Dr. Slaa, chagua maneno...

Dr. Slaa, chagua maneno...

Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi wakati anajiuzuru alisema kuwa ameshirikiana na Slaa kufanya mikakati mbalimbali mizuri na mibaya kwa taifa.

Pengine Slaa anaamini kuwa nchi yetu ina mfumo sawa na Afrika Kusini ya apartheid na anaamini kwamba matumizi ya kigaidi kuuondoa huu mfumo ni halali!!!

Muua tembo kahutubia watu 31 Njombe ahahaha!
 
“Sasa unaachaje kumsikiliza huyu na ukamsikiliza zaidi mtu ambaye hana sifa za kimageuzi katika ngazi ya kitaifa? Wanaozua tuhuma dhidi ya wenzao hawana hata miaka mitano ndani ya chama?
“Labda nikupe mfano mzuri. Hivi unategemea leo, CCM kwa mfano, eti akina Richard Tambwe Hizza, waanzishe mkakati wa kumng’oa kwenye chama mtu kama Kingunge Ngombale Mwiru kwa madai ni msaliti? Haya mambo yako CHADEMA tu,” alisema mwanasiasa huyo

Dr slaa isn't a medical dr but a phd dr
 
Div 5 ingine ya Mulugo hii hapa!
Dr Bilali awe wa kwanza kujiondoa madarakani kwa ukikongwe wake!

Tatizo sio umri kama namba ya miaka, tatizo ni umri unapoleta mabadiliko ya haraka ya uwezo wa kufikiri na kuchanganua mambo.

Wapo watu wanafikiri vizuri at the age of 80, wengine uwezo wao unafifia at the age of 60.

Slaa anapaswa kujipima...
 
Umezungumzia ubaguzi kwa mtazamo finyu sana. Ubaguzi unaofanywa na CCM ni zaidi hata na uliofanywa na makaburu, kwani makuburu hawakuwa waafrika wenzetu lakini CCM ni watanzania wenzetu. Dr.Slaa hata hivyo nafikiri alitumia maneno mepesi zaidi kuliko na ambavyo alipaswa kusema kuonesha ubaguzi mkubwa unaofanywa na tuliofikiri ni wenzetu katika kuikomboa nchi na kuweka usawa kwa raia wote. Kaa chini utafakari upya dhana ya ubaguzi.
 
Umechambua vizuri kiasi kauli ya DR. Slaa, lakini unachokisahau ni kuwa
1. CCM huruhusu wananchi kuchagua mgombea wamtakae lakini atakayetangazwa ni yule wanaomtaka mfumo wa chama.
2. CCM hii hii ndio imekuwa ikinuka rushwa katika chaguzi zote, huku wengine wakibashiri kuwa hiyo ni takrima. Je penye rushwa pana haki?
3. CCM hii hii ndiyo inayokataa kufanya marekebisho ya daftari la wapiga kura ktk chaguzi ndogondogo, sababu hazijawahi kutolewa zikashika uwezo wa kufikiri wa watanzania.
4. CCM hii hii ndio imekuwa ikitumia wajumbe wa nyumba kumi (Mabalozi) wake kununua kadi za wapiga kura
5. CCM hii hii ndio imekuwa ikikamata wale wote wanaoonekana kuibana katika chaguzi na kuwafanyia usumbufu wa hapa na pale ikiwepo ofisi za chama kugeuzi lupango katika baadhi ya chaguzi
6. CCM hii hii ndio imekuwa ikishindwa kuwawajibisha viongozi wake hata pale wanaposhindwa na kwenda tofauti na misingi si ya chama pekee bali hata wanapovunja sheria za nchi. Vigogo wamekuwa mafisadi wa kutupa, Mikataba feki, wabakaji, waizi na hata kufanya biashara haramu n.k lakini hatujawahi shuhudia hatua dhidi yao.
7. CCM hii hii ndio viongozi wake wamekuwa baadhi ya koo toka nchi ipate uhuru mpaka sasa.
Kwa kuwa kila mtu ana uwezo wake binafsi kufikiria, kuona na utashi hivyo anaweza kuendelea kuongeza / kupunguza awezavyo
 
Jana nilikuwa kwenye basi natoka Dodoma kuja Dar, kuna akina mama walikuwa wanakiri kuwa Slaa mtu mbaya sana kwa kauli zake tofauti na kazi aliyoitumikia awali.

