Elections 2010 Dr. Slaa kumuwekea pingamizi Kikwete!

Hiyo nyekundu ni ungo mkubwa. Dr. Slaa hiyo sheria kaisomea wapi au sheria ya kanisa ndio inamfanya kubobea kitaaluma katika sheria?

Nawasiwasi kama Dr. Slaa hana washauri wa kweli. kwani habari ya mshahara kuongezeka sio ya leo na wala hajaanza baada ya kampeni. watu wamesha kula mishahara miwili mpya na kampeni hazina hata wiki sasa hapo si ukilaza jamani. Hao FOS au FOD wanamshauri nini kama ndio anatuletea hizi pumba hata kabla hajaanza kampeni.

Tatizo la jf hatujui umri wa mtu na elimu yake. Hili ndilo linachangia waropokaji kama wewe kupata jukwaa la kufukiza moshi! Sijakuelewa umeuliza unataka kujibiwa! Au umejijibu tayari? unahitaji kuwa na msimamo kama hujui kuwa kasoma sheria subiri sio unajifanya kuuliza na kujibu. Hatutaki mtu anayesaidia watu kufikiri kwa kuwapa uwanja mdogo tena ukiwaelekeza kwenye dini!
Kama unasema mishahara ilishaongezwa miezi miwili kwa nini haikutangazwa miezi hiyo miwili ya mwanzo? Badala yake anatangazia jukwaani kwenye kampeni? Ina maanisha alifanya siri ili iwe sera/ilani ya uchaguzi kipindi cha kuomba kura! Hii ni rusha au takrima!
 
Hivi nauliza: Kama kawaida Vyama vya Siasa vitatupilia mbali pingamizi hilo (maana mara nyingi sana sana pingamizi zinazokubaliwa ni zile za CCM dhidi ya vyama vya upinzani) Itakuwa ndiyo mwisho? Au kuna njia nyingine ya kwenda Mahakamani?
 
Hili la mishahara Dr Slaa angeliliacha kwa sasa. Hali ya WAFANYAKAZI wa Nchi ni mbaya. Kupinga nyongeza yoyote kwao hata kama sheria, taratibu na kanuni hazikufuatwa itamweka pabaya Dr Slaa. CCM wanajua sana kupindisha na kutoa tafsiri mbovu kwa kauli za wapinzani wao. Yeye Dr Slaa aseme atawafanyia nini Wafanyakazi wa nchi hii atakapokabidhiwa dola.
 
WC
Hata mimi mwanzoni niliona hilo suala CHADEMA wangeliacha kwa sasa. Lakini hoja aliyojenga Dr Slaa wakati akiongea na waandishi wa habari kama nilivyoiona kwenye Mlimani TV, naona ni vizuri kuifanyia kazi sasa. Kwa sababu kwanza ni ukiukaji mkubwa wa kanuni za fedha za serikali. Kwa sababu fedha za serikali ili zitumike ni lazima zipitishwe na bunge, sasa kama JK yeye anakuwa wa kwanza kuzipindisha huoni kama huo ndiyo msingi wa ufisadi. Pili CCM walisema kuwa Rais wao hajawahi kukataa kura za wafanyakazi bali alichosema ni kwamba mshahara ulioombwa na wafanyakazi haulipiki. Sasa kama ni hivyo kwa nini walipe sasa hivi na siyo wakati ule ulipoombwa na wafanyakazi? Hapo CHADEMA (nadhani wanafanya mikakati ya kisiasa) ni kutaka kuwaonyesha wafanyakazi kwamba CCM haiwatakii mema na kwamba hata wakiichagua inaweza kuja kuwageuka.
 
Alisaini sheria hiyo kwa mbwembwe na kuahidi kuwa atahakikisha inafuatwa mbele ya wageni mbali mbali wakiwepo Mabalozi kutoka nje. Sasa kaivunja yeye mwenyewe pengine kwa kutokujua(jambo ambalo sio kinga kisheria) au kwa makusudi akijua atafanywa nini wakati yeye yuko madarakani. Kupitia Msajili wa vyama au Tume ya uchaguzi hili litakuwa jambo gumu sana kwao kulitolea maamuzi kwa sababu ambazo wote tunazifahamu.
Mimi nadhani kwa vile ubavu wa kupambana nae kupitia vyombo hivyo utakuwa na utata, Balozi za nje ambazo zilishirikishwa na kuelezwa umuhimu wa sheria hiyo pale zilipoalikwa kwenye uzinduzi wa mbwembwe nazo ziwe alerted na nini kinaendelea iwapo haki haitatendeka, maana hao wana nguvu kwa sasa kwa vile ndio tunao watembezea BAKULI kila siku na hata uchaguzi huu wameuchangia kwa kiwango cha juu.
 
