Katika Dunia hii hakuna nchi hata moja, hakuna chama cha siasa hata kimoja kinachoweza kusema kuwa ndani ya nchi yake au ndani ya chama chake watu wote ni wasafi. Kilicho tofauti ni kuwa nchi na vyama vile vyenye uongozi na vilivyo makini huchukua hatua dhidi ya waovu. CCM, serikali yake na JK wanalaumiwa na wanastahili kulaumiwa siyo kwa kuwa na watu wachafu ndani ya serikali na chama chao bali ni kutokuchukua hatua dhidi ya uchafu, kuukumbatia na kuulinda uchafu, na hivyo kuwa sehemu ya uchafu.
Kama vyama vya upinzani vitaweza kuwawajibisha wabunge wao/viongozi wao kwa kupokea au kutoa rushwa, hapo watakuwa wameonesha umakini mkubwa na kuweka bayana utofauti wao na CCM, utofauti wao ni JK.