Mama Obama
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 1,621
- 1,087
Leo tarehe 06/02/2018, Dr. Wilbroad Slaa anaongea na Clous Tv, hakika namwelewa sana huyu mzee.
Kuna kitu kimoja amesema huyu mzee kuwa aliwahi sema kuwa aliamua kuacha siasa za vyama vingi ambazo ni siasa za uvuguvugu. Hivyo yeye hajawahi tangaza kuacha siasa.
Anakili kuwa yeye kwake siasa ni maisha hivyo kumwambia ameacha siasa ni sawa na kusema aachane na maisha. Kimsingi anadai kuwa siasa ni maji, siasa ni elimu, siasa ni chakula, siasa ni biashara na kila kitu unachofanya.
Kwa kauli yake ya kuwa ANAACHANA NA SIASA ZA VYAMA VINGI (opposition parties) kwangu naichukulia hii kauli kama ni kauli ya kuomba CCM, wapime kwa namna yeyote kama anafaa kuwa mtu mhimu kuongoza chama na nchi kwa huko mbeleni.
Kusema kweli upo uwezekano kama yeye binafsi atapenda kujijenga katika CCM, msije shangaa siku moja akawa rais wa jamhuri kupitia CCM.
Hii ndoto yangu ipo wenda ikaja timia na kila mtu atabaki mdomo wazi.
Wenye mtazamo wenu, naomba mawazo yenu.
Kama WATANZANIA wanaohitaji mabadiliko yaendelee, Rais Magufuli Akimaliza Wakati wake, Dr Slaa ashike usukani. Tanzania itaendelea. Sioni mwingine wakuendeleza mufumo wa Rais Magufuli ni Dr Slaa tu. Hapa nakuunga mkono kabisa.