mzamifu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2010
- 6,410
- 3,876
uwezo wa akili wa mtu unaathiriwa sana na aina ya makuzi aliyokulia. mtu aliyekulia katika utamaduni wa "zidumu fikra za ... " ni vigumu kuukiuka utamaduni huo. mtu anaweza kuheshimika kama atachukua msimamo tofauti na kuutetea msimamo wake na pia kukubali watu wengine watofautiana naye. Ingawa Dr. anachukuliwa na baadhi ya watu kwa muasi kwa kuachana na useja/ukasisi mimi naona msimamo wake ni kuonyesha tofauti kimtizamo na kurudi kwenye asili( nature) bila kuutukana mfumo alioukimbia. Pili Dr Slaa alikulia ndani ya mfumo wa "zidumu fikra .. " lakini akaamua kuuacha na kuingia katika mfumo "mabadiliko ni lazima" na wale wahafidhina wametumia misimamo hii ya Slaa kama uasi lakini Slaa amesimama kidete na falsafa zake. hataki kugeuka jiwe. watu wengine wanakanyagwa na kumiywa ndani ya mfumo wa kihafidhina lakini wanajikaza na maumivu na kusema "tuko pamoja" bila kupaza sauti kama Dr. Slaa. Kama tunataka kuendelea ni lazima tuchukue misimamo ya kimapinduzi na kimaendele na kuitetea bila kutukana, kukejeli n.k. bali kujenga hoja kuntu. Hotuba ya Dr ni dira mpya kwetu na msimamo wa mataifa kama ya kwetu kama kweli tuko objective na sio kuponda tu kwa vile aliyesema hayo hatumpendi!