Dr. Slaa kumuwekea pingamizi Kikwete! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa kumuwekea pingamizi Kikwete!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mkulima mimi, Aug 26, 2010.

 1. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Wajameni nimechelewa kuona news. Dr. Anasema sheria ni nzuri kutunga na tuzifuate. Kipengele kipi jk anapingwa? Tujuzeni mliokuwepo kwani alikuwa na press conference
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Title iendane na habari, pls!
   
 3. k

  kiletsa New Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 1, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkubwa ametumia swala la kupandisha mishahara kama njia ya kuwaomba watanzania kura, ambayo according to Dr. Slaa, inapingana na sheria mpya ya uchaguzi!! Sijaipata hio sharia mpya yasemaje kiundani....
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,204
  Trophy Points: 280
  Leta source vinginevyo hatutaki majungu humu
   
 5. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  iweje labda!
   
 6. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  habari ITV, sasa hapo kuna habari gani ambayo mimi ninaweza kuipa source! Nilitaka mtu aliyeipata full alete data! Mkuu hapo juu kagusa sababu ni nyongeza ya mshahara kuwa imetumika kama mlungula!
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  na wewe unakuwa kama mlevi..majungu kivipi wakati kaongea kirumba mwanza kuwa atapandisha mishahara na kulipa deni la nyanza cooperative union..au hukusikia !! au ulisikia aliposema kulipia kodi ya 7m kuweka studio ya wasanii
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hivi wanao mpinga slaa ni wasaliti? Mbona wanaonekana kama watu wa ajabu...! Kulikoni hakuna uhuru wala demokrasia!?
   
 9. k

  kiletsa New Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 1, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani ingekua vema tukaendelea kumtambua kama Dr., sijui kama bado yeye ni Padri. Watever the case, sikubaliani na huyo Bull hata kidogo mana ktk kuongea ana mengi tufauti na wengine, ILA KAMA KAWAIDA YETU MANENO NA MATENDO NI TOFAUTI SANA!!, Labda kama una ushahidi wa utendaji wake, na sijui amekua tested wapi na how!!!
   
 10. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu uhuru na demokrasia viko mnadani. Tatizo watu wanahasira, wametest gari moja hivi kwa miaka 5, kumbe injini ya kichina, sasa spana mkononi
   
 11. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,204
  Trophy Points: 280
  Nimesema source Slaa aliposema anamwekea Kikwete pingamizi wewe unakurupuka mara mishahara mara nyanza, nakusamehe kwa sasa najua umevimbewa futari.
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  X-Paster,
  Hakuna aliyesema kumpinga Dr Slaa ni usaliti. Lakini Tanzania iko katika mapambano. CCM wanataka kuendeleza ufisadi na ulaji na Slaa anasimamia mabadiliko yatakayomweka Mtanzania katika usukani wa kuendesha nchi yao wenyewe.Chagua upande wako.
   
 13. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  sio kweli! Na hawapingwi kabisa ila wanafeli kwenye argument! Wanamchukia slaa bila sababu na kukuta wakimshambulia/kumhukumu slaa personal sasa ku-counter hilo wafuasi wa slaa humshambulia mshambuliaji kwa uzuri tu! Sababu watu wametoa hoja yeye kamshambulia mtu! Hoja vs mtu hapana mshindi hapo ndipo ulemsemo Kwamba when they change the rule of the game then we change the game! Mtu vs mtu lazima bingwa apatikane! Nadhani umemhurumia jamaa hapo juu! lakini hauoni humtendei haki kumtetea wakati kosa kafanya au ....?
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,204
  Trophy Points: 280
  Unatuonaje tunaomsupoti Slaa.......(.........)... na sisi tunakuona hivyo hivyo uliye mpenzi damu wa Kikwete.
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa inawezekana ningekuwekea thanx mara 5 mfululizo.
   
 16. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Niliwahi kusoma mahali kwamba Small Minds discuss People halafu zingne zina-discuss events na zingine bora au kubwa zinadiscuss IDEAS, sasa tuwahurumie hao wanaomwona Slaa ni Padre, ni Mkatoliki baadae watamwona sio handsome, watagundua anakunywa pombe watasema mlevi, watamwona amechukua mke watasema sijui nini, lakini hawaoni kingine, wanaweza hata wakasema akivaa nguo hazimpendezi, ni small minds hawa,

  tena mahali pengine waliandika usijibishane na mpungufu maana wote mtaonekana mapunguani, jamani!
   
 17. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Tafadhali tuweekeni hiyo sheria mpya ya uchaguzi tuione maana mara ya mwisho nilisikia inafanyiwa marekebisho baada ya kusainiwa na kikwete mwenyewe...

