Mimi kinachonichekesha na kunishangaza ni kuwa humu jf wanataka tuamini kwamba slaa atakuwa ndo suluhisho la kila kitu wakati watanzania ni walewale, shule yao ndogo na wasomi wanaotumika sasa ni haohao atakaowatumia au atashuka na wake toka mbinguni! Bila shaka wengi mliopo humu siajabu hamna uzalendo wa kweli bali mna viahadi vya maslahi ndo maana hamtaki kuandika na kusema ukweli. Ubnafsi umewajaa. Umimi umewajaa. Ndo maana hata ukileta wazo la chama kingine cha upinzani utaishia kutukanwa tu humu. Ngoja niseme ukweli tu japokuwa wengi JF mtachukia, mtatamani hata kuning'ata, buy yes ngoja niseme ukweli. Nashauri kama ingewekwa wazi tu kuwa hii ni Chadema forum. Bila shaka isingekuwa tatizo kwa wachangiaji wengine wasiokuwa wanachadema hata kama ni wapinzani wachama tawala. Na pia nchi haiongozwi na ntu mmoja na urais ni taasisi. Tumeona mabadiliko sehemu nyingi sana sehemu mbalimbali na hata majirani zetu hapa, nani anaweza kutuambia ninini hasa cha maana walichofanya. Mwai Kibaki kati anaingia madarakani alisema kuwa atabadilisha katiba ndani ya siku 90, mpaka uchaguzi mwengine ulifika hajafanya lolote.
Kwa hiyo tuache kuongopena, Slaa hajawahi kuwa hata mkuu wa mkoa/wilaya, hakuna anayejua utendaji kazi wake zaidi ya kuongea bungeni. Akina Brown hivyo hivyo, walikuwa watendaji wazuri sana chini ya akina Bliar lakini sote ni mashahidi jinsi alivyochemsa. Haya hayatoshi tu kuwa somo kwetu? au tunasubiri mwalimu aje na chaki ubaoni ndo tujue?
Lets we be realistis, kama unamasilahi labda ya ahadi za uwaziri kitu ambacho naamini Zito atakuwa nacho dhena leta sifa kama za Ngurumo, lakini kama wewe ni mwenzangu na mimi just write the reality, acha ushabiki usiokuwa na tija.
Bila shaka nitakuwa nimeeleweka kata kama nitapanda cheo na kuwa kingwendu kama mwalugali alivyosema.