Dr Slaa kuachia ngazi CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa kuachia ngazi CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NgomaNzito, Aug 31, 2009.

 1. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwananchi iliripoti Jumamosi iliyopita kuwa wazee wa Chadema walikuwa wamepanga kukutana na Zitto ili wamuombe aondoe jina lake kwenye nafasi ya uenyekiti na kwamba, angepewa cheo cha katibu mkuu wa chama baada ya anayeshikilia nafasi hiyo, Dk Willibrod Slaa kuripotiwa kuwa anataka kujiweka pembeni na majukumu ya chama, ili awatumikie kwa karibu wananchi wa jimbo lake la Karatu.

  Source: Mwananchi

  Naona wanabodi wamekoomaa na issue ya Zitto lakini kuna pigo jingine Chadema kuachia ngazi kwa Dr Slaa la uendeshaji na utendaji wa Chama litakuwa na msukosuko mkubwa zaid kwa chama. Dr ni mtu anayeaminika sana kwa matamko yake kuhusu Chama sasa akiondoka naona itakuwa vigumu kuziba pengo hilo.

  Nafasi hii akipewa Zitto anaweza kuvaa viatu hivyo??
   
 2. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Maisha lazima yaendelee na mabadiliko mengine yapo tu. Siku zote changamoto za mabadiliko huleta maendeleo kwa wenye mikakati mizuri ya kutumia mabadiliko hayo
   
 3. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sasa watakua nashughuli gani tena hawa Chadema ktk hii campaign yao popular figure(Zitto) sio mstari wa mbele ata konvince vipi watu na sera za chama, the Dr ana nia (the heart of the battle and wisdom). Labda sawa tu kama wana CCM wasiopenda ufisadi wanavyosema. Uache CCM uande upinzani, ni upinzani gani tunao-uongelea ni vichekesho tu. na kadi yangu na mashati yangu ya CCM nayaweka.
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Labda Dr. Slaa atagombe a Urais mwaka 2010 kwa tiketi ya Chadema?
   
 5. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sioni tatizo kwa sababu anayosema Dr. siku zote ni maamuzi na msimamo wa chama sasa hata kama aking'atuka bado chadema itaendelea kusimamia mambo yake kama kawaida kwa kupitia katibu mwingine.

  Dr. yeye ni katibu wa chama na ndio maana utakuta mara nyingi anazungumzia mambo na misimamo mbalimbali ya chama na yote anayozungumzia ni msimamo wa chama.

  Halafu kusema watampa Zitto ukatibu nadhani ni kupotosha kwa sababu taratibu za kumpata kiongozi zipo wazi katika katiba na wala hawapeani uongozi kwa kujuana hivyo ni vyema wakasema tu watamshauri agombee then wanachama waamue wanataka nani awe katibu.

  Katiba ya Chadema inaruhusu wananchama kugombea na wala hakutakuwa na tatizo kwa mtu kutumia fursa yake ya kimsingi. Ila katika hili jambo la uenyekiti kwa kweli Chadema inapaswa itoe taarifa rasmi ya nini hasa kimetokea la sivyo upo iwezekano mkubwa wa chama kupunguza heshima mbele ya jamii, maana ni juzi tu tumetoka kuzungumzia ufanyaji kazi wa CCM katika mkutano wao wa Dodoma halafu upinzani unaoheshimka na wenyewe unatibua, kwa kweli wakati mwingine inatupa shida sana kuamini kuwa tukiwapa nchi mambo si ndio yatakwenda kienyeji?

  Nikiwa mtaalamu wa mambo ya habari ni vyema nikawashauri Chadema kuhahikisha wanatoa tamko rasmi haraka sana na kuuelezea umma kuhusu kujitoa kwa gafla kwa Mh. Zitto kugomea otherwise, heshima itashuka, Chadema ni CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO sasa yakifanyika mambo yenye utata kwa kweli inashangaza sana.
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kimkakati kama Chadema watakuwa wamepanga Dr Slaa aache uenyekiti ili aende kugombea Urais na kama ikiwa kuna mkakati wa vyama vya upinzani kama ilivyowahi kuwa reported kwamba mgombea Mwenza atatoka CUF Zanzibar na walimtaja Hamad Rashid Mohamed, ambaye ni kiongozi wa upinzani Bungeni nadhani kutakuwa na changamoto kubwa kwa CCM na hiyo itawavuta CUF ambao walianza kupoteza nguvu bara kwa kuonekana kama wanagombana na Chadema.

