Dr Slaa kama Ditopile

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Dk. Slaa atisha mtu kwa bastola




na Tamali Vullu



MBUNGE wa Karatu, Dk. Willbrod Slaa (CHADEMA), ameingia katika mzozo na mtu aliye na mgogoro naye kuhusu shamba, baada ya jana kumtishia kwa bastola.
Dk. Slaa mwenyewe alilithibitishia gazeti hili kuwa alilazimika kuchomoa bastola yake na kupiga risasi hewani kwa lengo la kumtisha kijana huyo, mkulima mmoja wa Karatu, katika ugomvi wa shamba.

Katika tukio hilo, Dk. Slaa, alisema kuwa alifyatua risasi moja hewani kwa lengo la kuzima tafrani iliyoanzishwa na mkulima huyo, Daniel Yanffan Areso.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu kutoka Karatu, Dk. Slaa, alikiri kufyatua risasi hiyo baada ya kijana huyo kumvamia yeye na watoto wake walipokuwa wanalima shambani humo kwa kutumia trekta.

Alisema akiwa shambani na watoto wake, mkulima huyo alifika shambani hapo akiwa na fimbo na kuanza kumchapa dereva wa trekta hilo.

"Kutokana na hali hiyo, vijana wangu waliingilia kati, lakini nilipoona ugomvi umekuwa mkubwa, nilifyatua risasi hewani ili kumtisha kijana huyo," alisema Dk. Slaa.

Alisema baada ya muda polisi walifika kwenye eneo hilo na kuchukua maelezo yake kuhusu tukio hilo.

Dk. Slaa alisema anashangazwa na kitendo cha mkulima huyo kudai shamba hilo ni lake, kwani yeye alilinunua mwaka 1999.

Alisema kutokana na tukio hilo, polisi wamemshauri kufungua kesi ya jinai dhidi ya mkulima huyo kutokana na kumvamia katika eneo lake na kumfanyia vurugu.

Naye Areso akielezea tukio hilo, alisema Oktoba mwaka huu alipanda maharage na mahindi katika shamba hilo, lakini alishangazwa na kitendo cha mbunge huyo kwenda kulima shambani kwake.

Alisema jana alipofika shambani hapo, alianza kumzuia dereva wa trekta asiendelee kulima, ndipo watoto wa Dk. Slaa walimvamia na kuanza kumpiga sehemu mbalimbali mwilini.

Areso alisema katika tukio hilo, Dk. Slaa alitaka kumuua kwa kumfyatulia risasi, ambayo kwa bahati nzuri ilimkosa.

"Nilipoona hivyo, nilikimbia na kwenda kutoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kumchukua Dk. Slaa na kumpekea kituoni.

"Katika maelezo yake, polisi alieleza kuwa alifyatua risasi hewani, lakini alifyatua akinilenga kutaka kuniua na bahati nzuri ilinikosa," alisema.

Areso, alisema kutokana na tukio hilo amefungua jalada namba KRP/RB3032/2007 linalohusu shambulio.

Alisema kutokana na kupigwa fimbo sehemu mbalimbali mwilini, anahisi maumivu makali na amekwenda zahanati ya serikali ilyopo jirani ambako amepatiwa matibabu
 
haya tuonge ssa

wanaulizana kwa nn upinzani tanzania uko mnyaufu kuliko kenya?

majibu yako wazi, wapinzani wenyewe wanyaufu maradufu
 
Mbona nilisikia kwingine kwamba Dr Slaa alifyatua risasi hewani kuwatanya wananchi ambao walikuwa wameanza kuongezeka kumshambulia mvamizi wakitaka kumuua. Inasemekana ni baada ya risasi kufyatuliwa hewani ndipo jamaa alipopata wasaa wa kutoroka. Zitto si yuko hapa? hebu atupe ukweli kuhusu sakata hilo- Dr Slaa hawezi kufananishwa na Ditipole fisadi wa mjini.
 
Magazeti ya Tanzania na waandishi wao bwana . Wanaweza kusema jambo ukadhani kuubwa kumbe ni utumbo mtupu .Hivi hizi chokocjoko dhidi ya slaa mbona zinakuwa nyinyi ?
 
Mkomboziufisadi,
Huwa husomi habari nzima? Mbona kwenye habari inaonyesha wazi ni Tanzania Daima?
asante mkuu.nimeshaelewa..kazi ni nyingi hivyo huwa napitia btn lines tu,nina kazi za kupitia thesis za watu na majukumu menghine ya kujenga taifa..hapa ndio nimeshika gazeti la tanzania Daima naosma habari hiyo.
 
Hii huwezi kuilinganisha na ya Ditopile kabisa, Dito alikuwa public place, Slaa hakuwa public place alikuwa kwenye shamba lake na huyo mtu ali-trespass yaani kumuingilia eneo lake la private.

Kwanza ninavyojua jinsi heshima na desturi za kule kijijini zilivyo huyu mtu asingeingia hivi hivi tu kwenye eneo la Mbunge wake, bali angeenda kwenye uongozi wa kijiji au polisi na kushtaki kuwa mbunge kaniingilia shamba langu, lakini jinsi jamaa alivyomvamia mbunge na wanae inaonyesha wazi kuwa huyu mtu zile desturi za kijijini hana au ametumwa kumuanzishia Slaa sakata na sahizi labda ashapokea mshiko wake.

Tanzania kuna watu wanajaribu kutumia kila njia kumuharibia mtu ambaye yuko mstari wa mbele kutetea wananchi na kufunua maovu. Lakini Watanzania siku hizi si mambumbumbu sana kama zamani, haya wanayaona kabisa.
 
