Dr. Slaa, chagua maneno...

Dr. Slaa, chagua maneno...

Hata hizo ruzuku wanazokopesha wanapewa na serikali ya CCM,
 
Wewe si kila siku unawabagua wachaga na kuonyesha chuki ya wazi wazi. Ungekuwa na bubduki wewe si ungekuwa katili kushinda hawa Wa SA? Ni ukaburu tu sio lazima uwe mzungu ndo uwe kaburu sawa wewe popompo?

Nadhani umeshindwa kuelewa hoja.

Tunajadili MFUMO sio tabia za mtu mmoj mmoja wa mitaani.
 
Wewe na maccm mnatofauti gani na makaburu ilhali mnawatenga wachaga kana kwamba si raia halali wa nchi hii? Si nyie kila siku mnakesha hapa kuwatenga wachaga mkijidai nyie ndo watanzania kuliko wachaga?

Una ushahidi wa hiki unachoandika?

Lete post moja tu inayoonyesha mimi kufanya hiki unachonilaumu nami nitawajibika.
 
Kwahiyo unaunga mkono kauli ya Slaa kuwa apartheid ni sawa na mfumo tulio nao?

If yes, je utaunga mkono matumizi ya matendo ya kigaidi kuuondoa huu mfumo uliopo Tanzania?

If no, je una tofauti gani na comments hizo kutoka CNN?
Si afadhali hata makaburu walimfunga Mandela,nyie mna utaratibu wa kuuwa.Chuki mnazozieneza pamoja na kundi flani kujinufaisha na rasilimali za nchi ni sawa tu na apartheid,kuna characteristics nyingi zenye kufanana.
 
Hata hizo ruzuku wanazokopesha wanapewa na serikali ya CCM,

Slaa amepotoka.

Yeye analala kwenye nyumba aliyojenga kutokana na pesa za ruzuku ya serikali, halafu anasema serikali ni sawa na ile ya apartheid ya Afrika Kusini!
 
Ili iweje? Mi nilishasema kwamba chadema ni saccos ya kudandia hoja na kuzigeuza mtaji! Haya sasa mzee kadandia hoja ya ubaguzi wa rangi ndio anajilinganisha nayo,,huku anjua analindwa analala kwenye viyoyozi, anatumia gari la kifahari,helcopter n.k, kisa tu, amekosa urais basi nchi ni kibaguzi! Kweli uzee ni dawa lakini wa huyu mzee ni sumu!

Slaa yuko too desperate na Urais kiasi kwamba anatoa kauli zinazomdhalilisha yeye na chama chake...
 
Ukiendekeza ubaguzi wowote wewe ni Kaburu tu!

Kama watu weusi kutupiwa ndizi na wazungu tu inapigiwa kelele kuna tofauti na udini,ukanda mnaoneza makusudi?

Nyie ni makaburu tu!
Mbona slaa na mbowe wanambagua zito kwahiyo ni makaburu?
 
Jitafakari na ujipime kwa hiki ulichokiandika maneno ya Dr. Slaa yapo sahihi kabisa naomba tujikumbushe yafuatayo na tuone kama hayashabihiani na utawala dhalimu wa MAKABURU.

1.Viongozi karibu wote wa CHADEMA na wabunge wao wameisha shitakiwa na kuwekwa mahabusu katika vipindi tofauti kwa makosa ya kusingiziwa(kutengenezwa) - Hili pia lilitumika na Makaburu

2. Mikutano mingi ya chama Hiki (CDM) imekuwa ikifanyiwa vitu vya ajabu vikiongozwa na Polisi na wafuasi wa CCM Ref. Ndago, Arusha, Morogolo na sasa Kigoma

3. Vitisho utumika na hata kusababisha mauaji kwa raia ili waogope kushiriki mikutano ya kisiasa ya CDM na mbinu hii ilitumika pia na makaburu kwani walikuwa wanakamata watu na pia kuvuruga mikutano hiyo na kutumia siraha za moto na kuua.

Je, unadhani ilikuwa ni sahihi kwa Mandela kutumia njia za "kigaidi" kuuondoa mfuko wa apartheid?

Je, unadhani ni sahihi kwa Slaa kutumia njia za kigaidi kuuondoa CCM madarakani?

Twende kwa hoja...
 
Mambo mengine yapo wazi sana slaa hajaanza leo ulaghai na kuropoka amekuwa akilaghai tangu akiwa kwenye kazi yake ile aliyofukuzwa nalo ni miongoni mwa makosa yaliyofanya afukuzwe kwahiyo siyo mageni anayofanya mzoeeni.
 