Sasa nimeanza kuamini huyu Mzee amechanganyikiwa.
Ukiona umeanza kufikia kiwango hicho cha kukosa break ya ulimi basi ujue na break za maumbile mengine zimekata.

Suluhusho ni kustaafu tu ili usiendelee kujikojolea hadharani.
Nyerere aliwahi kunukuliwa kwa kusema kuwa "hatumchukii kaburu kwa rangi yake bali kwa matendo yake ya kikatili kwa wanadamu" Sioni kibaya alichokisema Dr Slaa zaidi ya kukubaliana nae 100% Chini ya CCM wananchi wananyang'anywa ardhi nzuri yenye madini na kupewa wanyonyaji, Chini ya CCM madaktari wamepigwa wameng'olewa meno na kucha, Chini ya CCM wananchi wamedhuriwa kwa kunyweshwa maji yenye sumu kutoka migodini, Chini ya CCM wachagga wanabaguliwa live! Chini ya CCM udini metamalaki, Chini ya CCM wakulima na wafugaji wanauana, Chini ya CCM wanafunzi wameuawa kifikra, Chini ya CCM wananchi wengi wamepoteza maisha kwa kukosa huduma muhimu za afya, Chini ya CCM utajiri wetu unakwapuluwa kwa kwenda mbele... Chini ya CCM Maisha yanazidi kuwa magumu Tembo wanaangamizwa Twiga wanakunjiwa kwenye ndege... Chini ya CCM wengi wameuawa wakiwemo waandishi wa habari kikatili... CCM = Apartheid era...
 
Sijamkataza Slaa kutoa maoni yake.

Hata hivyo Slaa kama kiongozi wa chama cha siasa, maoni yake hayabaki kuwa maoni tu hewani. Yanaweza kuwa na impact kwenye maisha ya watu.

Nakumbuka hata Mzee Mtei alipotoa kauli ya kibaguzi mlisema ana haki ya kutoa maoni yake. Well, hatukatazi mtu kuwa na maoni yake ndio maana wako huru na hiyo pia ni tofauti kati ya apartheid na nchi yetu. Lakini kila anayetoa maoni inabidi kupima kile anachosema kina madhara gani kwa jamii.

Kauli ya Slaa haiendani na nafasi yake kwa jamii...

Ua too foolishness
 
Umechambua vizuri kiasi kauli ya DR. Slaa, lakini unachokisahau ni kuwa
1. CCM huruhusu wananchi kuchagua mgombea wamtakae lakini atakayetangazwa ni yule wanaomtaka mfumo wa chama.
2. CCM hii hii ndio imekuwa ikinuka rushwa katika chaguzi zote, huku wengine wakibashiri kuwa hiyo ni takrima. Je penye rushwa pana haki?
3. CCM hii hii ndiyo inayokataa kufanya marekebisho ya daftari la wapiga kura ktk chaguzi ndogondogo, sababu hazijawahi kutolewa zikashika uwezo wa kufikiri wa watanzania.
4. CCM hii hii ndio imekuwa ikitumia wajumbe wa nyumba kumi (Mabalozi) wake kununua kadi za wapiga kura
5. CCM hii hii ndio imekuwa ikikamata wale wote wanaoonekana kuibana katika chaguzi na kuwafanyia usumbufu wa hapa na pale ikiwepo ofisi za chama kugeuzi lupango katika baadhi ya chaguzi
6. CCM hii hii ndio imekuwa ikishindwa kuwawajibisha viongozi wake hata pale wanaposhindwa na kwenda tofauti na misingi si ya chama pekee bali hata wanapovunja sheria za nchi. Vigogo wamekuwa mafisadi wa kutupa, Mikataba feki, wabakaji, waizi na hata kufanya biashara haramu n.k lakini hatujawahi shuhudia hatua dhidi yao.
7. CCM hii hii ndio viongozi wake wamekuwa baadhi ya koo toka nchi ipate uhuru mpaka sasa.
Kwa kuwa kila mtu ana uwezo wake binafsi kufikiria, kuona na utashi hivyo anaweza kuendelea kuongeza / kupunguza awezavyo

Can this equate to apartheid?
 
Sijamkataza Slaa kutoa maoni yake.

Hata hivyo Slaa kama kiongozi wa chama cha siasa, maoni yake hayabaki kuwa maoni tu hewani. Yanaweza kuwa na impact kwenye maisha ya watu.

