Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,331
Ish kweli lakini.......hivi Prof Safari ninani CDM?? msomi huyu kasomea yote na dini ni aalim,, yu wapi huyu??
Pro Abdallaah Safari ni mjumbe wa kamati kuu, baraza kuu na mkutano mkuu na ni mwenyekiti wa kanda ya Pwani yenye mikoa ya Pwani na Dar es salaam na ni miongoni mwa wanasheria wa chama.
Miongoni mwa kesi alizo simamia chama ni pamoja na ile ya ugaidi ya Lwekatare ambayo alishinda na Lwex hana kesi ya ugaidi tena na nyingine ni ile ya Kilewo ya Igunga ambayo alishirikiana na Kibatala nayo walishinda na kukihami chama na kesi mbaya ya ugaidi wa kubambikizwa.
Alikuwa pia wakili wa chama aliye simamia kesi ya uchaguzi mdogo wa Igunga na kwa hila na ghiriba za ccm kama mtakumbuka kama sio rais kuingilia kesi ile Kafumu angevuliwa ubunge kutokana na ushahidi wa wazi ulio shushwa na mwanasheria na wakali huyu msomi.
Ndiye aliye pendekezwa na chama kukiwalisha kwenye bunge maalumu la katiba lililo kwisha Dodoma.
Yupo chamani na anafanya majukumu anayo pangiwa na chama kama ulivyo ona hapo juu.
Kama kuna la ziada uliza.
Asante.