MASIORA
JF-Expert Member
- Mar 28, 2013
- 660
- 271
hiyo kodi unayozungumzia ni bidhaa zipi na aina gani ya kodi? Tunapozungumzia kodi kuna:
1. Ushuru wa forodha
2. Kodi ya ongezeko la thamani (vat)
nk.
Katika sheria ya kodi ya ongezeko la thamani (vat) ya mwaka 1997, kuna mambo ambayo kwa kiingereza wanasema:
1. Taxable supplies - which includes standard rate (18%), zero rated and special relief (which is either 100% or 45%)
2. Exempt supplies
3. Out of scope.
Ritz nakuomba umtafute mtu yoyote aliye mtaalamu wa masuala ya kodi akushauri na hatimaye utakapokuwa umeelewa ni aina gani ya kodi inayokwepwa basi utuletee hayo matokeo humu. Kwa jinsi ninavyoona kwa mbali ulicholeta hapa kinaweza kuwa utaratibu wako wa kawaida wa kuhangaika na maisha ya dr. Slaa hata kwa gharama ya kusema uwongo.
Kama taasisi inayotaka kujenga hospitali itaomba msamaha wa kodi basi itaomba kwa mujibu wa sheria kodi ya nchi hii. Na kama anakwepa basi taasisi hiyo na wahusika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya nchi. Wewe ulichokileta bado hakijakamilika na hapo hapo unadai ukwepaji wa kodi. Hapo hapo unazungumzia uagizaji wa vifaa na vifaa vyenyewe hujabitaja ili tujue kama kweli vinalipiwa kodi na kodi hiyo ni ya aina gani.
naaaaaaaaam