Huu ndiyo ukweli maana kwa tabia huyu Slaa si mlughalugha kama akina Ditto na Kinje .Hapa kuna namna ila wachoraji wa mchezo wanakosea kila mara . Wacha tutayasikia mengi .
 
Kuna mchezo mchafu wa kujaribu kumchafua slaa, kwa maelezo ya huyu jamaa haiwezekani huyu jamaa alengwe risasi katikati ya watu ( watoto wa slaa waliokuwa wanmpiga)

Pili anasema alipanda maharage mwezi octoba mwaka huu, slaa anasema hilo shamba ni lake toka 1999. Je alipata kibali cha kupanda hayo maharage yake kwenye shamba la slaa?

Hapa kuna shaka kubwa, hii ni michezo ya siasa zilizofiliska na mbinu chafu inayotumiwa na mafisadi ili yaendelee kuitafuna nchi hii. Yapo tayari kumlipa mtu kiasi chochote cha pesa anayoitaka mhanga ili mradi tu atekeleze matakwa yao
 
Kuna mchezo mchafu wa kujaribu kumchafua slaa, kwa maelezo ya huyu jamaa haiwezekani huyu jamaa alengwe risasi katikati ya watu ( watoto wa slaa waliokuwa wanmpiga)

Pili anasema alipanda maharage mwezi octoba mwaka huu, slaa anasema hilo shamba ni lake toka 1999. Je alipata kibali cha kupanda hayo maharage yake kwenye shamba la slaa?

Hapa kuna shaka kubwa, hii ni michezo ya siasa zilizofiliska na mbinu chafu inayotumiwa na mafisadi ili yaendelee kuitafuna nchi hii. Yapo tayari kumlipa mtu kiasi chochote cha pesa anayoitaka mhanga ili mradi tu atekeleze matakwa yao

Mi nashauri Dr Slaa amuingize huyu jamaa kwenye orodha ya mafisadi. Awe fisadi namba 12 aliyefisadi shamba na akaendeleza ufisadi wa kuzusha kuwa alitaka kupigwa risasi katikati ya kundi la watu waliokuwa wakimpa kipondo!

Asha
 
hii yote ni sehemu ya mapambano ya kifikra; si mnaona jinsi ilivyounganishwa mara moja na la Ditopile? Lengo ni kuwafanya wote wakose credibility. Kwanini hawakumlinganisha na mtoto wa Kingunge? Kwanini hawakulinganisha na viongozi wengine huko nyuma ile iwe Dito?

Kila raia anayo haki ya kulinda uhai na mali yake hata ikimlazimu kuua. Ditopile alikuwa na haki kama Dito endapo yule Dereva angeibuka na panga au alipoenda kwenye kipanya chake basi angeonekana amechukua silaha kumfuata Dito. Lakini mtu kajikalia ndani ya gari na vioo kafunga.

Na bado wanakuja na kisasi; wanakuja mwaka 2008 wakijiandaa mapigo; wamekasirika, wamenuna, na hawana hamu yaliyotokea 2007 yatokee 2008; kaeni "ready" kwani simba amejeruhiwa na sasa yuko tayari kupigana!
 
Kama habari zilivyoandikwa kwenye gazeti la Tanzania Daima ni sahihi, basi hali halisi ni kama ifuatavyo:

Kaja mtu na fimbo yake na kaanza kushambulia mfanyakazi wa Slaa. Slaa naye katoka na "fimbo" yake, ila hakushambulia, bali katishia kushambulia, kwa kuifanya fimbo yake ikohoe kidogo. Hakumpiga mtu risasi. Huyo mvamizi anadai alilengwa risasi; kwani kaiona ikipita karibu naye?

Mtu ukiwa shambani kwako na ukapiga risasi hewani ni haki yako. Hata kama kuna mvamizi bado ni haki yako kupiga risasi hewani.

Ama kweli bado tuko nyuma! Mtu utakwenda kupigana kwa fimbo shambani kwa mbunge wako ambaye analima na trekta? Ona sasa mbunge mwenyewe ana fimbo ya kisasa na angeweza kumjeruhi kwa madai ya kujilinda. Hilo lingekubalika.

Slaa ni kiongozi wa kweli wa Watanzania. Wanaomtafuta hawatampata, kwani tutaendelea kuamini asemacho yeye. Ni umbumbu uliokithiri kumlinganisha na Dito.
 
Wala msihangaishe vichwa,
Angalieni 'tu foot prints' za ''Paparazi muwazi'' Nahisi kuna watu wako kazini hapa!

Mada iko sawa, ila kichwa chake kina sema Slaa kama Dito
Angalieni ile mada nyingine alo anzisha anasema
Zitto na Mnyika kumzilia Mbowe CHADEMA

Paparazi kama huna ajenda ya siri anzisha mada zenye vichwa vinavyo endana na mada yenyewe siyo vinavyo mfanya mtu aelewe vinginevyo kabla ya kuisoma mada yenyewe!
 
yaani hizi habari zanikumbusha magazeti ya udaku bongo...kicha cha habari mbele kingine tena kikuuubwaaaaa kuvutia wanunuzi wa magazeti...ingia ndani usome mwee mbona utajuta kununua hata hilo gazeti??

sasa hii yafananishwa vipi na kesi ya Ditopile?au ndo katika kujaribu kuwasema watu wa upinzani wafananishwe maovu yao na ya CCM??kwani hewani ndiko kwenye dirisha la basi na kichwa cha dereva wa dala dala??
 
Back
Top Bottom