Hiyo nyekundu ni ungo mkubwa. Dr. Slaa hiyo sheria kaisomea wapi au sheria ya kanisa ndio inamfanya kubobea kitaaluma katika sheria?

Nawasiwasi kama Dr. Slaa hana washauri wa kweli. kwani habari ya mshahara kuongezeka sio ya leo na wala hajaanza baada ya kampeni. watu wamesha kula mishahara miwili mpya na kampeni hazina hata wiki sasa hapo si ukilaza jamani. Hao FOS au FOD wanamshauri nini kama ndio anatuletea hizi pumba hata kabla hajaanza kampeni.

Hiyo nyekundu nakuelewesha kuwa, Hao mapadre wanasomea mambo mengi sana na ndiyo maana kuna Madaktari Bingwa wengi sana Masista na mapadre na hata nyanja zingine nyingi tu. Tambua kuwa kuna vyuo, mashule, na vitengo mbalimbali katika kanisa na pia tambua kuwa viongozi wengi wa mwanzo wa nchi hii wenye taaluma maalum wamesoma huko, ila sheria za kuwa mapadre hazikuwaruhusu na wakaja huku katika siasa.
Kanisa ndo lilianza mambo ya upendo, umoja, amani na ndo sera zake ambazo Tz bado inajivunia.
Katiaka Bold; Jamaa kainua kwanza mishahara kimya kimya mara tu alipomsikia DR. wa kweli akinukuu ile hotuba na "wazee wa DAR" Mimi pia nishtuka kuona mshahara umeongezeka ghafla. Hilo ni dili tu na ni rushwa kwa mtu mkubwa kama yeye. Siku ile alidiriki hata kuwatukana wafanyakazi kupitia mwakilishi wetu, leo anakataa eti atatufikiria wapi na wapi.
Dr. slaa na haki ya kupinga. JK katuhonga laivu ni kwa vile tu sisi ni watanzania ingekuwa kwa wenzetu yaani kashatoka saa nyingi!!!
SEMA TU CCM NDO KASHIKA MPINI NA ATAFANYA LOLOTE KUIGEUZA ISHU
kAMA MUONGO KUWA NI WAMAFIA BASI SUBIRI UONE!
 
Hili la mishahara Dr Slaa angeliliacha kwa sasa. Hali ya WAFANYAKAZI wa Nchi ni mbaya. Kupinga nyongeza yoyote kwao hata kama sheria, taratibu na kanuni hazikufuatwa itamweka pabaya Dr Slaa. CCM wanajua sana kupindisha na kutoa tafsiri mbovu kwa kauli za wapinzani wao. Yeye Dr Slaa aseme atawafanyia nini Wafanyakazi wa nchi hii atakapokabidhiwa dola.
No Dr hajapinga ongezeko la mishahara na hata wafanyakazi wanalifahamu hilo na kila siku anazungumzia tofauti ya kipato kati ya juu na chini. Anachosema ni kuwa kwa nini uwaambie huna fedha za kuwapa nyongeza hata kama kura hawatakupa halafu ukiona wamechukizwa na jambo hilo wakati wa kampeni unaongeza nje ya utaratibu wa matumizi ya fedha za umma?
Acha awe wazi,wafanyakazi wa sasa sio Mabwege tena watamwelewa Dr. Slaa na kufahamu kuwa nyongeza hiyo ni kebehi kwao na wameuza utu wao uliodhalilishwa pale Diamond. Sheria ifuate mkondo wake pingamizi lisonge mbele.
 
Miheshimiwa ilisema kuwa hata wagome miaka minane hatapandisha mishahara, iweje sasa akapandisha hata bila ya ridhaa ya bunge. Hii si rushwa kwa wafanyakazi? Ili wakihoji waambiwe wamesikilizwa?? Safi saaana CHADEMA, wasiwasi wangu ni kuwa je Tendwa / Makame wana guts za kumwondoa mtu aliyewaweka madarakani??
 