  Pia kama pingamizi hilo litafanikiwa ni kama vile msemo usema kila mwamba ngoma.. ngozi huvutia kwake.. kikwete alisaini hiyo sheria mpya ya uchaguzi kwa mbwembwe na akina Slaa wakataka ifanyiwe marekebisho ya haraka... sasa kama walifanikiwa basi watamnyonga kwa kamba zake mwenyewe kikwete kwa sheria hiyo aliyosaini kwa kuita kadamnasi...
   
 18. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mkuu X-PASTER,
  Nakutambua kama miongoni mwa "vichwa vya JF".Ninyi ni miongoni mwa watu mnaoifanya JF kuendelea kuwa na hadhi yake kama chombo mainstream cha habari ndani na nje ya Tanzania.However,and with all due respect,stance yako kuhusu Slaa inanitatizo kidogo.Naamini kabisa unafahamu kuwa nyingi ya hoja zinazoletwa against Dkt Slaa zinaelemea zaidi kwenye personal attacks kuliko kuangalia maslahi ya taifa.

  Hivi ni kweli kuwa X-PASTER of all the people hafahamu kwanini hoja zinazompinga Dkt Slaa tend to be unpopular?Unfortunately,katika hoja hii iliyopo (na ambayo imepelekea wewe kuhoji kwanini kila anayempinga Slaa anaonekana msaliti) mwenzetu mmoja ameamua kuweka kando busara zake na kumuita "Dkt Slaa padre vuvuzela".Sasa unless unaafikiana na stance hiyo,kauli ya mwenzetu huyo ni defarmatory.Sawa Slaa alikuwa padre lakini alishaacha,na hilo la kumuita vuvuzela ni utoto usiopaswa kuwa na nafasi mahala kama hapa.

  Kumbuka kwamba uhuru na demokrasia pasipo matumizi ya akili na busara ni sawa na uchizi.Wanaompinga Slaa wana haki ya kufanya hivyo lakini ni vema wakatumia lugha za kistaarabu,na kutumia nguvu za hoja badala ya hoja za nguvu au kashfa.Demokrasia haihalalishi kuwakwaza wengine (eg name calling) au kuchezea religious sentiments.

  By the way,unaweza kujiuliza kwanini wengi wetu tunamsapoti Slaa and only a pocketful seem to be opposing him?The answer,as they say,is in the question.
   
 19. f

  fyosa Member

  #19
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Washabiki wa JK na muambata wake Balali ooh sorry Bilali ni lazima mtoke kwenye utumwa wa kimawazo na kiakili, miaka mitano tumeishuhudia wote jinsi watu walivyopigika na mafisadi walivyo shine. Leo kama matahaira mnaambiwa mtaletewa maendeleo kwa hari zaidi,nguvu zaidi na kasi zaidi mnashangilia na kuamini utadhani JK ni mtume wa MUUMBA kumbe ni mtume wa Sheikh Yahya. Fungukeni macho nyie vipofu wa kujitakia amasivyo tutawafumbua kwa nguvu okt 31, watu gani nyie mliosoma lakini hamkuelimika. Bahati mbaya sana watetezi wengi wa JK hata kununua kandambili ni tatizo vocha wanazonunua ni za tsh 300 mkibisha waangalieni kwenye kampeni zake mtawaona wanavyotia huruma mashati ya kijani waliyonunuliwa yote oversize midomo imewakauka lakini jamaa akidondoka jukwaani na wao wanadondoka na kuzimia yaani mchawi aliye waroga ni kiboko. Lakini mwaka huu tunao tunajua hawataki ukombozi lakini tutawakomboa kilazima maana ni wenzetu,ndugu zetu mama nadada zetu kakana baba zetu hawa hatutokubali kuwaacha tutawaburuza tuwe nao hadi ktk siku ya ukombozi wa nchi hii okt 31
   
 20. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,204
  Trophy Points: 280
  Geofrey Nyang'oro na Lilian Mazula-Mwananchi

  SHERIA ni msumeno na sasa mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete atalazimika kufanya kazi ya ziada isimdhuru baada ya Chadema kumwekea pingamizi rais huyo wa serikali ya awamu ya nne.Kikwete alisaini Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa mbwembwe mapema mwaka huu akitaka itumike mwaka huu, lakini Chadema imeitumia sheria hiyo kumwekea pingamizi, ikidai kuwa mgombea huyo wa CCM ameikiuka.

  Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Kikwete amekiuka sheria hiyo kwa kwa kutangaza ongezeko la mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya umma akiwa kwenye mikutano ya kampeni.

  "Wanasheria wetu wanashughulikia suala hilo kwa kusaidiana na naibu katibu mkuu, John Mnyika kukamilisha pingamizi hilo na kesho (leo) asubuhi tutawasilisha pingamizi letu kwa msajili wa vyama vya siasa,"

  alisema Dk Slaa ambaye pia ni mgombea urais kwa tiketi ya Chadema.
  Dk Slaa alidai kuwa Kikwete alikiuka kipengele cha 6, sehemu ya 21 (1) cha sheria hiyo inayotoa tafsiri ya mambo yanayokatazwa wakati wa mchakato wa uteuzi wa wagombea na kampeni za uchaguzi.

