Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,100
- 5,649
Bora mmejua kua mwisho wa siku binadamu ni binadamu tu awe kutoka ccm au cdm wote ni wezi na wote ni wala rushwa.. Kuna siku nilisema cdm wakichukua nchi na wao wataiba ka ccm nikashambuliwa hapa haya tumejionea wenyewe.. Kuna msemo unasema 'its better the devil you know'
Hauwezi kutumia issue iliyopo kusema kwamba CHADEMA wataiba kama CCM. CCM inajurikana kama taasisi kwamba inashiriki rasmi kabisa kwenye rushwa, mfano wizi wa fedha za EPA ulibarikiwa na viongozi waandamizi wa CCM kwa ajili ya manufaa yake kisiasa.sitegemi kwa siku za hapa karibuni mpaka kufikia miaka ishirini ijayo kama CHADEMA kinaweza kutumbukia kwenye uchafu wa namna hii. Nitakitetea chama hiki kwa nguvu zangu zote katika hili.
Lakini swala la wanachama wake, kwa hurka zao za kibinaadamu kuweza kushiriki kwenye matendo ya rushwa, sitegemei mtu kushtushwa na hilo, wanaweza na katika hili inawezekana kabisa kabisa kwamba wapo wabunge wa CHADEMA ambao wamekengeuka tayari ni kupokea rushwa.
Ninachokisubiri ni kuona chama kitawachukulia hatua gani. Kwa upande wa CCM najua hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa na katika hili niko tayari kupinga. Na ninapinga kama unabisha tegua.