  Haya ni mawazo yangu na pia ni mawazo ya Watanzania wengi kuona CUF na Chadema, pamoja na tofauti zao wanakaa pamoja na kuchukua nchi. Kina Kibaki, Raila, Saitoti, Ruto na wengine, hawakuwa wakielewana na hawaelewani hadi sasa, lakini walifanya uamuzi kwa kufuata matakwa ya wananchi wao na wakaunda NARC ambayo ilichukua nchi. Ni Raila Odinga aliyetaja jina la Kibaki pale Uhuru Park (nilikuwapo) na alisema, "Kibaki atosha?" akaitikiwa "atoshaaaaa!!!" na yeye akasema, "basi tuacheni tukajadili na kuwatangazia" na baadaye wakajadili na kutangaza.

  Kama kina Kibaki na Raila wangefanya tofauti, na kama Moi na wenzake wangezuia mkutano wa Uhuru, basi Kenya leo hii ingekuwa kama Rwanda na matukio ya uchaguzi yangekuwa mabaya zaidi ya yaliyotokea katika uchaguzi uliopita. Haya ni mawazo yangu na ninasema kwamba viongozi wa upinzani wasome alama za nyakati na wasome matakwa ya Watanzania wengi bila kujali vyama vyao. Wajue Watanzania wa sasa wa kizazi cha dot com wana uelewa mkubwa sana na wengi ni wapiga kura wapya kabisa.
   
 7. b

  bambumbile Senior Member

  #7
  Aug 31, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania hatuna Raila Odinga. Ule uamuzi wa raila kusema anatosha huyu mzee ulikuwa wa kishujaa mno. Madaraka ni kitu kibaya mno ndio maana kuyaacha inakuwa kazi kweli kweli.

  Ni nani katika viongozi wa vyama Afrika wangeweza kusema vile? labda Nyerere kama angekuwa kwenye hali kama hiyo.

  Mwaka 1995 nilikuwa naombea tu Mrema awavute akina Mtei na hata JK na kisha kumwachia mmoja wao kugombea urais ili yeye aje awe PM. Lakini wapi hakuwa na busara hizo na akaona ataweza kuwa rais bila hata kushirikiana na vyama vingine. Matokeo yake wote tumeyaona.

  Kwa Tanzania hii ambayo hata kugombea tu mwenyekiti aliyepo inakuwa shida; tusitegemee kumwona Raila Odinga wa Tanzania siku za karibuni.
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mkuu maneno yako mazito, lakini yanaashiria hali mbaya zaidi, KUKATA TAMAA. Hatuna sababu kabisa ya kukakata tamaa kama Taifa. Wanasiasa makini lazima waangalie wapiga kura wao wanasema nini, japo kwa Tanzania hali ni tofauti kabisa na tumeona mifano ya NEC ya CCM, Butiama na Dodoma mara kadhaa na hivi karibuni maana kilichoamuliwa si matakwa ya wananchi. Angalieni maamuzi na kauli nzito ya vyama vyetu vya siasa, CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi, TLP na TPP-Maendeleo, haviashirii kulenga matakwa ya wapiga kura wetu. Angalieni vyombo vyetu vya habari, sina hakika kama kweli vimefanikiwa kubeba ajenda za umma kama si ajenda za wanasiasa, ambao mara zote wanaangalia maslahi yao ya kisiasa.

  Tumeona Wakatoliki na waraka wao wameibua mjadala, lakini umekuwa na nguvu kwa sababu umewagusa wanasiasa. Wakatoliki hawajakurupuka, wamesoma alama za nyakati. Pamoja na tofauti za kidini, bado wameonyesha njia na kwa kweli kinachohitajika ni mshikamano wa pande zote husika, kuanzia Viongozi wa dini, Vyombo vya Habari, Wanasiasa, Wapigania Haki za Binadamu, vikundi vya sanaa na muziki na kadhalika kwa nia njema kabisa ya kuhakikisha Tanzania kama Taifa tunasonga mbele.

