Dr Slaa na mchumba wake watakiwa kufika mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa na mchumba wake watakiwa kufika mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mwanajamii, Feb 22, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hakimu aagiza Slaa, mchumba wake wafike mahakamani
  Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha; Tarehe: 21st February 2012
  [TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"]Habari Zaidi:[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Marquee"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Marquee"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  HAKIMU wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Charles Magesa ameagiza Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa na mchumba wake Josephine, kufika mahakamani hapo leo asubuhi kabla ya kuanza kwa kesi dhidi yao na kinyume na hapo atatoa hati ya kuwakamata.

  Magesa alitoa amri hiyo jana baada ya washitakiwa hao na mwenzao, Aquiline Chuwa kutofika mahakamani hapo na wakili wao, Albert Msando alipoulizwa akawatetea kuwa wamechanganya siku ya usikilizwaji wa kesi ya kufanya maandamano yasiyo halali na kesi ya kutoa matamshi ya uchochezi.

  Jana katika kesi hiyo, usikilizwaji wa awali ulikuwa uanze kwa washitakiwa 19 akiwemo Dk. Slaa kusomewa mashitaka mapya 13 yanayowakabili.

  Awali wakili wa Serikali, Edwin Kakolaki aliiomba Mahakama kutoa hati ya kuwakamata washitakiwa hao na kuwaleta mahakamani kwa nguvu kutokana na kudharau Mahakama.

  “Si kweli kuwa wamechanganya tarehe ya kesi kutokana na wingi wa kesi walizonazo kwa kuwa wanaowadhamini wangepaswa kufanya nao mawasiliano pamoja na wakili wao.

  “Naomba mahakama itoe hati ya kuwakamata na kuwaleta hapa kwa nguvu ili wasipate mkanganyiko wa kuchanganya tarehe,” aliomba Wakili Kakolaki.

  Kakolaki pia aliiambia Mahakama kuwa washitakiwa hao wanadharau mahakama hiyo kwa sababu Januari 17 mwaka huu waliambiwa wakumbushane ili wasikose mahakamani siku hiyo kwa sababu ndiyo usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo utafanyika, lakini hawakufanya hivyo.

  “Mimi nasema hawajasahau wamefanya makusudi, kwa sababu wangeweza kutumia njia ya kuandika katika kumbukumbu zao ili wasisahau tarehe za kesi zao, pamoja na kudai wana kesi nyingi zinazowachanganya lakini hiyo siyo sababu ya msingi,” alisema Kakolaki.

  Baada ya wakili Kakolaki kutoa ombi hilo, aliomba Mahakama iendelee na usikilizwaji wa kesi hiyo kama walivyokubaliana na washitakiwa ambao hawakuwepo, wasomewe mashitaka yao siku watakapofika leo.

  Kakolaki baada ya kutoa ombi hilo, Hakimu Magesa alimwamuru aendelee na usomaji wa mashitaka ya awali.

  Wakili Kakolaki alidai washitakiwa wote 19 wanashtakiwa katika kosa la kwanza, kula njama Januari 3 na 5 mwaka jana katika Manispaa ya Arusha ya kutenda kosa la kufanya fujo.

  Katika kosa la pili linalowahusu washitakiwa 18, wameshitakiwa kula njama kufanya mkusanyiko usio halali na kufanya vurugu baada ya katazo halali.

  Katika shitaka linawahusu Dk. Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, wanashitakiwa kwa kutoa matamshi yenye lengo la kuleta uchochezi.

  Pamoja na mashitaka mengine, pia walishitakiwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali kwa ajili ya lengo moja la kukataa kutii amri ya OCD iliyowataka watawanyike.
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  dah! Dr. Slaa na 62 yrs zake bado anamchumba? Kumbe sijachelewa!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hakimu aagiza Slaa, mchumba wake wafike mahakamani
  Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha; Tarehe: 21st February 2012

  Huyo Veronica ndio nani?...Inaonekana kama vile hii habari ina malengo maalum!...huh!
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hao si wana kesi ya Josephine kudai talaka kwa mumewe? mnhhhh, kazi ipo.
   
 5. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  huh..hivi kumbe inawezekana?yasser arafat alipooa akiwa na miaka 75 nilishangaa ila slaa amenifumbua macho na vile mademu wanazengua zama hizi i gonna wait till i hit 60.then i find maself a fiancee of 20.hongera dr for your inspiration.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hakuna aliye juu ya sheria ingawa wengi hapa tutaijadili kisiasa.
   
 7. only83

  only83 JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hii habari imekaa kimbeambea...hawa waandishi wa habari makanjanja bwana.
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Umbea ujaacha tu wewe mwanaume?
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Jamani inabidi Dr. afanye kweli haya mambo ya kusema mchumba wa Dr. Slaa (Rais mtarajiwa!) yanatia ukakasi. Si amuoe tu yaishe. Kama kanisani hawataki aende kwa DC.
   
 10. only83

  only83 JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Unaumwa sana wewe,hivi wewe na hiyo sura yako kama kibabu cha miaka 100 utaweza fananisha na Dr Slaa?
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  sikuamini niliposikia huyu mama Josephine anaomba talaka kwa mume wa zamani. kwa nini asingetangulia kuomba talaka kabla hajaanza mahusiano ya nje?
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  Ndoa ya kanisa haivunjwi kirahisi rahisi hivyo labda akimbilie mahakamani kuivunja nasikia kanisani walikataa.
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  suala hili si umbea liko wazi mahakamani.
   
 14. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Hiyo status ni balaa!Mke halali wa Mahimbo at the same time Mchumba wa Slaa.
   
 15. m

  msalisi Member

  #15
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  porojo tupu
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mungu kaumba wanaume kwa mfano wa pekee kumbe katika umri huo bado machine ni bomba kiasi cha kumtosheleza binti mdogo.
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilikuwa na maana kwamba afunge ndoa kanisani au kama hawataki aende kwa DC. Kumbe sasa hata ndoa ya mwanzo ya mchumba wake bado haijavunjika! Basi kuna kazi hapa. Inabidi kwanza ndoa ivunjwe ndio kuwe na mchakato wa kufunga ndoa. Mambo yananichanganya haya: Kama ndoa haijavunjwa inakuwaje awe mchumba wa mtu? Kwa mila za kwetu damu ingeishamwagika kitaaaambo.
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kazaa naye mtoto hivi majuzi, ni ajabu ya tatu kabla hata mahakama haijatoa taraka. Mahimbo anaweza kufungua kesi nyingine ya kuzaa na mke wake.
   
 19. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  acheni kuchanganya kila kitu na siasa za kuchafuana,mwandishi hapo ana kosa gani?yeye kafanya kazi yake yani kwa kuwa ni slaa basi hata kama kuna stori mwandishi asiandike?
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Najua roho inakuuma sana kwani alikuzibia kwa DR slaa hahahahahah nenda kwa Sugu hajaoa......
   
Loading...