Nakumbuka hata Mzee Mtei alipotoa kauli ya kibaguzi mlisema ana haki ya kutoa maoni yake. Well, hatukatazi mtu kuwa na maoni yake ndio maana wako huru na hiyo pia ni tofauti kati ya apartheid na nchi yetu. Lakini kila anayetoa maoni inabidi kupima kile anachosema kina madhara gani kwa jamii.

Kauli ya Slaa haiendani na nafasi yake kwa jamii...

Wewe na maccm mnatofauti gani na makaburu ilhali mnawatenga wachaga kana kwamba si raia halali wa nchi hii? Si nyie kila siku mnakesha hapa kuwatenga wachaga mkijidai nyie ndo watanzania kuliko wachaga?
 
Nyerere aliwahi kunukuliwa kwa kusema kuwa "hatumchukii kaburu kwa rangi yake bali kwa matendo yake ya kikatili kwa wanadamu" Sioni kibaya alichokisema Dr Slaa zaidi ya kukubaliana nae 100% Chini ya CCM wananchi wananyang'anywa ardhi nzuri yenye madini na kupewa wanyonyaji, Chini ya CCM madaktari wamepigwa wameng'olewa meno na kucha, Chini ya CCM wananchi wamedhuriwa kwa kunyweshwa maji yenye sumu kutoka migodini, Chini ya CCM wachagga wanabaguliwa live! Chini ya CCM udini metamalaki, Chini ya CCM wakulima na wafugaji wanauana, Chini ya CCM wanafunzi wameuawa kifikra, Chini ya CCM wananchi wengi wamepoteza maisha kwa kukosa huduma muhimu za afya, Chini ya CCM utajiri wetu unakwapuluwa kwa kwenda mbele... Chini ya CCM Maisha yanazidi kuwa magumu Tembo wanaangamizwa Twiga wanakunjiwa kwenye ndege... Chini ya CCM wengi wameuawa wakiwemo waandishi wa habari kikatili... CCM = Apartheid era...

Je, unafikiri matumizi ya vitendo vya kigaidi kuondoa mfumo wa apartheid Afrika Kusini ilikuwa sahihi?
 
Je, unafikiri matumizi ya vitendo vya kigaidi kuondoa mfumo wa apartheid Afrika Kusini ilikuwa sahihi?

Maccm ni makaburu tu. Udini? Kutenga watu kimakabila wachaga for instance? Ni makaburu tu
 
Je, unafikiri matumizi ya vitendo vya kigaidi kuondoa mfumo wa apartheid Afrika Kusini ilikuwa sahihi?

Maccm ni makaburu tu utaki unaacha. Ni sawa tu na yale makaburu ya SA hayana tofauti. Mabaguzi yamejaa chuki na wivu kwa makabila flani flan ni makaburu tu
 
Mhhh, kawaambie Mwangosi family au Ulimboka. Nafikiri Mwangosi (RIP) angelichagua kuwa Mandela. Wee subiri siku JEMBE Msangi akukamate huna Panadol ndiyo utakoma. Na hapo kama atakuwepo Rama Mgogo, weeee.....

mwangosi.jpg
ulimboka.jpg
 
Kwahiyo unaunga mkono kauli ya Slaa kuwa apartheid ni sawa na mfumo tulio nao?

If yes, je utaunga mkono matumizi ya matendo ya kigaidi kuuondoa huu mfumo uliopo Tanzania?

If no, je una tofauti gani na comments hizo kutoka CNN?

Maccm ni makaburu tu. Mwache Mandela mwache apumzike usimtumie kwenye masiasa maji taka yenu haya. Kaburu wewe
 
Weka picha tuone:

Ili iweje? Mi nilishasema kwamba chadema ni saccos ya kudandia hoja na kuzigeuza mtaji! Haya sasa mzee kadandia hoja ya ubaguzi wa rangi ndio anajilinganisha nayo,,huku anjua analindwa analala kwenye viyoyozi, anatumia gari la kifahari,helcopter n.k, kisa tu, amekosa urais basi nchi ni kibaguzi! Kweli uzee ni dawa lakini wa huyu mzee ni sumu!
 
Ze marcopolo au ze layland tena ya 1700:
Anyway, nimeshindwa kuendelea kusoma uchafu wako.
 
Dr. Slaa ni mwanasiasa mlaghai.