Si afadhali hata makaburu walimfunga Mandela,nyie mna utaratibu wa kuuwa.Chuki mnazozieneza pamoja na kundi flani kujinufaisha na rasilimali za nchi ni sawa tu na apartheid,kuna characteristics nyingi zenye kufanana.
Haya yote unayosema yanafanywa na viongozi wa chadema yuko wapi wangwe na grace tumia akili vizuri.
 
Haya yote unayosema yanafanywa na viongozi wa chadema yuko wapi wangwe na grace tumia akili vizuri.
Ungekuwa unatumia akili ungetumika kwa style hiyo?Wangwe alikuwa mwiba kwa mafisadi kwasana,sema alikuwa anakula kotekote,mafisadi ndo walimwua baada ya kuona mbali na kumtumia dhidi ya chadema,bado alikuwa mwiba kwenye dili zao,alikuwa akifanya vikao vya siri na kina RA kwenye vyumba vya hoteli za kimataifa....fuatilia hoja aliyokuwa anaipeleka bungeni na Sita alipomwambia awe makini atakapokuwa akirudi bungeni(kuhusu Barrick nk).Wengine wakitumia akili wewe unatumika kama dodoki.
 
Dr Slaa alipokuwa ccm alikuwa anafanya vitu productive sana. Alienda chadema sio kwa mapenzi yake bali chuki tu na kutoheshimu democrasia ndani ya ccm.
 
Wewe si kila siku unawabagua wachaga na kuonyesha chuki ya wazi wazi. Ungekuwa na bubduki wewe si ungekuwa katili kushinda hawa Wa SA? Ni ukaburu tu sio lazima uwe mzungu ndo uwe kaburu sawa wewe popompo?
Nchi hii inawagojwa wengi kweli hayo unayoongea unaushahidi nayo? Au ni ile dhana ya ulaghai kama mzee wenu.
 
Ungekuwa unatumia akili ungetumika kwa style hiyo?Wangwe alikuwa mwiba kwa mafisadi kwasana,sema alikuwa anakula kotekote,mafisadi ndo walimwua baada ya kuona mbali na kumtumia dhidi ya chadema,bado alikuwa mwiba kwenye dili zao,alikuwa akifanya vikao vya siri na kina RA kwenye vyumba vya hoteli za kimataifa....fuatilia hoja aliyokuwa anaipeleka bungeni na Sita alipomwambia awe makini atakapokuwa akirudi bungeni(kuhusu Barrick nk).Wengine wakitumia akili wewe unatumika kama dodoki.
Akili yako umeivalia kwenye viatu haifanyi kazi kabisa kilichomtoa wangwe duniani ni uenyekiti wa chama chako zingine porojo za kilaghai kama mlivyozoea.
 
Si afadhali hata makaburu walimfunga Mandela,nyie mna utaratibu wa kuuwa.Chuki mnazozieneza pamoja na kundi flani kujinufaisha na rasilimali za nchi ni sawa tu na apartheid,kuna characteristics nyingi zenye kufanana.

Kwa msingi wa kauli yako hii na kwa kumbukumbu ya kauli yako uliyotoa siku za nyuma kuwa ni bora damu imwagike ili Chadema iingie madarakani, naomba unijibu maswali haya mawili.

Je, unadhani ilikuwa ni sahihi kwa Mandela kutumia njia za "kigaidi" kuuondoa mfuko wa apartheid?

Je, unadhani ni sahihi kwa Slaa kutumia njia za kigaidi kuuondoa CCM madarakani?
 
Dr Slaa alipokuwa ccm alikuwa anafanya vitu productive sana. Alienda chadema sio kwa mapenzi yake bali chuki tu na kutoheshimu democrasia ndani ya ccm.

Survival of the fittest. Slaa was not fit, he couldnt survive in CCM.
 
Ungekuwa unatumia akili ungetumika kwa style hiyo?Wangwe alikuwa mwiba kwa mafisadi kwasana,sema alikuwa anakula kotekote,mafisadi ndo walimwua baada ya kuona mbali na kumtumia dhidi ya chadema,bado alikuwa mwiba kwenye dili zao,alikuwa akifanya vikao vya siri na kina RA kwenye vyumba vya hoteli za kimataifa....fuatilia hoja aliyokuwa anaipeleka bungeni na Sita alipomwambia awe makini atakapokuwa akirudi bungeni(kuhusu Barrick nk).Wengine wakitumia akili wewe unatumika kama dodoki.

Kwahiyo kuongea na Rostam Aziz ndio kosa la Wangwe!!!

Mushi siku hizi sijui nini kimekukuta...
 
ZeMarcopolo,

Inawezekana ID imevamiwa na 'zuzu' la mtaani, maana haingii akilini kuwa unaweza kuandika hoja dhaifu kiasi hiki, imajaa contradiction.

