Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

TANGAZO.
kwa wale mnaolala sasa kesho tukutane hapa kwenye huu uzi muhimu sana.
wengine tujumuike pamoja katika mkesha hapa katika uzi huu japo salaly amekimbia najua atarudi tu kwahiyo tulizeni bolu(mh hivi ni bolu ama ball),i mean mtulize mshono cause libereke liko on full time.
katibu wa uzi

Haya katibu wa uzi lakini hii ligi inayoendelea hapa ni hatari kwa afya naomba katibu uisimamie mi siiwezi.
 
Babu anajidai Eti kageuka Sumaku (magnet)ya kunasa mawasiliano. Kila mtu anajua kuwa unaweza kuanzisha Email mbili tofauti kwa kutumia majina unayotaka then ukarusha email ukaenda kutangaza umenasa mawasiliano.mfano fmbowe@yahoo.com na nyingine drslaa@Gmail.com then ukarusha any sms kutoka one account kwenda nyingine ukajitokeza kujifanya Sumaku ya kudaka mawasiliano.

Hivi waliotuhumiwa kutumiana emails wamekanusha ama..? Nauliza tu kutaka kuhakikisha maneno ya Dr. Slaa na ya kwako..
 
Hawezi hata kujaribu, kama anaweza aje JF Palace, jukwaa la Kiingereza kitupu, tunachapa kule kimombo tu, vijana wa shule za santa Mlupo inafaa mpitie kule mpate mazoezi, umkumbushe na huyo anaejiita sandy candy aje, maana huwa anahororoja hapa bila mpango, aje kule nimpe za uso kwa hiyo hiyo lugha nisiyoielewa na nimpe darsa kuhusu hilo jina analojiita (inasikitisha kijana kujiita sandy candy) pengine hajuwi hata maana yake.

Link hii hapa: Jamii Forums Palace

We ajuza ni janga la taifa
 
Hana ishu. Anaichambua imekuwa mchele?

Slaa n khanisi sasa Rais kuitwa Dear. ndo nin?aahh me nlvokuwa naomba KAZ nandka dear sir/madam pia dear n mpenz mpenz baba mpz mama dear president eehhh we kweli ukawe padri ......sasa muhongo kawekwa kiporo si anachunguzwa upatkane ushhhidi wa kutosha au
 
Hivi waliotuhumiwa kutumiana emails wamekanusha ama..? Nauliza tu kutaka kuhakikisha maneno ya Dr. Slaa na ya kwako..

Hivi ukitaka kila anachongea mpumbavu wewe ukijibu utajibu mangapi? Dr slaa mpumbvu yan ukase me eti Rais kaitwa Dear aahh kwan dear kitu gan na yeye nan katka nchi hii atayeweza kunasa mawasiliano ya rais?atafute Wa kumdanganya otherwise atafute cha kusema sio upuuz Wa email na hawana mamlaka ya kumtaka rais Ajiuzulu n wapumbavu namshangaa sana huyu jamaa yenu kikwete aliposhinda alsema amtambui kkmm rais baadae wanamuomba waende ikulu hivi uyu slaa mzma au kauli zenu aziwez kumfanya rais ajiuzulu amjamchagua nyie mapunjuuu
 
Soma aliyosema CAG mstafu: Raia Mwema: Turudi kwenye suala la Escrow. Hivi ile ripoti uliiona kabla haijatoka?

Ludovick Utouh: Ni kweli kwamba mimi ndiye niliyeanza na suala hilo lakini sikulimaliza kwa vile nilikuwa nimestaafu tayari. Sitaweza kuwa msemaji mzuri kuhusu ripoti hiyo.

Raia Mwema: Kuna kitu kimoja kwenye ile ripoti ambacho kimechanganya watu wengi ni pale CAG anaposema fedha zilizokuwepo katika akaunti ya Escrow zinaweza kuwa za umma au zisiwe za umma. Kwanini ripoti haikwenda moja kwa moja kusema zile ni fedha za umma au si za umma?

Ludovick Utouh: Hilo swali lake lingeweza kujibiwa vizuri zsaidi na aliyekuwa Kaimu CAG ambaye ndiye aliyesaini ile ripoti. Yeye ndiye anayejua zaidi. Lakini naomba kusema yafuatayo.

Kama ulifuatilia mjadala ule wa bungeni, kitu cha kwanza ambacho kilisemwa na kipo kweli ni suala la kodi. Ndani ya fedha zilizokuwapo kwenye akaunti ya Escrow kulikuwa na kodi. Kodi ni mali ya umma. Hivyo kwenye eneo hilo la kodi, fedha za umma zipo.