  Serikali na chama tawala cha CCM inabidi wafumbe macho na kuamua kufuata wananchi wanakotaka waelekee hata kama ikibidi baadhi yao kupoteza nafasi zao. Hawatadharauliwa bali watakuwa mashujaa wa Taifa kwa kuepusha haya yanayotokea sasa.
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ni sala zangu kwamba Mzee Slaa hataiacha Chadema hapo ilipo kwa sasa .Inabidi isogezwe mbele .

  CUF haina nguvu bara labda waunganishe sijui iweje huko Visiwani .CUF Bara ni kama vile haiko hili walikubali .

  Wazee wamuombe Dr.Slaa kama awalivyo muomba Zitto aendelee kuwa kwenye uongozi wa Chadema bado anahitajika sana .Kuna watu wengi hapa forum mnasema tu mko Ulaya na Karekani hata kuja nyumbani hamji mana you cannot leave those countries na baadaye ukapata visa ya kurudia so mnaongea tu kwa kuwa una access ya comp.Hali ya siasa tanzania ni ngumu na watu kama Slaa , Zitto , Mbowe wana sacrifice sana .Ushabiki tuache tuje kwenye ukweli wa siasa .Kitila waambie hawa .
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Aug 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Halisi,
  Mkuu shukran na pongezi kwani mawazo yako ndio yale yanayojenga.. CUF na Chadema wanatakiwa kusoma alama za wakati..
  Dr.Slaa - For President, Mwenza akiwa Hamd Rashid, hivyo Dr. hana sababu ya kugombea tena uongozi wa chama.

  Zitto kusema kweli mtu kaa mimi nimeisha msoma na naelewa nini dhamira yake kwani nakumbuka vizuri habari ya Harper!.. Zitto hana znia mbaya kwa chama isipokuwa ni mtu ambaye Unachukulia kuwa mwaka huu 2010 - Ushindi kuwa ni lazima.

  Binafsi nampongeza sana Zitto kwa azma hiyo kwani ndani ya Chadema inaonyesha wazi kwamba Ushindi kwao sio kitu muhimu sana ila kuwaelimisha wananchi na kupigana na mafisadi. Vita ya Chadema imegeuka kuwa sio ya Kiitikadi ila ni vita against vichwa vya watu (Mafisadi) ndani ya chama CCM as if Chadema ni part au kitengo cha CCM.
  Chadema wanatakiwa kufikiria Ushindi mwaka 2010 ni kumwondoa CCM ktk utawala na sio kuendeleza kampeni za kuondoka kwa baadhi ya vichwa vibaya (mafisadi) ktk Uongozi na uwakilishi wa CCM kuwa ndio ushindi unaotegemewa..
   
 11. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka Raia Mwema waliandika

  http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1344

  http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=513
   
  Last edited: Aug 31, 2009
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Wajipanga kwa urais
  Na Mwandishi Wetu
  Mei 21, 2008


  • Masha, Membe watajwa CCM
  • Slaa, Hamad kusimama upinzani
  MIAKA miwili tu kabla ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza kipindi chake cha kwanza mwaka 2010 na huku serikali yake ikiandamwa na kashfa za ufisadi, wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na wale wa upinzani wanajipanga kwa nia ya kujiandaa kushika nafasi hiyo, Raia Mwema imefahamishwa.

  Habari zinaeleza kwamba kwa sasa baadhi ya wana CCM wanajenga msingi wa kuwawezesha kumrithi Rais Kikwete katika uchaguzi mkuu ujao lakini wakishindwa, angalau basi kwa uchaguzi mwingine wa 2015; huku wapinzani wao wakipania kuchukua madaraka mwaka 2010, wakitumia kuyumba kwa nchi katika sehemu kubwa ya awamu ya kwanza ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne.

  Kwa mujibu wa habari hizo, tayari mazungumzo na mikakati imekuwa ikifanyika katika maeneo mbalimbali nchini kwa nia ya kuangalia wanasiasa wanaoweza kushika nafasi ya urais, lakini pia kuwazuia wale ambao wanahofiwa kuweza kuharibu mikakati hiyo.

