Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...!

Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...!

Mkuu Kengemumaji na wakuu wangu GT wa JF! Taasisi kama CCBRT ni kubwa na mambo mengi inayoyafanya hapa nchini kila mtu anaweza aka-google na kujisomea. Dr. Slaa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Shughuli za kila siku zinasimamiwa na Mtendaji Mkuu ambaye ni mzungu. Wanaandika ktk mtandao wao kwamba wanatibu wagonjwa 120,000 kwa mwaka. Ukisoma zaidi unaona wengi kati ya wagonjwa wa Fistula ambao wanatibiwa bure wanatokea mikoa ya Nyanda za Juu Kusini huko Njombe,Ludewa na Songea. Sikufanikiwa kupata gharama zao kwa huduma nyingine. Lakini mtu yeyote anaweza akaingia ktk wavuti yao ambayo ni; www.ccrbt.or.tz
hili ulilolifanya ni la msingi sana...!
 
Kaka ushapiga kura tayari.Mi najua uchaguzi bado.Huyo slaa iwaje tena?
We wapi huelewi???hakuna asiyejua hili, tena naimani hata wewe ukijufunika shuka usiku ukitulia kabisa kitandani ukweli unauona ila hapa unajifanya huelewi, sio fair mlichakachua.
 
Mkuu Kengemumaji na wakuu wangu GT wa JF! Taasisi kama CCBRT ni kubwa na mambo mengi inayoyafanya hapa nchini kila mtu anaweza aka-google na kujisomea. Dr. Slaa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Shughuli za kila siku zinasimamiwa na Mtendaji Mkuu ambaye ni mzungu. Wanaandika ktk mtandao wao kwamba wanatibu wagonjwa 120,000 kwa mwaka. Ukisoma zaidi unaona wengi kati ya wagonjwa wa Fistula ambao wanatibiwa bure wanatokea mikoa ya Nyanda za Juu Kusini huko Njombe,Ludewa na Songea. Sikufanikiwa kupata gharama zao kwa huduma nyingine. Lakini mtu yeyote anaweza akaingia ktk wavuti yao ambayo ni; www.ccrbt.or.tz
Brazaaaaaaa..,hizo tuhuma zinataja wagonjwa wa fistula tuu..?
 
Majungu mengine bwana, mimi ni mtu wa kutoka Iringa, kaka yangu anaishi Mbeya na alikua na tatizo kubwa sana la jicho la kushoto, alishughulikiwa kwa muda mfupi sana tu, kwanza ilikuwa tumpeleke Mwezi december baadhi ya rafiki zetu wa Dar wakatwambia (Nadhani walikuwa wana hisi, hawakuwa na uhakika) mwezi huu madaktari wengi wa kihindi wameenda kwao kwa mapumziko so tulirudi mwezi February ana alipata matibabu bila ubaguzi wowote, Mleta hoja siku nyingine uwe unakuja na ushahidi na sio kuja na Cooked data hapa.

Huko nyuma tuliwahi kuaminishwa kuwa Nyerere ndiye aliyefuta mahakama ya Kadhi nchini, ukweli huu uliendelea sana hata nami nikauamini but siku Kikwete anahutubia sherehe za Idd-el Fitri pale Dodoma nilimsikia akisema, "Nchi hi haijawahi kuwa na mahakama ya Kadhi, waliokuwepo ni maliwali ambao walihukumu bila kuzingatia dini ya mtu bali sehem husika, yaani kama kwetu Iringa walihukum kwa kuzingai uenyeji tu" Kuanzia wakati huo nimekua pro active kusikiliza malalamiko ya watu hasa wanapolenga kumchafua mtu au Chama hasa cha upinzani.
 
Huu ni upupupupupupupupupupupupu!!!! Jinsi CCM inavyopenda majungu, huu ungekuwa ni mtaji namba moja wakati wa kampeni za urais 2010. Kama Makamba aliweza kumnunua mtu aliyejifanya ni mume wa Mushumbusi, mpaka akafungua kesi ya madai mahakamani kumchafua Dr. Slaa, kweli aliikosa hii skendo? Utafiti wa 2008 uujue wewe Maralia Sugu leo? Intelijensia ya CCM iliweza kujua majasusi walioingizwa Igunga na CDM, wasijue ufisaji na ukabila wa Dr. Slaa (Muiraqwi) kwa wachaga? Jinsi walivyopiga kampeni chafu za udini na ukabila kweli hii ishu CCM hawakuijua? Hovyo!
 