Padre alitumia suala la TUCTA na wafanyakazi kuwa ni chambo ya kujinasia kura. lakini hakujua kuwa JK ana utaratibu wa kuongeza mishahara kwa watumishi kwa utaratibu maalum.Sasa sijui atatoka vipi?

tena, Hiyo nyekundu ni uwongo wa kupakwa,
JK hana utaratibu huo yeye kama yeye. hii ni tangu enzi za TANU, na utaratibu wake ingekuwa kuwaongezea maswahaba wake siyo eti watu ambao hata haawajui.
Ukweli wake ni pale kwa wale wazee aliowaita na kusema kiwango cha TUCTA hikilipiki na mwakilishi wao ni mnafiki akinukuu barua za kughushi zenye mda wa owongo.
Slaa ana uchungu wa kweli na ndo maana alipigia kelele hata mishahara nanayoipoke yeye mwenyewe Bungeni!! Ungekuwa wewe si ungekula ganzi kama walivyofanya wapinzani wengine!
Slaa ametumia ile ya TUCTa sahihi kabisa, maana kwa sasa watanzania wenyewe tu kuna ubaguzi mkubwa sana katika mishahara na hii imeanza kwa huyuhuyu JK. Leo mtu anapoke Tsh 103,000/= wakati kuna mtanzania mwingine anapokea milioni 10. je huyu ni binadamu kama huyo mwingine???
Nyumba cheki ile ya gavana halafu geukia kwa zile za polisi ( walinzi wetu wapendwa) utachekka uvunjike. Bilion 3 kwa silingi laki 3 ( kama Komedi vile>
Huo ndo uongozi wa huyu jamaa uliovusha bei za vitu kwa asilimia 200 na zaidi.
Be real great thinker!
 
Serikali ilikuwa haina uwezo pale alipowafokea mbayuwayu wa kupandisha mishahara; ila sasa serikali imepata uwezo wa kufanya hivyo...
 
No Dr hajapinga ongezeko la mishahara na hata wafanyakazi wanalifahamu hilo na kila siku anazungumzia tofauti ya kipato kati ya juu na chini. Anachosema ni kuwa kwa nini uwaambie huna fedha za kuwapa nyongeza hata kama kura hawatakupa halafu ukiona wamechukizwa na jambo hilo wakati wa kampeni unaongeza nje ya utaratibu wa matumizi ya fedha za umma?
Acha awe wazi,wafanyakazi wa sasa sio Mabwege tena watamwelewa Dr. Slaa na kufahamu kuwa nyongeza hiyo ni kebehi kwao na wameuza utu wao uliodhalilishwa pale Diamond. Sheria ifuate mkondo wake pingamizi lisonge mbele.

Wafanyakazi wa Tanzania hawako hivyo unavyowafikiria. Hawajui kugoma. Ni watiifu sana. Wengi wao wanaridhika sana anapopewa nafasi inayomwezesha kufanya ubadhirifu. Hawatamwelewa Dr Slaa hasa katika kipindi hiki ambacho CCM inaweza kucheza rafu yoyote ile ikiwemo hiyo nyongeza kinyemela ya mishahara. CCM wanajua marefa wote ni wao. NEC, RPP na vyombo vya DOLA.
 
Hivi wanao mpinga slaa ni wasaliti? Mbona wanaonekana kama watu wa ajabu...! Kulikoni hakuna uhuru wala demokrasia!?

na wao ndoyo maoni yao. Yawezekana nio wale wanaotegemea kuwa miongoni mwa wakuu wa ile mikoa iliyoongezwa. Ili kukuza matumizi ya serikali na kuongeza mfumuko wa bei
 
JK ni sawa na the late ODUAR wa Nigeria, hakuna muda R.I.P.Dr kaona wafanyakazi wameongezwa mishahara siku chache kabla ya kampeni ndio maana anataka kumuwekea pingamizi JK pia namuongezea amuwekee pingamizi ili kulinda afya yake asije akatutia hasara ya kuendesha uchaguzi mdogo hapo baadae.
 
Hiyo nyekundu ni ungo mkubwa. Dr. Slaa hiyo sheria kaisomea wapi au sheria ya kanisa ndio inamfanya kubobea kitaaluma katika sheria?