Siku za hizi karibuni Dr. Slaa amekuwa akisema maneno bila kupima maana na ujumbe unaobebwa na maneno hayo.

Matokeo yake, Dr. Slaa amekuwa sababu ya mitafaruku kutokana na kauli zake.

Hali hiyo tuliishuhudia hata hapa JF ambapo sasa hivi Dr. Slaa anapaogopa kama ukoma kutokana na wadau kuwa wakali kwa kauli zake.

Kiujumla kauli za Dr. Slaa huwa zina madhumuni ya kuwalaghai wale watakaozisikia. Hata hivyo Slaa anapaswa kupima kiasi cha ulaghai anachokitumia kwa sababu sasa ameanza kupitiliza.

Akitoa salam za rambirambi kwa kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini na Kiongozi wa ANC Mzee Nelson Mandela, Dr. Slaa ametamka kuwa matendo ya serikali ya CCM ni sawa na mfumo wa apartheid wa makaburu wa Afrika ya Kusini.

Kauli hii iliyolenga kulaghai watu (kwa sababu Slaa anajua kuwa anachosema sio ukweli au more correctly ni uongo) ina madhara makubwa kwa namna mbili.

Kwanza ni kupunguza uzito wa mateso waliyopata watu weusi wa Afrika ya Kusini, ambao hata kupiga kura walikuwa hawaruhusiwi. Slaa anaposema kuwa maisha ya watu wa Afrika ya Kusini kipindi cha ubaguzi wa rangi ni sawa na maisha ya watanzania wa leo chini ya serikali ya CCM anamaanisha kwamba watu weusi walikuwa wanalalamika bure bila kuwa na sababu ya msingi. Hapohapo anasahau kuwa yeye, Slaa, hajafungwa kama Mandela na wanasiasa wengine wa Afrika Kusini. Slaa anapata ulinzi wa polisi, anagombea Urais na kufanya kampeni kwa uhuru, lakini kwa vile tu ameshindwa kupata kura za kumfanya awe Rais, basi anaona hiyo ni kero sawa na apartheid!!!

Katikia hili Slaa, pengine bila kujua, anajiunga na wale wanaomuweka Mandela kwenye kundi la magaidi wasiostahili heshima yoyote. Katika mtandao wa CNN kuna wachangiaji wengi wenye mrengo huu wa Dr. Slaa. Mifano yake ni hii hapa chini.

JimmyBoston • 2 days ago
Mandela is dead. What scares me the most is the people on this board, left leaning liberals, who find the murder of innocent people, going about their daily business, as acceptable to promote a Socialist cause. It sickens me.

Confucius Say • 2 days ago

Whatever Mandela's reasonings, and they are questionable, his methods were criminal. He gave orders to plant I.E.D's and they killed innocent people. Women and children. Over 80% black. How can we be so blind as to forget that? Whatever the cause the means were beyond wrong and to celebrate this man is a shame. To simply gloss over or completely ignore this is atrocious. Church Street Bombings, look it up people. Stop drinking the Kool Aid and do some research.

Kwa mifano zaidi ya comments zinazofanana na hiyo na ya Dr. Slaa soma hapa http://edition.cnn.com/2013/12/05/world/africa/nelson-mandela-
humor/index.html#disqus_thread

Wenye maoni ya namna hii, yanayofanana na kile alichosema Dr. Slaa, ni watu ambao wanadhani mfumo wa ubaguzi wa rangi (apartheid) unaweza kufananishwa na maisha ya kawaida ya mtanzania wa leo, kama jinsi alivyofananisha Dr. Slaa. Pengine tunaweza kumvumilia hawa wamarekani walioandika hivyo kwenye mtandao wa CNN kwa vile hata ukiwaonyesha ramani ya dunia wanaweza kupata shida kuonyesha Afrika ya Kusini iko wapi kwenye ramani hiyo. Tatizo ni pale mwafrika mtanzania mwanasiasa wa ngazi ya kitaifa anapofananisha ubaguzi wa rangi wa Afrika ya Kusini na maisha ya mtanzania wa leo!!!

Wamarekani hawa wanafananisha mfumo wa apartheid na changamoto wanazokutana nazo kila siku kwenye maisha yao ya Marekani ya leo. Slaa anafananisha mfumo wa apartheid na changamoto za kisiasa anazokutana nazo katika maisha yake ya Tanzania ya leo. Slaa na wachangiaji hawa wote WAMEPOTOKA...

