Elections 2010 Dr Slaa ITV Live sasa

Ndo ile reform program ya ITV sio? namwona na magwanda yake anazungumzia watu wanaoishi kwenye nyumba za tembe 50 years on
 
ameongelea umaskini, nyumba bora za nafuu, elimu bure, afya bure na anaongelea atakavyopata pesa za zoezi hilo
 
sasa hivi anatackle issue ya muungano..anasema kuwa jibu la matatizo ya Muungani ni kuwa na serikali TATU......Tanganyika, Zanzibar na ya Muungano utacaoshughulikia mambo ya fedha, ulinzi nk
 
Kwa mara ya kwanza nimebubujika machozi -- hasa pale alipochambua sera yake ya elimu bure na afya bure kwa kugusia kuwa Nyerere aliweza hivyo bila ya kuwa na migodi ya dhahabu na madini mengine mengi -- na pia kubanwa na wafadhili!!

Kwa mara ya kwanza naamua kumpa kura yangu Dr Slaa na ninaahidi kila siku nitajaribu kuwashawishi watu wengine kumi wafanye hivyo. Na ninawaomba watu wenye nia njema na nchi hii wafanye hivyo. Machozi yalizidi pale alipojibu swali la uamuzi wa kugombea kwake -- kwamba alitetemeka wakati anaombwa hivyo.

Kwa mara ya kwanza pia nimeelewa kwa nini JK hataki mdahalo: Hana ufasaha wa kuongelea mambo. Na huo ndiyo ukweli jamani, baada ya kumsikiliza mheshimiwa Dr Slaa.
 
Kwa Mahojiano ya Leo, Dr. Slaa amezidi kumtisha JK, nakwambia hata kwa Bunduki JK hatii timu kwenye mdahalo, Dr. Slaa ni Naumer
 
Kwa mara ya kwanza nimebubujika machozi -- hasa pale alipochambua sera yake ya elimu bure na afya bure kwa kugusia kuwa Nyerere aliweza hivyo bila ya kuwa na migodi ya dhahabu na madini mengine mengi -- na pia kubanwa na wafadhili!!

Kwa mara ya kwanza naamua kumpa kura yangu Dr Slaa na ninaahidi kila siku nitajaribu kuwashawishi watu wengine kumi wafanye hivyo. Na ninawaomba watu wenye nia njema na nchi hii wafanye hivyo. Machozi yalizidi pale alipojibu swali la uamuzi wa kugombea kwake -- kwamba alitetemeka wakati anaombwa hivyo.

Kwa mara ya kwanza pia nimeelewa kwa nini JK hataki mdahalo: Hana ufasaha wa kuongelea mambo. Na huo ndiyo ukweli jamani, baada ya kumsikiliza mheshimiwa Dr Slaa.
Shukrani Mkuu, kuwa sehemu ya Mabadiliko.
 
AAH Jamaa zangu wananiambia umeme umekatika kabla ya kipindi kwisha, halafu umerudishwa baada ya kipindi. Haya mambo haya.....
 
Mwenye macho ya kuona ameona, mwenye masikio ya kusikia amesikia. Dr anajua kujieleza jamani, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Nimependa jinsi anavyomuogopa na kumuomba MUNGU.
 
AAH Jamaa zangu wananiambia umeme umekatika kabla ya kipindi kwisha, halafu umerudishwa baada ya kipindi. Haya mambo haya.....
Too late. Ujumbe ulishafika. Na tumeshampata Hard Hitter na wenzake 10 kwenye column.
 
Dr. Slaa anatisha. ndo maana CCM wameamua kubeba wapiga kura ili wawaonee huruma hapo 31.10 lakini wapi!
 
Back
Top Bottom