  Wanasiasa kadhaa wakubwa nchini wa sasa, wastaafu na hata wale walioguswa na kashfa, wamekuwa wakitajwa moja kwa moja kujihusisha katika mikakati hiyo ama kwa kupima upepo kama wanaweza kujitokeza wao au kwa kuandaa watu wanaowaunga mkono.

  Kwa upande wa upinzani, wanasiasa wapya kabisa wanatajwa kuweza kuibuka na kwa kupishwa na wanasiasa waliogombea katika Uchaguzi Mkuu uliopita, ikiwa ni mkakati unaoelezwa kujaribu kuwavuta wapiga kura wengi.

  Imeelezwa kwamba waliogombea katika chaguzi za nyuma ikiwa ni pamoja na ule wa mwaka 2005, kupitia vyama vya upinzani, wanaweza kuwaunga mkono wagombea watakaouzika katika uchaguzi wa mwaka 2010.

  Wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuweza kusimamishwa kwa nafasi ya urais kwa upande wa upinzani ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa na Kiongozi wa Upinzani ndani ya Bunge, Hamad Rashid Mohamed, ambao wanaelezwa kuweza kukubaliana mmoja akawa Mgombea Mwenza.

  Wanasiasa hao wa upinzani wanaelezwa kusukumwa zaidi na wabunge wenzao pamoja na watu wa kawaida wanaofuatilia mwenendo wa kisiasa nchini hasa kutokana na mchango wao ndani ya Bunge ambalo limebadili hali ya kisiasa nchini kwa kurudisha mwamko wa wabunge na wananchi.

  Hamad Rashid amelithibitishia Raia Mwema jana kwamba ameshauriwa kujiandaa kuwania urais mwaka 2015 lakini baadhi wametaka aanze mwaka 2010, akiwataja baadhi ya wabunge waliomshauri, wakiwamo hata wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
  "Ni kweli nina nia ya kuwania urais lakini si wa Zanzibar na kwamba nilijiandaa kwa mwaka 2015, lakini wabunge wenzangu baadhi kutoka CCM wamenishauri nianze kujitokeza mwaka 2010," alisema Hamad, ambaye amewahi kuwa ndani ya Serikali ya Muungano katika wizara za Fedha na baadaye Mambo ya Ndani.

  Akizungumzia suala hilo, Dk. Slaa alisema sasa ni mapema mno kuzungumzia mambo ya urais kutokana na nchi kuwa katika harakati za kupambana na ufisadi unaoihusisha hata Ikulu yenyewe.

  Alisema Dk. Slaa: "Bado tuko mbali tukipambana na ufisadi. Nchi haitaki wanaokimbilia Ikulu. Inataka wenye ujasiri wa kusafisha Ikulu. Ukisema nawe unakimbilia Ikulu, unakuwa unataka ukafanye biashara au ukachote Ikulu. Wakati ukifika, hayo tutayajadili."

  Kwingineko kumekuwa na minong'ono kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chacha Wangwe pia ana nia ya kugombea kwa tiketi ya chama. Nia ya kuwania urais ya viongozi hao wawili huenda ikawagombanisha na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, aliyesimama mwaka 2005 na ambaye inaaminika angependa asimame tena mwaka 2010.

  Alipoulizwa kuhusu habari hizo za yeye kutajwa kuwania urais, Chache Wangwe alisema, "Ni kweli, ikiwa chama changu kitanipendekeza, nitakua tayari kugombea."

  Mkanganyiko mwingine wa Chadema unaweza kutokana na habari kwamba Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, akizungumza na Watanzania walioko Houston, Marekani alikokuwa kwa ziara hivi karibuni, alisema atawaunga mkono Dk. Slaa na Hamad kama mazingira ya kisiasa yatawafikisha watu hao wawili katika kugombea mwaka 2010.

  Siku za karibuni zimeshuhudia kutoaminiana miongoni mwa viongozi wa Chadema na hata kumhusisha Zitto na madai ya kuwa na urafiki wa karibu na Rais Kikwete, kiasi cha Kikwete kutaka kumteua kuwa waziri katika Serikali kabla ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ya Februari mwaka huu.
  Zitto ameiambia Raia Mwema wiki katika mahojiano kuwa wakati hapingi kuwa ana ukaribu wa kiasi fulani wa siku nyingi na Rais Kikwete, hakuna wakati alipotaka kuingia katika serikali yake.