Jambo la pili lipo kwenye historia ya kuanzishwa kwa akaunti hiyo. IPTL na Tanesco walikuwa na mzozo kuhusu malipo ya capacity charge. Mgogoro ulikuwa mkubwa na wakaamua kuweka fedha za malipo hayo kwenye akaunti ya Escrow huku wakisubiri shauri lao kutoka katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro.

Sasa, nizungumze kama mfano tu, kwa kufikiria kwamba IPTL walikuwa wanaichaji Tanesco shilingi 30 kwa siku. Tanesco wakaona kwamba wanalaliwa kwa gharama hizo. Wanalipa zaidi ya wanavyotakiwa kulipa.

Wakaenda mahakamani kushitaki. Uamuzi uliotoka ni kwamba, ni kweli Tanesco wamebambikiwa hizo gharama. Inabidi gharama za capacity charge zikokotolewe upya. Sasa ofisi ya CAG haina mamlaka ya kufanya ukokotoaji huo.

Kwa hiyo, kama ukokotoaji ungefanyika, labda tuseme IPTL ingetakiwa kutoza shilingi 20 kwa siku, maana yake ile tofauti ya shilingi 30 inayotozwa na shilingi 20 inayotakiwa kutozwa, yaani shilingi 10, ingekuwa ya Tanesco.

Hii maana yake ni kwamba, katika kila shilingi 30 iliyokuwepo katika Escrow, ukiondoa zile za kodi, shilingi 20 zilikuwa za IPTL kwa sababu ya umeme wake iliyouza na shilingi kumi zilikuwa za Tanesco ambayo ni taasisi ya umma.

Ndiyo maana, nafikiri, Kaimu CAG katika ripoti yake akasema kwamba ndani ya akaunti ile kulikuwa na fedha za umma na pia kulikuwa na fedha zisizo za umma.

Raia Mwema: Kama leo wewe ungekuwa CAG na Mheshimiwa Rais akakuuliza achukue hatua gani kwa wahusika wa Escrow wewe ungemshauri nini?

Ludovick Utouh: Unajua jambo ambalo napenda watu wajue hapa ni kwamba ripoti ya CAG haichunguzi jinai. Sisi kazi yetu na kukagua mahesabu na kutoa maoni yetu kuhusu tulichokiona.

Ndiyo maana, mwaka 2010, tulifanya marekebisho kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Umma kifungu cha 27 ambapo CAG aliruhusiwa kupeleka taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya uchunguzi wa jinai kama zipo kwenye ukaguzi uliofanyika.

Kama Rais angenitaka ushauri, ningemwambia Mheshimiwa Rais naomba utumie vyombo vyako. Atumie Takukuru, DCI na vyombo vyake vingine kuchunguza kujua nini hasa kilifanyika nyuma ya pazia. Hii si kazi ya CAG. No, Thank You.

Sasa akipata taarifa zote, ya CAG, Takukuru na DCI, hapo anaweza kuwa amejipa taarifa za kutosha kuhusu suala hili. Kama ataona kuna jinai yoyote, basi achukue hatua ya kuwasimamisha kazi wahusika na kuwapeleka mahakamani ili mkondo wa kisheria uchukue nafasi yake.

Raia Mwema: Kuna maneno yameenea kwamba maazimio ya Bunge kuhusu suala la Escrow yalikuwa yametawaliwa na mihemuko ya kisiasa zaidi kuhusu ukweli. Wewe una maoni gani kuhusu mawazo hayo?

Ludovick Utouh: Kwanza niseme kwamba ukiangalia tulikotoka miaka minane iliyopita na sasa kwenye eneo la usimamizi wa mapato na matumizi ya umma utaona kwamba tumepiga hatua kubwa. Bado hatujafika mwisho wa safari lakini tumesogea.

La pili niseme kwamba linapokuja suala la usimamizi wa mapato na matumizi ya mali na rasilimali za umma, mambo ya itikadi ya kisiasa yanatakiwa kuwekwa pembeni.

Maendeleo tuliyoyapata katika maeneo ya mapato na matumizi yanapaswa kuchagizwa kwa kuongeza zaidi wigo wa mapato ambayo yanaweza kukusanywa.