Nawasiwasi kama Dr. Slaa hana washauri wa kweli. kwani habari ya mshahara kuongezeka sio ya leo na wala hajaanza baada ya kampeni. watu wamesha kula mishahara miwili mpya na kampeni hazina hata wiki sasa hapo si ukilaza jamani. Hao FOS au FOD wanamshauri nini kama ndio anatuletea hizi pumba hata kabla hajaanza kampeni.
Amekurupuka huyo na washauri wake wako kisiasa zaidi badala ya kutafuta ukweli.kura hazitafutwi hivyo .
 
Wafanyakazi wa Tanzania hawako hivyo unavyowafikiria. Hawajui kugoma. Ni watiifu sana. Wengi wao wanaridhika sana anapopewa nafasi inayomwezesha kufanya ubadhirifu. Hawatamwelewa Dr Slaa hasa katika kipindi hiki ambacho CCM inaweza kucheza rafu yoyote ile ikiwemo hiyo nyongeza kinyemela ya mishahara. CCM wanajua marefa wote ni wao. NEC, RPP na vyombo vya DOLA.
Mkuu hilo (red) ni kweli, hawajui kugoma na ni watiifu sana. Ila sasa hivi wamekeisha elewa kuwa kile chumba cha kupigia kura uyafanyayo mule ni siri yako. Na wao wana siri yao moyoni. Wamechoka,wamefedheheshwa na kupuuzwa sana na utawala uliopita na sasa ndio wakati wao wa kutumia silaha waliyo nayo, KURA. Kama huliamini hilo mkuu ni bahati mbaya. Hakuna watumishi walikuwa wagumu kuelewa kuwa wanatumiwa kama walimu,lakini hebu fanya utafiti kidogo uone misimamo ya walimu sasa hivi utaona mabadiliko ambayo hata CCM wenyewe wameshashtukia.
 
Amekurupuka huyo na washauri wake wako kisiasa zaidi badala ya kutafuta ukweli.kura hazitafutwi hivyo .
Luiza naona una michango 11 tu uliochangia kwa mwezi huu wa nane hapa JF na kama michango 10 iliyopita inafanana na hivi utakimbia hapa JF muda si mrefu maana hapa ni pa watu vichwa tu. Huwa hoja baki ukisoma hoja za wenzio.
 
JK ni sawa na the late ODUAR wa Nigeria, hakuna muda R.I.P.Dr kaona wafanyakazi wameongezwa mishahara siku chache kabla ya kampeni ndio maana anataka kumuwekea pingamizi JK pia namuongezea amuwekee pingamizi ili kulinda afya yake asije akatutia hasara ya kuendesha uchaguzi mdogo hapo baadae.
Pingamizi ni la kitoto hilo. halijaenda shule.limekurupuka
 
Luiza naona una michango 11 tu uliochangia kwa mwezi huu wa nane hapa JF na kama michango 10 iliyopita inafanana na hivi utakimbia hapa JF muda si mrefu maana hapa ni pa watu vichwa tu. Huwa hoja baki ukisoma hoja za wenzio.
Hoja ikiwepo manake husomwa na kuchangiwa kulingana na maono ya mchangiaji. Usiogope tuko pamoja. si lazima tukubaliane katika unayoyawaza wewe.JF inakutana na vichwa mbalimbali.ni kwa hoja tu si kukimbizana.hasira ya nini?
 
CV ya Dr Slaa
EDUCATION
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993-1993
TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985-1985
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980-1981
St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977-1981 [Doctor of Canon Law (Latin: Juris Canonici Doctor or JCD)]
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974-1977
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972-1973
Itaga Seminary School A-Level Education 1970-1971
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966-1969
Karatu Primary School Primary Education 1962-1965
Daudi Primary School Primary Education 1961-1961
Kwermusl Primary School (Mbulu) Primary Education 1958-1960

Nikiangalia hapo sioni sehemu inapoonesha kasomea sheria zetu nje ya sheria ya kanisa (Canon Law)

Hebu weka na wewe CV yako tuione, hatukawii kuona form Six ulikuwa na Four la nguvu - lakini cha ajabu una ka advance diploma ka kuungaunga kanakokufanya uishi hapa mjini then unakurupukia C.V za wenyewe. Huna mamlaka kuhoji Elimu ya mtu bila hoja ya msingi.

Weka C.V ya katibu wako tuichambue. http://www.parliament.go.tz/bunge/mpcv.php?vpkey=1497#
mmhh
 
Back
Top Bottom