acha ushabiki usiokuwa na tija.
Bila shaka nitakuwa nimeeleweka kata kama nitapanda cheo na kuwa kingwendu kama mwalugali alivyosema.
 
hii ni Chadema forum
Jitoe humu kama unaliamaini hilo.

Mwai Kibaki kati anaingia madarakani alisema kuwa atabadilisha katiba ndani ya siku 90, mpaka uchaguzi mwengine ulifika hajafanya lolote.
Kwa hiyo tuache kuongopena
Mfano wako hauna mashiko,ona Obama anafanya nini kwa sasa...
Slaa hajawahi kuwa hata mkuu wa mkoa/wilaya, hakuna anayejua utendaji kazi wake zaidi ya kuongea bungeni

Inaonekana hufuatiliagi mijadala ya Bunge ambayo ina masilahi kwa Taifa...
Jiulize Issue za EPA, Deep Green Finance,Meremeta ni nani alikuwa anazisema bila kumung'unya maneno Bungen...Dont forget list of shame (Muungwana akiwa ndani ya Nyumba) na hawajakana bado.
Suala la Masilahi na ahadi za kishkaj utalisemaje kwa serlikali ya JK
 
Asante PJ kwa makala iliyokwenda skuli. Natamani makala hii ingesomwa na watu wengi zaidi ingeleta mabadiliko ya kifikra na kimtazamo pia. Kila la kheri Dr Slaa na kikosi chako.
Print makala hii halafu toa photocopy nyingi sana halafu sambaza. Ni 2 pages hivyo kwa photocopy itacost 100/=. Kama umeguswa sana na suala hili, ukitumia 20,000/=, utatengeneza copy 200 ambazo wakisoma kwa kupokezana watu 5 then ujumbe utakuwa umewafikia watu 1000!
Let us act now.
 
Hapa hakuna la CHADEMA. Ni Utanzania. Na hii ndiyo bendera ambayo baadhi yetu tunataka ipeperushwe na Dk. Slaa. Tusisite, tusione aibu kutetea kitu chema. Watanzania muungeni mkono.

Source: By Ansbert Ngurumo Tanzania Daima

Jibu kwa Ansbert,

As long as Slaa anagombea kama mgombea wa CHADEMA tu bila ya kuungwa mkono ama kuungana na wenzake atleast CUF na NCCR Mageuzi basi huyo ni mgombea wenu CHADEMA na sio wa watanzania. Hizi propaganda zenu mzifanye kukiwa na nia thabiti ya kumfanya awe mgombea wa watanzania na mojawapo ni kuchana na upuuzi wa kutokuaminiana na kuonana kuwa wenzenu wanatumiwa na CCM kuliko ninyi wakati attitude hiyo tu inayopelekea kutokuunganisha nguvu ni moja ya aina ya kutumiwa na CCM.

Lakini pia dawa pekee ya kuondokana na mazingira ya kufanikiwa kwa tuhuma na propaganda za udini kwa upande na ukabila (Uchaga - Ukristo) na CUF (Uislamu - Uswahili) ni kuungana na sio kuwatuma watu ambao kwa undani wanaamini kuwa watafaidika na siasa hizo kukanusha.

Waambie hao mabosi wako kuwa bila ya kuungana ama kushirikiana wajiandae na adhabu ya nguvu ya umma.

omarilyas
 
Kwa hiyo Kikwete ni Rais wa CCM?
 
Jitoe humu kama unaliamaini hilo.

Mfano wako hauna mashiko,ona Obama anafanya nini kwa sasa...