Naipongeza sana Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kazi kubwa ya kukusanya mapato ambayo wameifanya. Ukiangalia ni kiasi gani ukusanyaji wa mapato umeongezeka tangu enzi ya Rais Benjamin Mkapa hadi sasa utaona ni kiwango kikubwa sana.

Lakini bado watu wengi hawalipi kodi inayotakiwa. Hapa Dar es Salaam kuna watu wanauza maziwa au mayai na wanapata fedha ambazo ni mara tano ya mishahara wanayopata. Sasa wanakatwa kodi kwenye mishahara yao lakini hawakatwi kodi yoyote kwenye mapato haya ya nje. Ziko biashara nyingi sana ambazo hazilipiwi kodi na zingeweza kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi kikubwa.

Ningetoa ushauri kwa TRA kuhakikisha kwamba wanatumia vema fursa hii ya kuwapo kwa vitambulisho vya Taifa vya NIDA ili kuweza kubaini watu walipo na kuwatoza kodi stahiki kwenye shughuli zao.

Kuna pia umuhimu mkubwa wa kuziba mianya iliyopo kwenye mfumo wetu wa utawala ili kuhakikisha Taifa linakingwa na matukio ya kifisadi kama yalivyokuwa kwenye EPA na hii Escrow. Ni lazima tufanye jitihada kuziba hiyo mianya ya ufisadi kwenye mfumo wetu.
 
Msikilize Dr.Slaa live ITV akiongelea sakata la Escrow na hotuba ya Kiwete.

Dr.Slaa, anamlaumu raisi Kikwete kwa kukosa uzalendo kwa jinsi anavyoshughulikia sakata hili la Escrow na kumlaumu kwa kuvunja katiba.

Dr.Slaa amlaumu Kikwete kwa double standard.Yaani kumuondoa Tibaijuka kazini na kumuweka kiporo Muhongo.Pia, amehoji utaratibu wa kumuweka mwanasiasa kiporo.

Dr.Slaa anasema Kikwete anapuuza bunge na kwamba hivi sasa ni serikali inayolisimamia bunge na si bunge linaisimamia serikali.

Dr.Slaa anasema Seth anastahili kuwa amekamatwa kwa kugushi nyaraka na pia kutolipa kodi na kwamba raisi anafumbia macho.

Dr.Slaa anasema singasinga huyu ana uhusiano na Ikulu kwa muda mrefu na ndio maana hachukuliwi hatua.

Pia,Dr.Slaa ameishaangaa polisi kupewa msaada wa fedha na singa singa.

Dr.Slaa pia anashangaa raisi kuwasiliana kwa email na mtuhumiwa mmoja na huku mtuhumiwa huyo akimwita raisi "dear".

Dr.Slaa anungana na maaskofu kutaka uwajibikaji wa watuhumiwa wa sakata hili na pia ameungana na wanaosema raisi anapaswa kujiuzulu(Deus Kibamba ni mmoja wa watu waliotoa kauli kuwa, kwa sakata hili,hata raisi anapaswa kuondoka madarakani-Tanzania Daima la leo).

Dr.Slaa amemalizia kwa kusema hawana chuki binafsi na Muhongo wa raisi.

Sawa Dr.tunakuamini hao wanaokuponda humu jf najua wanaundugu na hao mafisadi tena washindwe na walegee 2015 nguvu ya umma inakuweka ikulu.
 
Hawezi hata kujaribu, kama anaweza aje JF Palace, jukwaa la Kiingereza kitupu, tunachapa kule kimombo tu, vijana wa shule za santa Mlupo inafaa mpitie kule mpate mazoezi, umkumbushe na huyo anaejiita sandy candy aje, magna huwa anahororoja hapa bila mpango, aje kule nimpe za uso kwa hiyo hiyo lugha nisiyoielewa na nimpe darsa kuhusu hilo jina analojiita (inasikitisha kijana kujiita sandy candy) pengine hajuwi hata maana yake.