Tatizo la pili katika kauli ya Dr. Slaa ni kwamba inawasafisha makaburu mbele ya macho ya vijana wa leo. Unapomwambia kijana wa kizazi cha sasa kuwa mfumo wa ubaguzi wa rangi, apartheid, ulikuwa ni sawa na jinsi CCM inavyoongoza Tanzania, unampa ujumbe kuwa apartheid was not a problem. Mbaya zaidi ni kwamba unatoa ujumbe, pengine bila kujijua, kuwa apartheid ilikubaliwa na watu wengi.

CCM imekubaliwa na watanzania wengi kwa njia halali ya kidemokrasia ambapo kila aliyekidhi vigezo vya kikatiba kupiga kura aliruhusiwa kupiga kura.Vigezo vya kikatiba vya kupiga kura Tanzania havikutenga walio wengi ili wasishiriki kwenye kuchagua vionngozi. Vilevile, wale wote waliokidhi vigezo vya kugombea, akiwemo Dr. Slaa, waliruhusiwa kugombea. Katika Afrika Kusini ya apartheid, hali haikuwa hivi.

Pamoja na kwamba Slaa amebobea kwenye siasa za kilaghai, lakini sasa amefikia hatua anapaswa kuchagua maneno ya kusema. Slaa asiwe TOO DESPERATE kwenye kutaka kuwafanya watanzania waichukie CCM kiasi cha kutoa kauli za kukejeli harakati muhimu kama alizofanya Mandela za kupiga vita ubaguzi wa rangi.

Dr. Slaa anapaswa kujipima na kuomba radhi kwa kauli hii aliyoitoa. Vilevile anapaswa kuchagua maneno ya kusema katika siku zijazo...

Tafakuri: Katika taarifa yake ya kujiuzuru, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi, alikiri kushirikiana na Dr. Slaa kufanya mikakati mizuri na mibaya kwa nchi yetu. Je, Slaa amekuwa akihalalisha mikakati hiyo mibaya kwa kufananisha na jinsi ANC ilivyolazimika kutumia mikakati ya namna hiyo kupiga vita apartheid?

Rest in Eternal Peace Nelson Mandela...

Jitafakari na ujipime kwa hiki ulichokiandika maneno ya Dr. Slaa yapo sahihi kabisa naomba tujikumbushe yafuatayo na tuone kama hayashabihiani na utawala dhalimu wa MAKABURU.

1.Viongozi karibu wote wa CHADEMA na wabunge wao wameisha shitakiwa na kuwekwa mahabusu katika vipindi tofauti kwa makosa ya kusingiziwa(kutengenezwa) - Hili pia lilitumika na Makaburu

2. Mikutano mingi ya chama Hiki (CDM) imekuwa ikifanyiwa vitu vya ajabu vikiongozwa na Polisi na wafuasi wa CCM Ref. Ndago, Arusha, Morogolo na sasa Kigoma

3. Vitisho utumika na hata kusababisha mauaji kwa raia ili waogope kushiriki mikutano ya kisiasa ya CDM na mbinu hii ilitumika pia na makaburu kwani walikuwa wanakamata watu na pia kuvuruga mikutano hiyo na kutumia siraha za moto na kuua.

Mazishi ya mwangosi. mkejpg.jpg

Huyu mama anamlilia Mme wake Mwangosi aliyeuawa kinyama, hiki pia hakipo mbali sana na yaliyofanywa na Makaburu kwani wanawake wengi sana walilia kama mama huyu
 
Ili iweje? Mi nilishasema kwamba chadema ni saccos ya kudandia hoja na kuzigeuza mtaji! Haya sasa mzee kadandia hoja ya ubaguzi wa rangi ndio anajilinganisha nayo,,huku anjua analindwa analala kwenye viyoyozi, anatumia gari la kifahari,helcopter n.k, kisa tu, amekosa urais basi nchi ni kibaguzi! Kweli uzee ni dawa lakini wa huyu mzee ni sumu!

Wewe si kila siku unawabagua wachaga na kuonyesha chuki ya wazi wazi. Ungekuwa na bubduki wewe si ungekuwa katili kushinda hawa Wa SA? Ni ukaburu tu sio lazima uwe mzungu ndo uwe kaburu sawa wewe popompo?
 
Back
Top Bottom