  Alisema Kikwete amekiuka kifungu hicho kwa kutangaza ongezeko la mishahara ya wafanyakazi akiwa katika majukwaa ya kampeni, jambo ambalo linaweza kutafsiriwa na sheria hiyo kuwa ni rushwa ya uchaguzi.

  Alieleza kuwa Kikwete amekiuka sheria hiyo kwa kuwa yeye kama mgombea, hana mamlaka ya kuongeza mshahara wa wafanyakazi katika kipindi hiki cha kampeni.

  "Kwa kutungwa kwa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kusainiwa Julai 17 mwaka huu pamoja na marekebisho yake, tulitegemea kungesaidia kuleta mabadiliko," alisema Dk Slaa ambaye kitaaluma amebobea kwenye sheria.

  "Kitendo cha Kikwete kukiuka sheria hiyo kimenishtua sana.

  Watanzania tungependa kupewa ufafanuzi; fedha hizo za (mishahara) zimetoka wapi na kwa mamlaka ya nani kwa kuwa wenye mamlaka ya kuidhinisha matumzi ya fedha za umma ni Bunge," alisema Dk Slaa.
  Alifafanua kuwa kwa mujibu wa katiba, Bunge ndilo lenye mamlaka ya kuidhinisha matumizi ya fedha ikiwa ni pamoja na ongezeko la mishara kwa wafanyakazi wa umma.

  "Kitendo cha serikali kuamuru ongezeko hilo nje ya vikao vya bunge, ni ukiukwaji wa sheria za nchi na ndio mwanya uliosababisha kutoweka kwa fedha za Akaunti ya Madeni ya nje(EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT)," alisema Dk Slaa.

  "Sehemu ya tano ya sheria hiyo sura ya 21.-(1) inaweka bayana vitendo vinavyokatazwa wakati wa uteuzi wakati wa kampeni za uchaguzi na inasomeka:

  "(a)Kila mtu ambaye kabla au wakati wa kipindi cha kampeni, moja kwa moja au kwa namna nyingine yoyote, kupitia kwa mtu mwingine yeyote au kwa niaba yake, anatoa, anakopesha au anakubali kutoa au kukopesha, au anatoa, anaahidi au kumpatia au anajaribu kumpatia fedha yoyote au kitu chochote chenye thamani,

  mpiga kura au kwa ajili ya mtu yeyote kwa niaba ya mpiga kura yeyote au kwa ajili ya mtu mwingine yeyote kwa nia ya kumshawishi kupiga kura, au kuacha kupiga kura au kumrubuni mtu yeyote kutendo hicho kwa niaba ya mpiga kura huyo kupiga kura au kuacha kupiga kura katika kura za maoni au uchaguzi wowote;

  "Kikwete alisema yeye mwenyewe hahitaji kura za wafanyakazi, na akasisitiza katika hotuba yake iliyoitoa kwa wazee wa Dar es Salaam kuwa serikali haina uwezo wa kulipa mishahara hiyo na kama wanafanya hivyo kwa kushinikiza kigezo cha kura, yeye hazitaki; leo mishahara imeongezeka, fedha hizo zimetoka wapi?Tunataka utueleze matumizi hayo ya fedha za umma kinyume na utaratibu."

  Kwa mujibu wa Dk Slaa mgombea urais anapaswa kulinda katiba na sheria zilizopo, ili kulifanya taifa liendelee kuwa katika hali ya amani na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

  Dk Slaa alisema kuwa kitendo cha rais kutumia nafasi hiyo kutangaza mishahara kwenye kampeni ni kujipa upendeleo kwa kushawishi watu kumpigia kura kwa kutumia nafasi aliyonayo.

  Dk Slaa pia alitumia fursa hiyo kukemea kitendo cha kufanya maamuzi kwa kukiuka sheria zilizopo akieleza kuwa kufanya hivyo kunaweza kuhatarisha usalama wa nchi.

  Dk Slaa pia alienda mbali zaidi na kuituhumu CCM kwamba imekiuka taratibu za uchaguzi kwa kutengeneza mabango yake ya mgombea nchini Canada.

  "CCM wametumia Sh1.5 bilioni kutengeneza mabango nje ya nchi kwa kutumia fedha za serikali pia ankara ya malipo "invoice" inaonyesha imeandikwa 'VAT INVOICE' kitu ambacho hakieleweki," alisema Dk Slaa.
  Alisema kuwa ni muhimu CCM kutoa ufafanuzi juu ya hilo kwa kuwa ushahidi upo na unaonyesha kuwa kuna mchezo mchafu umeanza kufanywa.
   
Loading...