Tuanze:Msingi wa hoja yako ni, 'Dr. Slaa kusema kuwa matendo ya serikali ya CCM ni sawa na mfumo wa apartheid wa makaburu wa Afrika ya Kusini.'

Tunajua Apartheid - ni mfumo wa kibaguzi kati ya mwa mwanadamu mmoja na mwingine kutokana na vigezo anavyoweka yeye 'mgabuzi', mfano Makaburi wa Afrika ya Kusini waliwabagua watu wale wote ambao hawakuwa na rangi nyeupe - yaani wazungu. Hapa Wahindi na Weusi (Waafrika) waliwekwa daraja la chini, na hivyo hawakuwa na haki sawa na wazungu kwa sababu tu ya rangi zao. Iwe elimu, matibabu, usafiri, na hata kupiga kura, Makaburu wa Afrika ya Kusini waliwapora haki watu waliowaona ni daraja la chini.

Chama cha Mapinduzi - kama kilivyokuwa TANU - kiliundwa kwa misingi ya kutombagua binadamu mwenzio kwa namna yoyote ile, na ndio zamani (kwa waliokula chumvi) tulikuwa tunaimba binadamu wote ni sawa. Na tukaenda mbele zaidi kwa kuitana NDUGU fulani. Hali ikoje sasa?

Kwanza tuna waheshimiwa! (ubaguzi). Kama mtu si mheshimiwa anakuwa nani? Na ana haki sawa na Mheshimiwa? Jibu- hapana. Kwa sasa tuna mfumo ambao watu fulani wana haki ya kutibiwa India, Afrika ya Kusini na kwingineko ambako wanaona 'kunawafaa' kwa fedha ya umma, lakini wengine wanapiga miayo kwenye Zahati ambao hata Asprin hakuna!. (ubaguzi)

Kwa sasa, kuna mfumo ambao watu fulani wakitaka kufanya medical check-up wanapanda ndege, lakini wakina mama wanajifungulia sakafuni! (Ubaguzi)

Kwa sasa tuna mfumo amabo baadhi ya watoto wanapitiwa na vibasi asubuhi wanapelekwa shule za St. St ... wakati wengine watembea 4km kwenda shule ambayo ni mbavu za mbwa na wanakalia mawe, hapo hujaongelea walimu. (ubaguzi).

Zamani mtoto wa mama ntilie alikuwa anasoma shule moja - darasa moja na mtoto wa rais. (pitia orodha kwenye shule mfano Weruweru, Pugu, Ilboru, Umbwe Secondary, n.k. utakuta majina ya watoto wa viongozi wa juu kabisa enzi hizo!

Zamani kulikuwa na mfumo ambao vyombo vya dola villikuwa vinamlinda kila raia na mali yake - mwenye kipato cha juu au cha chini, lakini sasa vyombo vya dola (i.e. polisi) vimekuwa ni kero kwa walala hoi (Soweto)

Mfumo wa sasa ambao umejaa kasoro unawanyima raia haki ya msingi ya kupiga kura (pitia Hansard za bunge). Kule Zanzibar Sheha anaamua nani ana haki ya kupiga kura na nani hana haki, na kwa kiasi kikubwa maamuzi yake yanaegemea kwenye itikadi za siasa. (ukaburu)

Mtu anapofananisha mfumo wa sasa na Apartheid ni kwa sababu haki za msingi zinatolewa kwa kimatabaka. Mzee Mandela alipinga matabaka, TANU ilipinga matabaka na hata CCM (ya Mwl Nyerere) kiliyapinga matabaka.

Kule Mara kuna watu wako korokoroni kwa sababu tu ya matabaka ya kisiasa. Kimatendo, mfumo wa nchi hii kwa sasa umejaa ubaguzi. Kwanini wagonjwa walale chini sakafuni, wakati wengine wanapelekwa India?
 
Una ushahidi wa hiki unachoandika?

Lete post moja tu inayoonyesha mimi kufanya hiki unachonilaumu nami nitawajibika.

Kuuona tu mtu ambaye mnafata itikadi moja anafanya kitu amabacho si cha kiungwana au yumkini naweza kusema kulea tabia hiyo katika kundi au chama hata kama wewe hujafanya moja kwa moja ni kuonyesha kuunga mkono jambo hilo. Unaweza kutuambia hapa kuwa watu mithili ya faizafoxy, ritz, chamviga, au kiujumla lumumba buku 7 guys huwa huwaoni wakifanya kuwatenga na kueabagua wachaga? Hujawaona wakitukana dini specificaly katoliki hapa? Mbona hujawai hata kuwakemea hata siku moja? Hiyo ni kuonyesha kwa njia moja au nyingine unawaunga mkono. Sipendi unafiki kama ulishawakanya lete hiyo posti hapa ili nikuondoe katika listi ya makaburu.
 
Back
Top Bottom