Dr. Slaa(Balozi): Siendi kutekeleza Sera ya CCM bali Sera ya Taifa. Aongelea sakata zima la Lowassa kuingizwa CHADEMA

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Habari waungwana,

Leo anahojiwa balozi mteule, Dr. Wilbroad Slaa kuhusu maisha yake ya kisiasa, kikanisa hadi sasa balozi mteule, kuwa nami nikujuze..
====



Slaa anasema gari lake limeshawahi kukamatwa na cocaine tani tano mwaka 1991 na lilikaa polisi miaka 8 ila uzuri alilikodisha kwa kampuni hivyo yeye hakuusishwa. Baada ya hapo aliingia kwenye siasa na anaelezea nafasi alizoshika CHADEMA.

Anasema baada ya hapo watu wanasema ameondoka kwenye siasa, anasema Serena Hotel alisema anaachana na siasa za vyama vingi na active politics, na akaahidi kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa na amejiuzulu siasa za vyama.

Amesema, Serena alisema mtu akihitaji jambo la kupigiwa kelele lenye maslahi atalipigia kelele.

Anasema yeye hakusepa wala kufukuzwa kanisa katoliki bali alifata taratibu za kutoka na alipata decree ya kutoka mwaka 1998 ndio maana yeye hana tatizo na kanisa katoliki. Ndio maana hata lilipokuja suala la ndoa, anasema ndoa haifungwi na padri bali ndoa inafungwa na wahusika wawili, padri ni ofisa.

Amesema February 2016 alifunga ndoa ya validation kwenye kanisa katoliki, anasema yeye amekuja nchini kwa sababu ni mwenyekiti wa CCBRT na sio mambo ya ubalozi. Amesema nchini kuna mabadiliko mengi na wao CCBRT wameguswa, ilitakiwa kujiandikisha upya na waliandikiwa kuwa wanaweza kufutiwa usajili, sheria iliyotungwa mwaka 2002 na kufanyiwa marekebisho 2015. Hivyo kilichomleta ni mchakato wa kuhamisha usajili wa shirika.

Slaa anasema Canada ni nchi ambayo ni kama haina mwenyewe, miaka 500 iliyopita watu wengi walihamia, wao wanaona popote ulipotoka, ukifika Canada wewe ni mcanada. Anasema Canada, kazi ni maisha na sio msemo kama Tanzania na ndio maana ya maendeleo. Anatolea mfano watu wanavyofika ofisini na kufikia kusoma magazeti karibu saa nzima au kunywa chai.

Anasema nchi ni tajiri na watu pia matajiri na ni kwa sababu wanafanya kazi, pia huduma zote ziko standard.

Slaa: Balozi siendi kutekeleza sera ya CCM, naenda kutekeleza sera ya taifa. Mambo yakishaingia bungeni na kupitishwa hayawi tena ya CCM, yanakuwa ya taifa. Anatolea mfano Karatu walivyotekeleza sera ya Taifa kwa namna ya CHADEMA kwa sababu walikuwa na madiwani theluthi mbili.

Slaa anatolea mfano walivyomsomea Mkapa sera ya zahanati kila kijiji Karatu na yeye alivyofika Arusha akaifanya sera ya taifa kwa zahati kila kijiji nchi nzima. Kuhusu kauli ya Mnyeti kuhusu watendaji wasiounga mkono serikali, amesema itakuwa ni makosa kwani analazimisha.

Kuhusu kadi za CHADEMA na CCM, anasema hakurudisha kadi ya CCM na sheria inasema uanachama unajulikana kwa kadi lakini pia kuonekana kwenye jukwaa la chama kingine unakuwa sio mwanachama. CHADEMA alisema ameondoka lakini kadi ni kumbukumbu yake na ameilipia hivyo ni haki yake.

Amesema mwelekeo wa siasa nchini haumfurahishi, anasema baada ya Uhuru kulikuwa na vyama vingi, baadae vikaanza kufa vyenyewe kwa sababu vilikatisha tamaa wananchi na baadae vikaondoka kisheria.