  "Sijawahi kuombwa na Rais Kikwete kuingia katika serikali. Msimamo wangu siku zote umekuwa ni kutumikia taifa bila kujali itikadi. Hata Rais anajua hili, kwamba siwezi kuhama chama au kwenda kinyume na maamuzi ya chama changu. Kwamba Rais Kikwete ni rafiki yangu, si kweli. Ninafahamiana naye kitambo. Ninajua ananiheshimu sana. Lakini hakuwa chaguo langu la urais wakati wa mchakato wa chama chao na hata katika uchaguzi mkuu," alisema Zitto.

  Lakini wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa wanasema Zitto hajawahi kusikika akimshambulia Rais Kikwete katika hotuba zake na mara kadhaa amekuwa akimsifia katika maamuzi yake mbalimbali ambayo yamepingwa na wenzake. Hata kuingizwa kwake katika Kamati ya Madini ya Jaji Mark Bomani kulizua maswali mengi kutoka kwa wanasiasa wa CCM iliyombana alipoibua hoja ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, na wa Upinzani.

  Wengi hawaamini maelezo ya Zitto kwani anaonekana ni mtu mwenye kujiandaa kutokana na kuwa kwake na mahusiano ya karibu sana na wastaafu kama Jaji Joseph Warioba na Dk. Salim Ahmed Salim, watu ambao wana ushawishi mkubwa katika jamii.

  Alipoulizwa kuhusu hili Zitto alisema kuwa yeye anawaheshimu sana viongozi wastaafu na hupenda kujifunza kutoka kwao na mahusiano yake nao hayana maana ya kutafuta kuungwa mkono.

  "Nimekuwa na mahusiano na wazee hawa kama viongozi. Sio hawa tu. Ninazungumza na mzee Kaduma (Ibrahim), mzee Butiku (Joseph), mzee Kimiti (Paul) na mzee Jackson Makweta. Pia ninazungumza sana na Spika Samuel Sitta. Huwezi kusema hawa wote wananiandaa mimi kuwa Rais. Huo ni woga tu wa watu. Ni hulka yangu kuheshimu wakubwa na kujifunza ndiyo maana ukinikuta na Hamad Rashid hutaona mahusiano ya kiubunge. Utaona mahusiano ya mwalimu na mwanafunzi," anasema Zitto ambaye mwaka jana gazeti moja la kila wiki lilimshutumu kwa kujipendekeza kwa viongozi wakubwa.

  Kwa upande wa CCM, habari zinaeleza kwamba tayari makundi yameanza kujipanga kwa uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2010 na wa 2015 kama Rais Jakaya Kikwete atafanikiwa kushinda patashika ya mwaka 2010 na kuendelea muhula wa pili ambao ni wa mwisho kwa mujibu wa katiba.

  Makundi hayo yanajipanga mapema na kwa kuanzia imeelezwa kwamba wanasiasa na wafanyabiashara wanajiandaa kuweza kupata wajumbe wa kutosha katika Mkutano Mkuu wakati wa uchaguzi, wajumbe ambao ndio watakuwa waamuzi wakubwa wa mgombea kutoka chama hicho.

  Licha ya kwamba kuna fununu za wagombea wengine kujitokeza kushindana na Rais Kikwete katika kinyanganyiro cha ndani ya CCM mwaka 2010, inaonekana uwezekano wa ushindi ni mdogo kutokana na utamaduni wa CCM kuendeleza muhula wa pili wa Rais aliyeko madarakani utaendelea. Hata hivyo, hali inaweza kubadilika kama Kikwete atakumbwa na dhoruba yoyote kubwa ya kisiasa kabla au kuelekea 2010.

  Magazeti kadhaa, hivi karibuni, yalimtaja Profesa Mark Mwandosya kama mgombea anayetajwa kuweza kumkabili Rais Kikwete ikifika mwaka 2010. Mwandosya alikuwamo katika hatua za mwisho za mbio za urais mwaka 2005.