Link hii hapa: Jamii Forums Palace

Faiza foxy shikamoo bibi, unataka niende jukwaa la English kujibizana na mataahira wanaoongea broken English? Mimi na English za form 2 waliofeli wapi na wapi? Nilishaenda kule nikaona watu wanavyoongea vitu vya ajabu....hawajui singular and prural, hawajui tenses present, future ect.ni aibu tupu.siwezi kubishana na wapumbavu nami nitakuwa mpumbavu bure! Sijui hizo English niza wapi labda kariakoo au manzese
 
Faiza foxy shikamoo bibi, unataka niende jukwaa la English kujibizana na mataahira wanaoongea broken English? Mimi na English za form 2 waliofeli wapi na wapi? Nilishaenda kule nikaona watu wanavyoongea vitu vya ajabu....hawajui singular and prural, hawajui tenses present, future ect.ni aibu tupu.siwezi kubishana na wapumbavu nami nitakuwa mpumbavu bure! Sijui hizo English niza wapi labda kariakoo au manzese

Umegwaya candy! candy? pole sana.
 
mkuu huyo mwana mama umsamehe bure, huyu muda wote kazi yake ni kutukana tu wapinzani na sio kujibu hoja. Pia hupenda kutumia dini ya mwenyezi mungu kama ngao ili kutetea mapungufu ya ccm/jk. Hana jipya zaidi ya kujifanya yeye anaijua dini kuliko wengine. Sijaona mwanamke wa kiislamu mwenye mdomo mchafu kama huyu mama wallahi.

Jana alikubaliana na mimi si vizuri kutukana lakini alijitetea anafanya hivyo kulipiza wapinzani wa CCM/JK ambao humtukana JK, CCM na viongozi wa CCM au serikali. Nafikiri taratibu ameanza kuelewa umuhimu wa kutunza amani iliyopo Tanzania. Fedha au madaraka ni vitu vya kupita tu; havina maana kama nchi haina amani.
 
Umegwaya candy! candy? pole sana.

Faiza foxy una maana gani kusema hivyo?
Pia niambiye maana ya jina langu!
Pia ukiacha kutukana watu humu tutakuwa marafiki

DR SLAA NI INTERNATIONAL FIGURE ANA HESHIMA ZAKE NA AMESOMA KULIKO KIKWETE.UDOKTA WAKE SIO WA KICHINA KAMA WA KIKWETE. PIA ANA UWEZO WA KUONGEA FLUENT ENGLISH SIO KAMA KIKWETE HAJUI KUONGEA ENGLISH. ..BILA KUKUSAHAU WEWE...switch your self!
 
Faiza foxy una maana gani kusema hivyo?
Pia niambiye maana ya jina langu!
Pia ukiacha kutukana watu humu tutakuwa marafiki

DR SLAA NI INTERNATIONAL FIGURE ANA HESHIMA ZAKE NA AMESOMA KULIKO KIKWETE.UDOKTA WAKE SIO WA KICHINA KAMA WA KIKWETE. PIA ANA UWEZO WA KUONGEA FLUENT ENGLISH SIO KAMA KIKWETE HAJUI KUONGEA ENGLISH. ..BILA KUKUSAHAU WEWE...switch your self!

Pipi mchanga.
 
Faiza foxy una maana gani kusema hivyo?
Pia niambiye maana ya jina langu!
Pia ukiacha kutukana watu humu tutakuwa marafiki

DR SLAA NI INTERNATIONAL FIGURE ANA HESHIMA ZAKE NA AMESOMA KULIKO KIKWETE.UDOKTA WAKE SIO WA KICHINA KAMA WA KIKWETE. PIA ANA UWEZO WA KUONGEA FLUENT ENGLISH SIO KAMA KIKWETE HAJUI KUONGEA ENGLISH. ..BILA KUKUSAHAU WEWE...switch your self!

Amesoma nini wewe? tuoneshe shahada yake ya kwanza alichukulia chuo gani na ipi?

Hapo sasa.
 
Hivi ukitaka kila anachongea mpumbavu wewe ukijibu utajibu mangapi? Dr slaa mpumbvu yan ukase me eti Rais kaitwa Dear aahh kwan dear kitu gan na yeye nan katka nchi hii atayeweza kunasa mawasiliano ya rais?atafute Wa kumdanganya otherwise atafute cha kusema sio upuuz Wa email na hawana mamlaka ya kumtaka rais Ajiuzulu n wapumbavu namshangaa sana huyu jamaa yenu kikwete aliposhinda alsema amtambui kkmm rais baadae wanamuomba waende ikulu hivi uyu slaa mzma au kauli zenu aziwez kumfanya rais ajiuzulu amjamchagua nyie mapunjuuu

Kwa kuzingatia protocol, Waziri achilia mbali Raisi, hawezi kuwa addressed vingine zaidi ya kuweka Mheshimiwa, unless unaongea naye kishikaji kwenye issues ambazo sio official. Nafikiri hii ndio point wanayosimamia hao walioona hizo correspondences.
 
Back
Top Bottom