Anasema anasikitika kwa sababu ameshiriki kujenga upinzani nchini na haoni chama chenye sera zilizonyooka. Mikakati ya utekelezaji kwa serikali iliyoko madarakani duniani kote ni kipindi cha kutoa ahadi na sera sera mbadala na hakuna mtu anaesema wameiba au wamenyang'anya kwani sera ikitoka hadharani ni za nchi nzima.

Kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, amesema kama binadamu, hakuna anayependa binadamu mwenzake aumizwe lakini matukio ya kuumiza yanatokea nchini kwa watu wengi sana na yeye sio chombo cha dola kunyoosha mkono kwa mtu, amesema mwananchi wa kawaida anaweza kuwa mtu anaemuhisia lakini yeye ni msomi, kama ana taarifa anaenda kuripoti.

Anasema alipotaja list of shame, alipata maadui na alitishwa lakini wakati huo alikuwa na mtandao mkubwa wa chama wa kumlinda lakini leo hana na aliondoka kwenye chama hana mtandao na waliokuwa wanamlinda walimgeuka kuwa maadui zake hivyo akahamia Canada kwani inajulikana duniani kwa human rights record na ni nchi isiyokuwa na mwenyewe.

Slaa anasema yeye amekuwa padri hivyo hana kisasi na mtu na siasa haiwezi kumfanya awe na kisasi na mtu, kama padri wa kikatoliki anakumbuka biblia inasema nini, anajua theolojia hivyo hawezi kuwa na kisasi na mtu. Amesema mawasiliano ya kawaida na Gwajima yapo ila hayawezi kuwa kama kipindi kile.
 
Habari waungwana,

Leo anahojiwa balozi mteule, Dr. Wilbroad Slaa kuhusu maisha yake ya kisiasa, kikanisa hadi sasa balozi mteule, kuwa nami nikujuze..
Lori lake lilikamatwa na cocaine tani tano na lilikaa polisi kwa miaka minane
 
Mheshimiwa Dr Wilbrord Slaa yupo Live ndani ya Clouds 360.

Stay tuned
 
Si Alimegewa mkate wake kisha akakimbia Canada. Leo ana kipi kizuri cha kutueleza mpk tumsikilize
 
Dr Mihogo anababwaja tu....

Anaenjoy kulipwa pesa za ubalozi wakati hana kituo cha kazi alichopangiwa!

Anazitafuna pesa zetu za walipa kodi!
 
Ameulizwa kwa nini awali hakuwahi kusifia utendaji wa Magu hadi alipoteuliwa kuwa balozi?
 
Anabwabaja tu....

Aeleze ni kituo gani cha kazi alichopangiwa cha ubalozi.

Anakubali kulipwa pesa za walipa kodi kwa nafasi hiyo ya ubalozi bila kuifanyia kazi!
 
Leo tarehe 06/02/2018, Dr. Wilbroad Slaa anaongea na Clous Tv, hakika namwelewa sana huyu mzee.

Kuna kitu kimoja amesema huyu mzee kuwa aliwahi sema kuwa aliamua kuacha siasa za vyama vingi ambazo ni siasa za uvuguvugu. Hivyo yeye hajawahi tangaza kuacha siasa.

Anakili kuwa yeye kwake siasa ni maisha hivyo kumwambia ameacha siasa ni sawa na kusema aachane na maisha. Kimsingi anadai kuwa siasa ni maji, siasa ni elimu, siasa ni chakula, siasa ni biashara na kila kitu unachofanya.

Kwa kauli yake ya kuwa ANAACHANA NA SIASA ZA VYAMA VINGI (opposition parties) kwangu naichukulia hii kauli kama ni kauli ya kuomba CCM, wapime kwa namna yeyote kama anafaa kuwa mtu mhimu kuongoza chama na nchi kwa huko mbeleni.

Kusema kweli upo uwezekano kama yeye binafsi atapenda kujijenga katika CCM, msije shangaa siku moja akawa rais wa jamhuri kupitia CCM.

Hii ndoto yangu ipo wenda ikaja timia na kila mtu atabaki mdomo wazi.

Wenye mtazamo wenu, naomba mawazo yenu.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom