Dr Slaa azidi kuitia kiwewe CCM

Kamwe haki haichangamani na dhuluma. Mtetezi wa haki za wanyonge always ataungwa mkono na majority,

Mkuu winner na ndiyo maana Dr Slaa anazidi kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania.Yeye ndiye mwanasiasa anayependwa zaidi katika Afrika Mashariki.
 
Last edited by a moderator:
ccm wameishiwa mbinu za kutawala nchi kisiasa; halafu hili neno la mwenyekiti kikwete kuwakataza ccm kuitumia polisi limekuwa ni mwiba mwingine kwa magamba, hali ikiendelea hivi kwa miezi sita, ccm ndio basi tena. imagine kila shambulizi la ccm kwa chadema halidumu zaidi ya wiki moja, zaidi linaipaisha chadema, watu wanazidi kuikubali chadema na kamanda Slaa...mwacheni nape aunyeunye,
 
Mkuu 50thebe maneno kuntu haya.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu winner na ndiyo maana Dr Slaa anazidi kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania.Yeye ndiye mwanasiasa anayependwa zaidi katika Afrika Mashariki.

Siasa za kuchafuana zimepitwa na wakati kwa kuwa watanzania wa sasa tuna uelewa mkubwa mno,
Kazi kubwa kiongozi ye yote ni kuwaletea wananchi maendeleo, kuacha ujangili,kupunguza anasa za serikali,kuboresha afya, kufufua viwanda, kutengeneza ajira, kuboresha elimu, na siyo kutumia nguvu zinazotumika sasa hiv kuhangaika na Slaa au CDM. kamwe Majungu si Mtaji.
 
nape kamchokoza kipenzi cha watanzania,ona majority walivyoamka na hisia kali dhidi ya magamba
 
Dr Kawashika CCM pabaya, sasahivi walilala wanamuota ndoto, wanaweweseka na wanamgwaya! Hawana raha. Jamaa ana akili sana huyu, sasa akili zao ndogo zitawezaje kudhibiti akili kubwa kama ya Dr. Slaa?
 
kwa kweli nimeamini kuwa ccm hawamuwezi Dr Slaa kwani mpaka sasa wameisha tumia makatibu wakuu 3 kupambana na Dr Slaa lakini wote wamepigwa tko kuanzia Makamba,Mukama na sasa Kinana.Nimeamini kuwa Dr Slaa ni kiboko yao.
 
Hizi siasa wanazo Fanya CCM hazifanywi mahali popote pale Duninian, yaani zinafanywa na CCM pekee, hizi ni saisa za Ajabu za kutumia fedha za walipa Kodi zilizo ibwa na kuzitumia kuwahonga, watu, Nenda Kenya nenda Uganda hakuna Siasa za aina hiyo kabisa

umenena mkuu
 
kwa kweli nimeamini kuwa ccm hawamuwezi Dr Slaa kwani mpaka sasa wameisha tumia makatibu wakuu 3 kupambana na Dr Slaa lakini wote wamepigwa tko kuanzia Makamba,Mukama na sasa Kinana.Nimeamini kuwa Dr Slaa ni kiboko yao.
Landala hapo ndipo ninapoamini Dr Slaa ni tishio kubwa
 
Last edited by a moderator:
:plane::plane: I FELT SORRY FOR MYSELF BECAUSE I WAS RAGED SHOES UNTIL I MET A MAN WITH NO FEET.

TUMSAMEHE nAPE KWA SABABU siyo kosa lake,

DR SLAA HASHIKIKI
 
Magamba yana shida sana safari hii yani hawana pa kukimbilia kila kona kimenuka! pia hawaachi kulitaja jina la DR.. KILA WAENDAKO Chezea DR slaa... wewe viva CDM!
 
Dr Slaa ni mwanasiasa atakayekumbukwa daima na vizazi vingi sana vya Tanzania, sio kwa kuwa mwanaChadema la hasha bali kwa weledi wake, huruma, ukweli na jitahada zake za kumkomboa Mtanzania. Dr amekuwa mstari wa mbele kuweka maslahi ya Taifa mbele na kuonyesha uongozi uliotukuka ndani na nje ya chama chake. Ametetea rasilimali na mali asili za Taifa bila kuchoka katetea wanyonge na katetea wanaoonewa na kudhulumiwa bila kujali vyama vyao.

Ni Dr aliyewaonea huruma wenye nyumba za Tembe ndiye aliyeona EPA ndiye aliyeona ubadhirifu wa madaraka mabaya ya viongozi wetu.

Kutembea barabarani na kusema Dr amelipia kadi ya CCM ni uhuni na ujinga mkubwa. Wana CCM wanaonyesha wazi walivyotayari kuidhalilisha katiba yao kwamba hawaifuti ili kupata maneno rahisi mtaani. Kwa siasa za Tanzania ambazo itikadi na falsafa wala miiko na katiba hazifuatwi ndio maana maneno ya kipuuzi yanaweza tawala.

Chadema hakiruhusu mtu mwenye vyama zaidi ya kimoja. Dr ni mwachama chadema na wanaCCM wakiongozwa na Nape kusaidia na kundi njaa la ndani na nje ya CCM wanafanya siasa taka tu.

Tunaingia mtaani wenye nchi kuhakikisha chadema inaingia ikulu 2015.
Tunawatangazia watanzania wasichoke kuwabeza walioifilisi nchi kwa propaganda za kutengeneza.

2015 ni ikulu tu hakuna wakutuzuia hata wawahonge mamluki laki moja.

Tumejipanga, tunajua hamtakufa kirahisi na tunajua roho itawatoka mkiwa mmechoka sana.
 
Back
Top Bottom