Dr. Slaa ajibu tuhuma zipi? Mbona sizioni? Acha majungu.
 
Niliyaandika haya miezi mitatu iliyopita na badala ya kupata majibu (kwa kuwa hakuna majibu hayo) nikapata kejeli na kebehi za wafuasi wa Dr Slaa.,haya haya ama ya mfano wa haya yanaelezwa tena leo kumhusu Dr Slaa na CCBRT. Dr ni vema ukiwaeleza watanzania ukweli, na kwa ukweli huo ukuweke huru wewe lakini pia ukiweke huru chama chako. Si busara kuendelea kukaa kimya katika hili. Wanasema kukaa kimya kinga lakini mara nyingine kukaa kimya ni mauti.
 
Sioni cha kujibu. Dr. Slaa endelea na shughuli zako achana na thread za kinafiki kama hizi.
 
Hii post ilishajibiwa siku nyingi chakushangaza ili tope limeicopy likaileta tena leo
 
Ama hakika mtaji wa MASKINI ni MAJUNGU watu walikua hawajui ka Dr Slaa ni mwenyekiti wa Bodi pale CCBRT now imejulikana na ni kiongozi mkubwa wa chama kinachojiandaa kushika Dola wanaamua kumchafua Hii ni aibu na MUUNGWANA Hawezi jibu UJINGA HUU
 
Ni hoja nzuri kujibiwa itatupa mwanga mzuri zaidi na kumuweka huru Dr Slaa.inajulikana sana kuwa mtendaji wa kila siku ni mzungu yupo pale ila majibu yatasaidia sana sana kuelimisha jamii iliyopewa data za upande mmoja!!!
 
tuhuma huwa na kawaida ya kusubiri kuwa proved wrong or right..,ni tabia yake kile kiitwacho "TUHUMA" na mwenye tuhuma atabaki kuwa na jina mtuhumiwa na si muhalifu mpaka pale itakapothibitika beyond reasonable doubt kuwa ni kweli hilo analutuhumiwa kwalo kalifanya.

Mimi naiona sababu ya Dr. Slaa kuja kukubali, kukanusha ama kwa namna yoyote ile kulitolea ufafanuzi jambo hili. Lakini ukimya ukiendelea, hakika watu watajipa majibu wao wenyewe, lakini naamini wengi katika watakaojipa majibu hayo watajipa majibu hasi juu ya Dr kwa kuwa utata huzaa wasiwasi unaopelekea ukanusho.

Ni Busara kuwaambia watu kile wanachotakiwa kujua.
 
Mtoa mada, hata ukienda Mvumi- hospitali ya Misheni ambayo imespecialize kwenye matibabu ya macho bado utakuta takwimu zinakuonyesha kuwa si wagogo wengi wanaotibiwa hapo - Jiulize ni kwa nini?
 
Dr ajibu nini hapa!
Mnapenda kuwapandisha chat baadhi ya wapinzani!
 
Bado binafsi naiona sababu ya Dkt Kuja kujibu Tuhuma Hizi...!
 
Kuhusu surgery ya cataract nakataa ukisema bei yake ni 680,000 kwa kuwa nilifanyiwa surgery hiyo mwaka jana kwa
70,000, acha uzushi, habari ndeeefu lakini umejaza uzushi mtupu!
 
Kama hawa wagogo na wazaramo wanaumwa wanaogopa kwenda hospital unataka watu wa kaskazini wasiende kisa idadi yao kubwa? Kwa kuajiriwa waliotangulia kusoma ni akinanai? Wamakonde wazaramo au wakwere? Ajira zinatolewa kwa kuangalia taaluma.hakuna taasisi yoyote kubwa utakayo ingia umkose mchaga,

mwambie ukwel,anaisifu serikal kutoa bilion1,wakat bajet ya pale sio chin ya bilion 6,huyu kakurupuka kama yle magamba jmos viwanja vya chadema.
 
ni wale maTISS wa darasa la saba au chini ya hapo! Hivi mwenyekiti wa bodi ana monitor services kwenye instition!
 
Dr hatakiwi kujibu ***** kama huu, mleta hoja aende shule ya uongozi harafu ajitafakari apime km kuna hoja!
 
Dawa ya mjinga pamoja na bags & packagges zake ni kumpuuza tu. Dr Slaa endelea na shughuli za kitaifa, haya ni maji machafu ya chooni!
 
Back
Top Bottom