Mh. Dr. Slaa. Naomba kuwasillisha hoja zangu 2 kwa sababu wewe ndo unapaswa kubeba hizi rawama moja kwa moja ukiwa ndo mtendaji mkuu. 1. Wabunge wetu wote wawili jijini Mwanza wameamia Dar es salaam pamoja na familia zao wanakula maraha, na wakiacha mwanza haina viongozi wa kuwatetea. Hisipokuwa wakipewa taarifa kuwa kuna viongozi wa juu wa chadema wanakuja mwanza ndo nao wanakuja. Ukiwa kiongozi unaweza kumtofautisha mbunge aliepita na hawa wawili? Mbunge aliyepita naye alifanya hivi hivi alipochaguliwa huyo akaamia dar, wakati wa kura akarudi na akapigwa chini, hivyo na hawa sasa wakagombanie ubunge uko dar wanapoishi na si mwanza tena. 2. Tunatatizo la soko kuu la mwanza jini ni chafu sana hakuna choo watu wanajisaidia humo hili wala Wenje hajui si anaishi daaaaaaaaaaar. Anashindwa ata kuomba gari la manispaa la maji tusafishe Asante nawasilisha!! Mimi sikuelewi kutetewaje na hao wabunge kwa sababu kwa ufahamu wangu watetezi wa wananchi wa Mwanza wako wengi sana kwa kukutajia ni kwa mfano: RC tena kada wa CCM na Mteule wa Rais,City DirectorDiwani kwa kila Kata na wengine wengi tu na ambao wana maamuzi na utendaji wa moja kwa moja.Na kwa vyovyote vile tatizo la Mbunge au wabunge kutokukaa na kutulia katika majimbo ni tatizo la ki-mfumo na kinacholalamikiwa Mwanza ndicho tunachokilalamikia hapa kwetu Shinyanga kwa mbunge wetu Steven Massele ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini.......Sasa tutasemaje?....jibu ni rahisi tu kuwa mfumo wetu wa kuendesha mambo yetu(utawala) kama nchi ni mbovu,hauwalazimishi na kuwabana wawakilishi na watumishi wengine wa wananchi kutekeleza majukumu yao ipasavyo!! Hata wewe leo uingie katika mfumo wa dizaini hii kama mbunge au katika nafasi yoyote ya utumishi wa umma utajikuta tu system inakufunika na inakuongoza wewe.Hawa wabunge wa Mwanza na wengine karibu wote katika majimbo karibu yote ni waathirika tu wa mfumo huu mbaya tulionao LAKINI lililo zuri na labda la manufaa kwao ni kuwa wao ni wanufaika wa mfumo huu na sisi ambao hatumo kwenye system kazi yetu itakuwa ni kulalamika tu