  Wengine wanaotajwa kwa sasa kwa upande wa CCM kujiandaa ama kuandaliwa kumrithi Kikwete, iwe 2010 au 2015, ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrance Masha na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

  Kumekuwapo pia na mijadala ya Watanzania, na hasa walioko nje, inayotaka Dk. Salim agombee ama kupitia CCM au kupitia muungano wa vyama vya upinzani. Yeye na Profesa Mwandosya walishindwa na Kikwete 2005, wote wakiwa wamefikia hatua ya mwisho kabisa.
   
 13. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hii story ya Raia Mwema ya Mei, 2008 ilitabiri mambo mengi yanayoendelea sasa. Tuisome kwa makini. Ilitoka kabla ya Chacha Wangwe kufa.
   
 14. b

  bambumbile Senior Member

  #14
  Aug 31, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lunyungu,

  Acha hizo kamba zako. Wewe kuwa na visa hapo Holland mara hii unaanza kusagia Watanzania wenzako wanaoishi nchi zingine?

  Kama hawana visa inatakiwa uwaombee na wenyewe wafanikiwe na sio kuingiza vijembe.

  Umeongea upumbavu hapo juu na imebidi nikuambia ukweli kwamba uko Holland.

  Wengine pia tumewahi kuishi bila visa Europe wakati tunatafuta na sasa tumerudi nyumbani lakini hatudharau wenzetu ambao bado wanahangaika.

  Kuwa mwungwana brother! Acha vijembe visivyo na maana, au unataka mpaka tutaje na jina lako ndio ujue tunakufahamu vizuri?
   
 15. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lazima tusonge mbele sana na hivyo ni lazima kuona kuwa kuna haja ya CHADEMA kujipanga kwa ajili ya mwakani na ni tegemeo kubwa sana kwa Watanzania wote
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Aug 31, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,867
  Trophy Points: 280
  Well said Mkandara, we need people like you!!!!!!! kujadili vichwa inaumiza tutajaza post kibao hapa, nukisema hili naonekana mpinzani, CCM has to go away no matter what, sio nchi yao hii!!! safisha wote, wasafi nature itawaselect

  Hao wanasacrifice kuliko MKJJ? mkuu dunia hii kama Kijiji, walio nje wanapata data za siri nyingi na kufungua macho ya wengi, kupigana popote, ukiisha anza habari ya utoto kuwa kabla ya kupigana chora mstari chini, vua viatu vitaniumiza, mara hoo hakuna kutumia jiwe, wala hakuna kuuma, you are wasting your time, Jeshi ni jeshi haijalishi ni wa kikosi gani! mtu kama wewe hutakiwi kuongea haya, hao wa nje wako wangapi na Tz wako wangapi, mpaka umeweza kujua kuwa ndio wanaoongea na kushauri ujue 'WAMO, WA WAKWETU HAWA' wakikaa kimya, utawafanya nini?

  Ogopa kuwagawa watu wakiwa vitani!
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Join Date: Sun Aug 2009
  Posts: 6
  Thanks: 6
  Thanked 1 Time in 1 Post
  Rep Power: 0

  Mhhhhhhh lugha mbaya!
  Pamoja na ugeni wako hapa hatuongei kwa hasira hivi.
  Tulia sema kwa lugha nzuri utaeleweka.
   
 18. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Itakuwa ngumu kumpitisha Dr. Slaa 2010.

  Mtaniambia hii ni hoja ya udini lakini ukweli ni kwamba maraisi wawili waliopita walikuwa 'Wakatoliki' na sidhani kama 'Waprotestanti' watakubali nafasi hii iwapite pembeni. Tuliona mwaka 2005 jinsi Walutheri walivyojitahidi kumbeba Mrema ingawa hakuweza kufanikiwa.
   
 19. K

  Koba JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Siasa za Bongo ni ngumu sana...zimejaa rushwa tuu na utemi na wapiga kura wasiokuwa na akili kabisa!
   
 20. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  People you must be joking. Lawrence Masha aongoze Tanzania, are we really serious?? nchi itakuwa kichekesho kweli. wizara ya mambo ya ndani imemshinda, taifa ataweza?
  Membe urais? kwa kipi? Au ndio siasa zenyewe za mitandao?? CCM ina wengi wenye personality na uwezo wa kuwa viongozi wa nchi, si hao wawili. I stand to be corrected.
   
Loading...