Inaonekana hufuatiliagi mijadala ya Bunge ambayo ina masilahi kwa Taifa...
Jiulize Issue za EPA, Deep Green Finance,Meremeta ni nani alikuwa anazisema bila kumung'unya maneno Bungen...Dont forget list of shame (Muungwana akiwa ndani ya Nyumba) na hawajakana bado.
Suala la Masilahi na ahadi za kishkaj utalisemaje kwa serlikali ya JK
Ndugu utofautishe kuongea na kuact, hivi ni vitu viwili tofauti. Kila siku huwa anaongea sijui Mkapa alifanya hivi na vile unafikiri akiwa rais anaweza kumfikisha Mkapa mahakamani? Ni rahisi kihivyo? Mimi naona tumepoteza mtu mhimu sana bungeni kwani huwa nafurahia sana jinsi anavyojenga hoja. Lakini hilo halimaanishi kuwa na kuact itakuwa hivyo. Lakini pia nawasiwasi na huyu bwana anaweza akatufikisha pabaya kwani inaonekana si mvumilivu kabisa. Kama mtakumbuka alivyowafukuza uongozi wanachama wenzake kwa sababu tu watofautiana kitu ambacho ni cha kawaida kabisa hata mke na mme au kaka na dada hutofautiana. Je akiwa na mamlaka ya juu na akaingiza interest zake na kakikundi kake tutapona. Si tutakuwa tumejichimbia kaburi wenyewe na tutaanza kupigana? Again and again tuangalie haya mambo kwenye 3 dimension kama kweli tunataka tuwe salama.
 
Kauli mbiu ni DR SLAA, RAISI WA WATANZANIA, AMEONYESHA UAMININIFU KWETU NA NI LAZIMA TUUNGANE NAYE
 
Leo tarehe 4/8/2010, dola moja nimenunua kwa 1,588, halafu Mkulo anatuambia uchumi umeimarika,sisi siyo wajinga wa kiasi hicho,Tunaomba mpumzike mtuachie nchi yetu salama, ninaamini mpaka mwezi wa kumi pesa yetu itakuwa chini ya ile ya Zimbabwe
 
Jibu kwa Ansbert,

As long as Slaa anagombea kama mgombea wa CHADEMA tu bila ya kuungwa mkono ama kuungana na wenzake atleast CUF na NCCR Mageuzi basi huyo ni mgombea wenu CHADEMA na sio wa watanzania. Hizi propaganda zenu mzifanye kukiwa na nia thabiti ya kumfanya awe mgombea wa watanzania na mojawapo ni kuchana na upuuzi wa kutokuaminiana na kuonana kuwa wenzenu wanatumiwa na CCM kuliko ninyi wakati attitude hiyo tu inayopelekea kutokuunganisha nguvu ni moja ya aina ya kutumiwa na CCM.

Lakini pia dawa pekee ya kuondokana na mazingira ya kufanikiwa kwa tuhuma na propaganda za udini kwa upande na ukabila (Uchaga - Ukristo) na CUF (Uislamu - Uswahili) ni kuungana na sio kuwatuma watu ambao kwa undani wanaamini kuwa watafaidika na siasa hizo kukanusha.

Waambie hao mabosi wako kuwa bila ya kuungana ama kushirikiana wajiandae na adhabu ya nguvu ya umma.

omarilyas

Wivu tu unakusumbua huna lolote...
 
Leo tarehe 4/8/2010, dola moja nimenunua kwa 1,588, halafu Mkulo anatuambia uchumi umeimarika,sisi siyo wajinga wa kiasi hicho,Tunaomba mpumzike mtuachie nchi yetu salama, ninaamini mpaka mwezi wa kumi pesa yetu itakuwa chini ya ile ya Zimbabwe

Kibaya zaidi mishahara yetu tunapokea kwa Tshs, hutakiwi kutumia akili nyingi sana kujua uchumi wetu ni kaputi - mafuta juu, vyakula bei inapanda kiholela, hii nchi ya watu wa aina gani? Nafikiri jibu tumpe nchi hii DR. Slaa arekebishe haya mambo mapema tusije fikia level ya kuwa omba omba kwenye nchi yetu yenye mali kibao. Kila siku tunapongezana eti amani na utulivu - hii amani itatoweka kama wengine wanakula kuku sisi ugali wa pumba - tena kwa pesa za wizi hiyo amani itatokea wapi? huyu Mkulo mimi huwa simsikilizi na simwamini kabisa na hizo data zake za vitabuni. Nina imani watanzania si wajinga tena nafikiri sasa ni wakati muafaka wa kuishangaza CCM.
 
Back
Top Bottom